Friday, October 18, 2013

YOU DEFENETLY NEED TO WATCH THIS SHOW

Reality show mpya ya huko Marekani inayoitwa PREACHERS OF LA. Hii show imeanza kurushwa na kituo cha television cha OXYGEN Oct 9 mwaka huu, inaelezea maisha ya WACHUNGAJI 6 vijana wa huko Marekani.

Yani maisha ya kifahari wanayoishi hawa wachungaji mbona unaweza ukaacha yote ili uwe mchungaji, wake zao wanavyotanua ni balaa, kwa kifupi kama mnavyoona maisha ya wakina Jay zee na hawa majamaa wanajiachia vile vile, magari ya kifahari, majumba, yani kila kitu the same. Show hii imeandaliwa na LEMUEL PLUMMER & HOLLY CARTER ambao ni watoto wa wawachungaji. sasa ngoja nikupe majina na wasifu wa hawa wachungaji watano watakaoshiriki kwenye hii show.
 
                                                   MCH. CLARENCE MACLENDON

Huyu ni mchungaji kijana mwenye mafanikio makubwa, aliamua kukubali kujiunga kwenye hii show ili kutoa nafasi kwa waumini wao kuona maisha halisi ya wachungaji wao.

                                               MCH. DEITRICK HADDON
Deitrick yeye alianza kazi ya kuhubiri neon akiwa na umri wa miaka 13, na alipofikisha miaka 23 alioa ambapo baada wakaachana na mke wake, na pia anamtoto aliyezaa nje ya ndoa na mwanamke mwingine.
 
 
                                                MCH. JAY HAIZLIP
 Huyu aliwahi kua muathirika wa madawa ya kulevya kabla hajawa mchungaji na pia ana tattoo sita alizichoraga Enzi zake za usela.

                                                    
                                                  MCH. NOEL JONES
Huyu baba mchungaji yeye alizaliwa huko Jamaica kwenye familia ya kimaskini, baadae akaamua kua pastor huko LA, upastor ukamtoa, sasa anampango wa kustaafu ila anapata shida sana kumpata wa kumshikia kazi.
 
 
                                                MCH. WAYNE CHANEY.
Huyu alipata wito wa uchungaji akiwa kijana wa miaka 20 tu , akaanza kuhubiri kwenye kanisa alilolijenga babu yake na mpaka sasa anawaumini wengi sana.
 
MCH. RON GIBSON
Huyu Enzi hizo hana dili yupo kitaa alikua mtumiaji mzuri sana wa madawa ya kulevya na ukipita kwenye 18 zake pia anakuibia vilevile, sasa hivi ndo kaacha hayo yote na kua BABA MCHUNGAJI.
 
 
 
 
 
Angalia hii show kupitia OXYGEN TV ili upate kujionea mwenyewe. kila kitakachoonyeshwa huko ni ukweli mtupu yani ndo maisha yao ya kila siku, no acting, na wachungaji they are real sio actors.
 
 
 
 
 
 
 

1 comment:

TANZANITE MOVIE said...
This comment has been removed by the author.