Saturday, May 10, 2014

TUYACHAMBUE MAHOJIANO YA JACKLINE WOLPER






Kwa ambao hawajaona hii ndo show ya Sporah ambapo week hii walimuhoji muigizaji classic Bongo movies Jackline Wolper,

Jackie kama kawaida yake alipendeza mno kuanzia kichwani mpaka kwenye nguo, kiki fashion huwa anamtendea haki sana Jackie,

KUHUSU ALIYOHOJIWA,

Jackie alijitahidi kujibu maswali vizuri sana hasa swala la soko la filamu pamoja na wasambaji wa filamu aliliongelea vizuri.

ALIPOBORONGA.

 Bwana aliniua pale alipoulizwa kama amewahi kwenda kwa mganga akasema hajawahi ila hajui huko mbele akiwa kwenye ndoa labda anaweza kwenda, hivi kabisa mkristo unayeenda kanisani unaweza ukajibu hivyo jamani, yani swala la mganga kwa mkristo yeyote ni mwiko eti alisema anaweza akaolewa na mume anayependa kwa waganga hivyo akamfanya na yeye aende,jamani jamani, Jackie kama ulivyosema umetokea katika familia ya dini naamini uganga ulitakiwa usiuuweke kabisa, jibu simple lilikua ni mimi naamini kwenye maombi siamini uganga, hilo ndo jibu la mpenda dini yeyote.

Akaulizwa kama ni hela za movie ndo zinazowafanya wa shine Jackie akasema hapana ma boyf huwa wanawasaidia kwa kiasi kikubwa wenyewe kushine, yani hela za maboyf ndo zinazowa shinisha, jamani tuko kwenye dunia ya kuwahimiza wanawake wasimame wenyewe na watoto wadogo wanaowaangalia huwa wanataka kua kama nyie wakiamini mmesimama kwa miguu yenu sasa ulipojibu vile mbele ya watanzania wote kwakweli haiwafundishi watoto vizuri, yani mtu kama Julia Robert au Angelina hawezi kujibu namna ile hata Genevieve. sasa hata kama ukianza kushine kwa hela zako mwenyewe watu bado wataamini huwezi ishi bila kuhongwa,

KINGINE KINACHOLALAMIKIWAGA NI HIKI........

Kingereza cha kubeep jamani ni too much, yani mkisikiliza hyo interview mpaka inakera, haikatazwi kuchanganya lugha mbili lakini kama utachanganya na ukatiririka vizuri kama WEMA SEPETU inapendeza lakini sio sentensi unaianzisha kwa kingereza halafu unashindwa kuimalizia unaingiza Kiswahili yani mpaka neon linakua halina maana, mf  ( nikasema lemmi niende kanisani) mh mh mh haipendezi nahisi tungekua kama NANCY SUMARI huwa hana papara kwenye interview anajishusha na anaongea lugha moja mpaka mwisho na sio kwamba kingereza hajui anajua sana tu,kingine ni Jackie akiulizwa swali moja linachukua dakika mbili kujibu, kwanza sauti ya minato mno ila akijisahau anaongea kawaida akikumbuka tena anarudi kwenye minato, swali moja mpaka aseme aaaaam mmmmh oooh okay oh come on, oh my God, yani hapo watu ndukiiii maana wengine wako busy sana







ZAIDI YA HAPO HAKUNA KINGINE, MCHAGA MWENZANGU ALIPENDEZA SANA, NAPENDA SANA KA DIMPLE KAKE NA MACHO YAKE UWIII NISISAHAU JACKIE ANANGOZI LAINI MNO YANI NILITAMANI ASEME ANAPAKA MAFUTA GANI ILA HAKUSEMA, NGUO YAKE ILIMKAA SANA SANA.

2 comments:

Anonymous said...

mnuka uchi hana lolote

Anonymous said...

Shule na ustaarabu vinahusika, siku nilivyo watch hiyo sehemu ya uganga nilichoka kabisa nikastop kuwatch nikajisikia aibu sana na huzuni.