Friday, May 9, 2014

MARTIN KADINDA AUZUNGUMZIA UGOMVI WA KAJALA NA WEMA SEPETU

Martin ambaye ni Manager wa muigizaji Wema Sepetu leo ameamua kutoa tamko rasmi kupitia ukurasa wake wa IG kuhusiana na ugomvi wa hao warembo hapo chini.
Martin amesema kwamba anashangazwa sana na huu ugomvi wa Wema na Kajala unavyozidi kuchochewa kwenye social media, ni kweli hawa watu wametofautiana kidogo lakini ugomvi huo si mkubwa kiasi cha watu walivyoukuza, pia amesema itakapofika muda wawili hawa watakaa na kuyazungumza na kuyamaliza lakini kwa sasa kila mtu anahitaji space kidogo, pia Martin amesema endless fame ambayo ni company ya Wema haijawahi kuzungumzia chochote kuhusiana na ugomvi huo na wala haijawahi kusema kisa cha ugomvi huo nini na wenyewe wanasikia tu kwenye ma instagram watu wanavyochochea kua chanzo cha ugomvi ni mwanaume na mambo kama hayo, Hayo ni machache tu mengi yako kwenye page yake





No comments: