Saturday, May 24, 2014

ACTRESS WA BONGO ANAYEFANAN NA RIHANA HUYU HAPA.

           SABBY ANGEL                                                          RIHANA
Kwenye hii picha they realy do fanana,

Anaitwa Sabby Angel au Sabrina, niliwahi kumtoa humu ila nilikua bado sijaangalia movie yake, sasa nimeiona movie aliyoigiza, kaigiza movie na Ray inaitwa HARD PRICE, hiyo movie ndani yake yupo Ray na Jackline Wolper, niseme ukweli kwa nilivyoona mimi huyu dada kamfunika Wolper kwenye hiyo movie,  sehemu aliyocheza mpaka nikasema kamfunika Wolper ni ile sehemu ya ujauzito akawa anahangaika akahifadhiwa na mama mpika gongo, mikiki aliyokua anaipata kwa mama mpika gongo ya kufukuzwa hovyo na maaskari yani kwa ufupi sehemu nzima ya shida kaicheza ipasavyo, na mi huwa nikiona mdada mrembo huwa napenda kuangalia kama ataweza kumudu sehemu zile za shida au sehemu ngumu ngumu, hizi nyepesi za kuvaa kupendeza kua demu au mke wa mtu kuigiza mapenzi hizi rahisi mtu yoyote anacheza,  KINGINE NILIFWATILIA INTERVIEW YAKE MOJA KWA JINSI ALIVYOJIELEZA ANAONEKANA ANAMALENGO NA KAZI YAKE, KAMA YALE KWELI NDO MALENGO YAKE BASI ATAFIKA MBALI.

No comments: