Thursday, October 10, 2013

MASTAR WAKUBWA WA MOVIE DUNIANI AMBAO WATOTO WAO NAO WAMEKUA MASTAR WAKUBWA DUNIANI


1. huyu ANGELINA JOLIE na baba yake JON VOIGHT. Angelina ameshacheza movie kama Salt, Wanted na the tourist.
                                                         ANGELINA JOLIE& JON VOIGHT
 
2. Huyu ni muigizaji nguli wa india anaitwa Rakesh Roshan hapo pembeni ni mwanae ambae nae ni muigizaji mahiri Hrithik Roshan. motto mtu ameshacheza movie kama Kites na Krish.
 
                                             RAKESH ROSHAN & HRITHIK ROSHAN
 
3. Huyu ni muigizaji wa siku nyingi wa India Dharmendra, pembeni huyo kijana ni mwanae ambae ni tishio kwa uigizaji na ni maarufu sana anaitwa Sunny Deol na huyu binti pia ni binti wa Dharmendra na yeye pia ni muigizaji. Sunny Deol ameshacheza movie kama SHAHEED na AJAY.
 
                                            DHARMENDRA & SUNNY DEOL

4. Will Smith muigizaji kutoka Hollywood na mwanae anayekuja kwa kasi anayeitwa Jaden Smith. Jaden ameshacheza movie kama AFTER EARTH movie hii kacheza na baba yake na pia ameshacheza movie inayoitwa THE KARATE KID.

                                                     WILL SMITH & JADEN SMITH
 
5. Namba tano ni baba wa motto anaye make headline huko Hollywood kwa kudata nae si mwingine ni Billy Cyrus, pembeni ni mwanae Miley Cyrus. baba huyu na mwanae licha ya kua waigizaji pia ni wanamziki wanaokubalika sana. Miley ameshacheza movie kama SO UNDERCOVER na THE LAST SONG.
 
                                                         MILEY CYRUS & BILLY CYRUS


6. Anayefuata ni muigizaji nguli wa tamthilia ya DAYS OF OUR LIVES John Aniston, babu huyu alikuwepo kwenye hii tamthilia toka inaanza mwaka 1965, yani days of our lives ilianza kuonyeshwa mwaka 1965 mpaka leo bado anacheza tamthilia hiyo, jina lake la kisanii kwenye days of our lives ni VICTOR, kwa wale waliokua hawajui, huyu ndie baba wa American sweetheart bibi Janefer Aniston.

                                              JANEFER ANISTON & JOHN ANISTON
 
7. Namba saba inakamatwa na muigizaji na director nguli wa India mzee salim Khan, mzee huyu ni baba wa star matata nchini India Salman Khan. Salman ameshacheza movie kama WANTED, READY na DABANGG.
 
 
                                                SALMAN KHAN & SALIM KHAN
 
8. Hapa ni babu ambaye Enzi zake alikua hakamatiki na alitikisa dunia hasa, huyu si mwingine bali ni MITHUN CHAKRABORTY. Mithun bwana Enzi zake alikua bonge la actor, hivi sasa mwanae nae anashika ukanda, mwanae anaitwa Mahakshay Chakraborty. Mithun ameshacheza movie kama DISCO DANCER, hii movie ilitikisa mpaka watoto walikariri nyimbo za kwenye movie nikiwemo na mimi Enzi hizo,
 
 
                                            MITHUN CHAKRABORTY & MAHAKSHAY CHAKRABORTY
 
9. Wa mwisho ni aliyekua mpinzani mkubwa wa Mithun Chakraborty Enzi hizo nae si mwingine ni Amitah Batchan,  Amitah naye anamtoto wa kiume ambaye ni star mkubwa sana wa movie huko Bollywood anayeitwa Abhishek Batcha, Amitah ameshacheza movie kama SHOLAY, hii movie aliichezaga na Dharmendra, ilikua matata sana aisee, na pia motto huyu wa Amitah ameshacheza movie kama SAKAR, movie hii kacheza na baba yake, pia kacheza KUCH NA KA HO, RUN, DHOOM na BUNTY & BUBLY.
 
ABHISHEK BATCHAN & AMITAH BATCHAN
 
Kweli unaambiwa maji hufwata mkondo, unapokua upo kwenye fani Fulani hasa mambo ya sanaa, ni rahisi sana watoto wako kufwata, tumeona wanamziki wengi watoto wao wamerithi kazi zao, waigizaji na hata wacheza mpira. Vijana ni vizuri kujiangalia nini tunafanya kwenye maisha yetu ili watoto wetu waje warithi mema na si mabaya.

No comments: