Friday, April 18, 2014

WEMA APEWA USHAURI




Hii episode tulionyeshwa Petit man ambaye ni mfanyakazi na rafiki wa Wema akituhumiwa kula hela  za kazi, sasa baada ya watu kuangalia jinsi palivyowaka humo ndani kwa Petit kudaiwa kurudisha hela, kesho yake kwenye mitandao Petit, Martin na Wema wako kawaida tena urafiki kama vile hawadaiani, sasa watu wanauliza, je? Madam ni kweli Petit alikula hela au ile ilikua kwa ajili ya kunogesha kipindi, manake kwa hali ya kawaida kama Petit angekua kala zile million nne sasa hivi magazeti yangekua yanaongelea habari za police tu, na kama ilikua ni nogesha kipindi, Madam ile ni REALITY SHOW, sio movie, watu wanataka kuona kila kitu kikiwa ni cha uhalisia, yani watu wanataka kuona jinsi unavyoishi kiukweli, Madam ni mmoja wa waigizaji wazuri sana Tanzania sasa watu wanaogopa na pale usije ukawa unaigiza, NA PIA  MADAM  KAMA UTASOMA  HII  POST WAPENZI  WAKO  WANAOMBA  SANA  UWE  UNAWAHISHA  KUWEKA  U TUBE  KILA EPISODE  INAPOMALIZIKA  KUONYESHWA  MANAKE  WENGINE  HUWA  WANAKUA NA  RATIBA  MBALIMBALI  NA WENGINE WAKO NJE YA NCHI WANASHINDWA KUANGALIA EATV SASA WANAPONEA U TUBE NA BESTIZO AKICHELEWA KUWEKA INAWAPA TABU, MFANO MPAKA SASA EPISODE 20 SIIONI U TUBE. 

No comments: