Monday, May 12, 2014

HII HABARI KUHUSU KACKLINE WOLPER NI YA KWELI AU?






Mbovumbovu za staa! Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe anadaiwa kuwa tilalila na kujikuta akipiga mwereka kwenye shughuli ya kibao kata cha mwigizaji mwenzake, Vanita Omary





Kwa mujibu wa ‘shushushu’ wetu aliyekuwa ndani ya nyumba, tukio hilo lilijiri kwenye Ukumbi wa PG Hall (zamani FM Club), Kinondoni jijini Dar ambapo mastaa kibao walihudhuria.

Ndani ya kibao kata hicho, Wolper alicharuka kipombepombe kwa kucheza ovyo na kukimbiakimbia akiwa tilalila.
Katika kukimbia huko, ndipo akapiga mwereka na kuanguka huku akijaribu kusimama kwa kuchechemea.
Baadhi ya wageni waalikwa walibaki wakimshangaa na kusema kuwa hapendezi akinywa pombe kwani ustaarabu wote unapotea.
Mbali na pombe pia alikuwa kivutio kwa staili ya ukataji wake wa mauno akiwa na kivazi kilichoacha nje mapaja yake akiwa na rafiki yake aliyetajwa kwa jina moja la Vivi.


MH HIVI HAYO MANENO YA MWANDISHI NI YA KWELI AU WOLPER TU ALIKAA VIBAYA NGUO YA NDANI IKAWA NJE NDO WAKAAMUA KUITUMIA HYO PICHA KAMA KADONDOKA, anyway KAMA NI KWELI KWA KWELI HII INASHUSHA SANA HADHI YA U STAR, NA TUKIWEKA USTAR PEMBENI HII PIA SI NZURI KWA MWANAMKE YEYOTE.   mi mshamba mwenzanu mpaka leo sijui nasikiaga tu vibaoo kata lakini sijui ni nini, na wakienda watu wanafanyaje, na dhumuni la kibao kata huwa sijui ni nini, ila naona watu wengi wanapenda inaelekea itakua ni kitu kinachonoga sana, basi mastar mkienda ndo msilewe mpaka kesho muwekwe front page chupi ikiwa nje ni aibu kwa wazazi wenu jamani.

No comments: