huyu ndio muigizaji EVA MENDES
sasa bwana, huyu Eva na kijana wa watu Ryan wanamiaka miwili toka uhusiano wao uanze, na walianzisha mahusiano wakiwa wana shoot movie pamoja hiyo movie inaitwa THE PLACE BEYOND THE PINES. Ryan akaona kampata mwanamke wa kutulia nae, miaka miwili imepita na Ryan anataka kuwa na familia sasa, kimbembe ndo kikaja hapo, inasemekana Eva Mendes yeye huwa hataki kuzaa wala kuolewa yani ye anapenda maisha ya uboyfriend na u girlfriend tu, bila kusahau huyu mwanadada anamiaka 39 sasa, basi wakawa na vurugu za hapa na pale ndo Eva akaanza kumsaliti kijana wa watu.
Inasemekana kwamba huyu George na Eva waliwahi kuwa na uhusiano kipindi cha nyuma, uhusiano uliodumu kwa muda wa miaka kumi, kwa hyo naona Eva kaona bora arudi kwa yule wa zamani.
NINACHOSHANGAA NI KWAMBA, INAKUWAJE DADA WA MIAKA 39 BADO ANATAKA MAISHA YASIYO NAMUELEKEO, KWA KAWAIDA WANAWAKE WENGI TUNAPENDA KUA NA WATOTO HAPO BAADAE, LAKINI ZAIDI TUNAPENDA KUA NA MWANAUME AMBAYE ATAKUA BABA MZURI WA WATOTO WAKO, KWELI HELA INAHARIBU AKILI. tabia kama hii pia tumeiona kwa OPRA WINFREY ambaye hakupenda kuolewa wala kuzaa anaboyfriend waliyedumu nae kwa miaka 27, na GABRIELA UNION na kenyewe umri umekatupa mkono lakini hakataki kuzaa bado ,,
No comments:
Post a Comment