LELETI KHUMALO AU SARAFINA
Picha hii ya chini ndio SARAFINA anavyoonekana sasa, bado mrembo vile vile
LELETI KHUMALO AU SARAFINA
Hapa kwenye picha ya chini ndo cover la movie ya sarafina, hapo akiwa na mwigizaji bei mbaya wa Hollywood WHOOPI GOLDBERG. kumbuka kwamba kwenye movie licha ya Whoopi kuwepo, pia MIRIAM MAKEBA ambae ni marehemu sasa nae alikuwepo pamoja na DUMISANE.
Sarafina aliolewaga na msanii mwenzake aliyeigiza nae kwenye hii movie lakini waliachana inasemekana yule mwanaume alikua na uhusiano na wanawake wengi na pia alishakua na uhusiano mpaka na marehemu BRENDA FASIE. lakini sasa sarafina ameolewa tena na mfanya biashara maarufu wa huko South, na hii picha hapa chini ni ya siku ya harusi yao mwaka jana.
hayo ndo maisha ya muigizaji huyu aliyejizolea umaarufu mkubwa sana Enzi za miaka ya 90, Enzi hizo kila motto alikariri nyimbo za kwenye movie ya sarafina, na wengine mpaka step za kucheza walikariri, movie classic kama hizi ntakua nakuletea mara kwa mara ili tukumbukie Enzi.
No comments:
Post a Comment