huyo hapo juu ni WEMA SEPETU, huyu binti ni muigizaji wengi mnamjua manake ndo muigizaji top hapa Bongo, sasa Wema huwa anajulikana kwa kutokua na kinyongo na wenzie, hata akigombana nao huwa wakimuomba msamaha anayamaliza mpaka moyoni japo wenzie bado wanakua na unafki juu yake.
Wema kama mnavyojua anamahusiano ya kimapenzi na mwanamziki ambaye na yeye ni top hapa Bongo anayeitwa Diamond. HII PICHA HAPO CHINI NI SIKU YA KWANZA KABISA WEMA NA DIAMOND KUONANA NA KUANZA MAPENZI YAO RASMI MWAKA 2010 KIPINDI HICHO DIAMOND HANA KITU.
Basi bwana kwenye mapenzi kuna mikwaruzo Wema na Diamond wakagombana wakaachana na Diamond akaanza kutoka na rafiki wa karibu wa Wema anayeitwa Penny ambaye ni mtangazaji wa TV. kutokana na jambo hilo Wema na Penny wakawa maadui.
HII PICHA HAPO CHINI NI DIAMOND NA PENNY
DIAMOND NA PENNY
Mungu si athumani , miaka imeenda Wema na Diamond wamerudiana na wamewaacha wale wapenzi wao wa zamani, sasa bwana, toka wawili hawa wamerudiana wale waliochwa yani Penny na clement aliyekua bwana wa Wema wamekua na vinyongo na watu hawa, lakini wamemudu kukaa kimya na wawili hawa wanaendeleza mapenzi yao ambayo ni kivutio cha wengi,
NA HII PICHA HAPA CHINI IMEPIGWA JUZI TU NA WAMEITUNDIKA KWENYE MTANDAO WAO WA INSTAGRAM
WEMA NA DIAMOND
Wema anayerafiki yake mkubwa mwenyewe huwa anamuita dada kabisa, naye ni muigizaji anaitwa KAJALA MASANJA, wawili hawa wamekua mashost hasa kutokana na Wema kumsaidia Kajala faini ya shilingi milioni 13 kipindi Kajala yuko jela, basi wamekua wakiambatana pamoja kila mahali, Kajala ni mwanamke mpole asiyena makuu na mjua vizuri ndo maana naongea hivi, Wema pia hana makuu naye namjua ila tu mara nyingine anakua anabadilika na kua mkali sana lakini kwa moyo anamoyo wa upendo kwa kweli.WEMA NA KAJALA KWENYE PICHA
Sasa bwana hivi karibuni inasemekana kwamba eti Kajala shosti wa Wema kaanzisha mahusiano na aliyekua bwana wa Wema wa zamani Clement, na Kajala kanunuliwa mpaka gari na jamaa huyo, hii imewafanya wawili hao kua na kaugomvi ka chini kwa chini,
HII PICHA HAPA CHINI NI YA JACKLINE WOLPER
Jackline ni muigizaji na yeye, na yeye pia alishakuwaga na uhusiano na Diamond kipindi hicho Diamond hana kitu basi Jackie akaulizwa akamkana Diamond na akasema Diamond sio hadhi yake kisa tu hana hela, hivi sasa naona anamtamani, basi huyu Jackie alishagombanaga na Wema lakini baadae wakapana, na pia Jackie huyu huyu ni rafiki na Kajala lakini kwenye kumdhamini million 13 alijitoa Wema Jakie alikaa pembeni,
NASHUKA NA UMBEA SASA MANAKE NILIANZIA MBALI ILI TWENDENI SAWA.
huko kwenye mtandao wa Instagram vibwanga vimeibuka tena vimeibuka kweli, yani watu ni full kuchambwa, baada ya Jackie kuona Wema na Kajala hawaivi, na ukizingatia Jackie anampenda Kajala kuliko Wema basi unaambiwa Jackie kaununua ugomvi, kwanza kaanzisha ushoga na hasimu mkubwa wa Wema ambaye ni PENNY, eti kila siku Jackie ni anapiga picha huku akijilazimisha kumuhug Penny yani ili waonekane mashoga sana, mara wako club, mara cocktail date , mara hiv mara vile yani ilimradi tu Wema aumie, Jackie kila siku vijembe vya kumwendea Wema, watu wanajiuliza, siku zote walikua wapi kua mashoga Jackie na Penny, baada ya kuona kuna ugomvi ndo wameunga ushoga ili kumkomesha Wema, sasa basi Wema hamjibu mtu yuko busy na mpenzi wake, hii inaonyesha jinsi gani alivyo hana uswahili,
KWA KUINGILIA MAMBO YASIYOMUHUSU JACKIE HIVI SASA ANAPOKEA MATUSI KILA LEO HUKO INSTAGRAM, WENGINE WANAMKUMBUSHA KILA SAA KWAMBA ANANUKA ........, YANI KILA AKIPOST PICHA NA PENNY NI MATUSI TU, JAMANI WADADA KWELI MNAJUNGA MGOMBANE NA WEMA ANAYEPENDWA NA KILA MTU, PILI KWANINI MNAJIUNGA MUMKOMESHE MTU KWANI HAMJUI KABLA HAMJAMKOMESHA MUNGU TAYARI ANAKUA KASHAMPA ULINZI, HIVI HAMKO BUSY KABISA NA KAZI HAPA MJINI MPAKA MNAPATA MUDA WA KUGOMBANA, EMBU ONENI WENZENU NIGERIA WALIVYO BUSY, NYIE NI KUGOMBANIA MABUZ KILA LEO. JACKIE ACHA KUSHADADIA UGOMVI USIOKUHUSU UNAONEKANA MJINGA KWENYE JAMII,
1 comment:
kazi ipo...
Post a Comment