Kijana wetu mwenye Baraka zote kutoka kwa Mungu na kwa mama tunampa hongera sana kwa kuchaguliwa kushindania kipengere cha BEST INTERNATIONAL ACT AFRICA kwenye tuzo kubwa za Marekani B E T awards, uwiiiii jamani mwenzenu mpaka nataka kulia kwa furaha, kwa jinsi ninavyompenda huyu mtu leo hii kumuona kafika mbali kiasi hiki inatia raha sana, FROM TANDALE TO B.E.T AWARDS yani hata wale from MASAKI wanaisikia B.E.T kwenye radio, kijana anakwenda kusimama kwenye carpet moja na wakina Jay zee, Kanye,Future o.m.g, ila usisimame karibu na SOLANGE tu usije ukarudi na manundu bure almasi wetu.
kilichonivutia ni kwamba Africa mashariki nzima ni Diamond tu ndo kachukuliwa, (PREZZO UPO BABA) .
ZAMU YA WEMA SASA
Hakuna asiyejua kwamba Wema ni mchumba wa mwanamziki Diamond hapa Africa mashariki, na pia hakuna asiyejua kwamba mastar pekee wenye mashabiki wengi TZ ni hawa wawili, na swala hilo ndo lililomfanya Diamond kuchukua tuzo saba kwasababu mashabiki wote wa Wema walimpigia Diamond kura, kwa wale waliosema kapendelewa nendeni na b.e.t mkalalamike,
Wema unastahili pongezi kwa kila mafanikio ya Diamond kwa sababu ulianza nae kipindi Diamond anatembelea VITZ yess nakumbuka vizuri, kipindi hicho watu wanakucheka unatembea na motto wa tandale sio hadhi yako, lakini wewe moyoni ulikua unaamini Diamond atafika mbali na ukasimama nae hivyo hivyo japo watu walikua wanakuponda.
WEMA SASA NI ZAMU YAKO NA WEWE KUFANYA KIPAJI CHAKO KIJULIKANE KIMATAIFA KAMA BABY WAKO ANAVYOFANYA, sio kumpangia tu Diamond nguo kwenye mabegi na kumsindika airport hapana, sasa hivi na wewe amka, usijisahau kama na wewe ni msanii na unatakiwa ufike mbali, wewe bado mdogo, unamiaka nadhani 25, kama lupita na miaka 31 kafanikiwa kutikisa dunia na ametoka hapo Kenya basi na wewe ambaye miaka inaruhusu zaidi inawezekana, upo pembeni ya Diamond, piga chabo anafanya nini kufika alipofika na wewe ufuate nyayo zake, muangalie KIMORA LEE alivyofanya wakati yuko na RUSSEL SIMON na wewe
unatakiwa ufanye hivyo, ukikaa na mwenye mafanikio hakikisha na wewe unapata mafanikio,
Hatusikii kazi zako sana kama tunavyosikia uhusiano wako na Diamond, sasa hivi hakikisha unajitangaza vya kutosha nje ya nchi, ukiwa na hela maswala ya private jet mpaka Arusha na kula bata hapana sasa ni vyema ukaifanyia kazi ya maana funga safari hata mpaka Nigeria fanya kazi nao kwasababu wenzetu wamefika mbali itakusaidia na wewe, fanya kama marehemu Kanumba, hapa Bongo hakuna star kama wewe, unajielewa na ni mzuri hasa na umetoka kwenye familia inayojielewa,
na kwenye BET jamani si wanaendaga mr and mrs Wema usikose ati, usikubali hata siku moja Diamond ang'ae peke yake ng'aeni wote yani hili liwe kama shindano kwenu nyie wawili kila mmoja afanye kazi zaidi ili kumshinda mwenzake kama Jay zee na Beyoncé,
Pleese Wema usimuache Diamond atumie hii nafasi peke yake, anza na wewe, movie za bongo umeshacheza sana sasa songa mbele, wewe ni mzuri, anza kufanya diet urudi uwe kama miss Tanzania 2006 au pungua hata kidogo tu, na hivi huna kingereza kama cha Fulani chako wewe kimenyoooka basi hata ukicheza movie na Hollywood mtaenda sambamba, ni hayo tuuu
DIAMOND HONGERA SANA NA WEMA HONGERA SANA MANAKE DIAMOND AKIWA NA WEWE TU NDIO HUWA ANASHINE.
2 comments:
ushauri mzuri sana wema please wake up my dear
Umemaliza yote hv huwa anapitia huku
Post a Comment