Thursday, July 3, 2014

JACKLINE WOLPER KWA HILI TUNAKUPONGEZA...





Wakati kesi nyingi za unyanyasaji wa wafanya kazi wa ndani (housegirl) zikiwa zimepamba moto, msanii wa maigizo mwenye mvuto hasa JACKLINE WOLPER jana usiku kaonyesha mashabiki wake kupitia instagram jinsi anavyoishi vizuri na mfanya kazi wake na katika kumtambulisha alianza kwa kusema dada yake wa nyumbani ambaye pia ni marafiki, lakini kama hiyo haitoshi Jackie alirusha video inayoonyesha yeye na dada yake wa ndani wakifurahia maongezi juu ya movie, kwanza kabisa movie ile inaonekana ni dada ndo aliyokua anaipenda hivyo Jackie akawa anamuuliza dada amwambie jinsi anavyopenda movie hizo za kihindi, ingekua boss mwingine kwanza unapata wapi muda wa kukaa na ku tviika? halafu uangalie movie unayoitaka wewe boss wako awe anakuangalia tu weee, yani boss akitaka discovery chanel inabidi uminye tu kwa maboss madikteta, anyway kuna siku za nyuma niliwahi kumshuhudia Wolper akiwa na mfanya kazi wake wa ndani kwenye tamasha moja hivi Giraffe hotel, yani nilipenda sana jinsi alivyokua close na house girl wake, yani yule housegirl alikua huru mno kwa Wolper, kwanza kwa mara ya kwanza sikujua hata kama yule binti ni mfanya kazi nilijua ni rafiki wa Wolper.

KWA HILO MCHAGA MWENZANGU NAKUPONGEZA SANA, NAJUA MENGINE HUWA NAKUKOSOA SANA HUMU LAKINI KWA HILI JACKIE HONGERA SANA, MABINTI WENGINE WAKISHAKUA MA STAR BASI HAWAWEZI HATA KUKAA KOCHI MOJA NA MFANYAKAZI, HONGERA SANA JACKIE NA MASTAR WENGINE IGENI MFANO SIO TUWASIKIE MNASHTAKIWA KWA MAKOSA YA KUNYANYASA WAFANYAKAZI KUMBUKENI  JOYCE KIRIA IS WATCHING YOU OOOOO, mkinyanyasa tu mnawekwa wanawake live Tanzania nzima tunawaona.

No comments: