Friday, October 11, 2013

WASANII WA MAARUFU WA NIGERIA WALIOAGA DUNIA MWAKA JANA NA MWAKA HUU

Wengi tunazipenda movie za Nigeria, na tunaziangalia mara kwa mara lakini hatujui maisha halishi ya wasanii hao na pia kuna wengine tunaangalia movie zao kumbe tayari walishaaga dunia, inakua ni vigumu kugundua kwasababu mara nyingi tunafwatilia habari za wasanii wetu wa movie (mcheza kwao hutunzwa), hivyo basi nimeona nikujulishe wasanii waliotutoka hivi karibuni wa Nigeria naimani kwa wale waliokua hawajui nitakua nimewasaidia kujua jambo hili.

1. huyu ni ENEBELI ELEBUWA. nadhani wengi mmetazama movie za huyu baba, alikua anajua sana kuigiza, akiwa IGWE lazima kijiji kinoge, lakini kwa bahati mbaya alifariki mwaka jana nchini India kwa maradhi ya kupooza nusu ya mwili wake akiwa na miaka 66.

                                              ENEBELI ELEBUWA

2. Huyu ni David Ihezie. na yeye nafikiri wengi wanamfahamu, baba huyu alikua ananoga sana kwenye nafasi kama za uzee wa baraza wa IGWE, yani akicheza kama mshauri wa IGWE lazima kijiji kipate maendeleo. kwa kweli atakumbukwa daima.

                                                           DAVID IHEZIE
 
 
3. Huyu ni Sam Loco, baba huyu mara nyingi anaigizaga kama baba mtata sana, au anaigizaga sehemu za vichekesho chekesho. kwa kweli wengi watamkumbuka sana.
 
SAM   LOCO
 
4. Huyu baba huwa anasura ya upole, na huwa anapewa nafasi za kua baba au igwe mpole, sasa kimbembe kinakujaga akicheza kama mume wa MAMA G (Patience Ozokwo), yani huwa anaonewa na yule mama mpaka basi, ila ndo hivyo hatutamwona tena kwenye movie manake ameshaaga dunia.
 
                                                         PETE ENEH
 
5. Huyu mzee anaitwa Justus Esiri, mzee huyu kwakweli huwa anajua kuuvaa uhusika wake, yani tena akicheza kama baba yake Ini Edo au Rita Dominic, halafu awe ni baba mtata kwa hao mabinti zake mbona utafurahi.
 
JUSTUS ESIRI
 
Kwa kweli inauma sana kuwapoteza waigizaji kama hawa  ndani ya mwaka mmoja na nusu,walijizolea umaarufu na pia walituburudisha sana kutokana na uigizaji wao. MUNGU AZILAZE ROHO ZAO MAHALI PEPA PEPONI. AMINA
 

No comments: