Tuesday, April 15, 2014

MUIGIZAJI JOHARI YUKO JUU

Ray na Johari ni waigizaji wa toka Enzi za kaole, mpaka leo hii ulimwengu wa movie umeshika hatamu bado wako pamoja, watu hawa toka zamani iliwahi kuriportiwa kwamba ni wapenzi, wakaanzisha Company pamoja ya filamu inayoitwa RJ company yani Ray na Johari company.
sasa bwana kwenye mapenzi kuna milima na mabonde, Ray akachepuka kidogo na kua na chuchu ambaye pia ni muigizaji na magazeti nayo yakachachamaa nao kama kawaida na hapa chini ni jinsi magazeti yalivyoshadadia mambo.



Kutokana na magazeti watu tukajua kuna beef zito kati ya Ray, Johari na Chuchu, sasa kwa kuwa Ray na Johari licha ya mapenzi wenyewe ni ma partner kwenye hiyo company yao basi watu wakajua RJ ndo imefika mwisho.

Johari akatoa neno lake la mwisho na kusema yeye hayuko na Ray kama ilivyoandikwa kwenye hilo gazeti hapo chini.

Mpaka sasa nampongeza sana Johari kwa kuweza kutenganisha kazi na mambo binafsi, japo kulikua na tofauti na mwenzake lakini wameweza kusimama pamoja kwenye kazi.

Kilichonifanya niandike hii post ni jana Johari alivyopost kwenye ukurasa wake wa INSTAGRAM na kuwasihi mashabiki kumpigia kura Ray kwenye tuzo za action and cut viewers choice awards ili awe Director bora. johari alisindikiza picha na haya maneno " WANAMUITA  RAY KIGOSI  A.K.A SWAIBA  DIRECTOR  WA  RJ COMPANY  NATUMAI  KAZI  ZAKE  MNAZITAMBUA MPIGIENI KURA"  hakika huu ni ustaarabu ambao mademu wengi hawauwezi, Johari mama, sisi woteee hakuna anayejua wewe na Ray mlisota vipi kuanzisha RJ ni mangapi ulivumilia, kama ingekua mschana mwingine asingekubali kuanza moja na mwanaume kama mnavyojua waschana wa siku hizi wanasubiri mambo yakishaiva ndo amdake mwanaume, wewe ulisimama kuanzia chini, na sasa mnatambulika na mnaongoza vile vile, kulikua na waschana wengi sana lakini kwa kipindi hicho hakuna aliyesimama na Ray ila wewe ulisimama naye mpaka sasa, hiyo pekee inatosha kumfanya Mungu akupiganie, chochote kinachopita kwenye maisha yenu ni misuko suko tu ya shetani lakini mwisho wa siku MVUMILIVU HULA MBIVU. ni hayo tuuuuuuuu





No comments: