Tuesday, April 22, 2014

SPECIAL KWA WANAOMCHUKIA WEMA SEPETU DANGOTE.

                                                      WEMA SEPETU IJUMAA SEXIEST GIRL 2014.

Juzi Wema ameshinda sexiest girl wa gazeti la ijumaa, watu mapovu ya midomo yamewatoka mpaka motto wa watu akaandika ujumbe kwenye insta page yake.

                                TALL N SEXY, MISS TANZANIA 2006  WEMA SEPETU.

Sasa kwa kipindi kirefu huyu mschana anaandamwa, ni kweli kila mtu anamapungufu yake, na Wema anamapungufu lakini anamazuri yake pia, sasa kwa wale wanaojiringanisha na Wema au wale wanaomlinganisha Wema na watu Fulani, kwanza, hivi kuna yeyote kati yao ambaye amewahi kuwa Miss Tanzania. Hata ikitokea wakashinda mataji ya urembo mengine nchini swala litabaki pale pale Miss Tanzania ndo taji kubwa kitaifa la urembo na Madam alishashinda mwaka 2006, NA HATA MIAKA MIA MOJA IKIPITA KWENYE HISTORIA ITABAKI YANI VITUKUU VYETU VIKIANZA KUORODHESHA MA MISS TANZANIA BASI WAKIFIKA WA MWAKA 2006 LAZIMA WAMTAJE WEMA SEPETU. NYIE WENZANGU MTATAJWA MILIKUA MA MISS TANZANIA WA MWAKA GANI?


Ieleweke kwamba Wema Alishapokea taji kubwa la urembo kabla ya kupokea taji la juzi, kwa hyo kwa waliochukia nadhani wangerudisha kwanza miaka nyuma iwe mwaka 2006 wamchambe halafu ndo waje wamchambe na ushindi wake wa juzi, kama mtu alishachukua taji la ngazi ya JUU YA UREMBO NCHINI YANI MISS TANZANIA  sasa jamani taji la juzi si nikitu cha kawaida, alishazoea kuitwa mlimbwende miaka nane iliyopita watu mnastuka sasa hivi.

WEMA SIKU ALIYOSHINDA TAJI LA MISS TANZANIA 2006.
 
MISS TANZANIA 2006 WEMA SEPETU
Huwa nacheka nikiona watu wanamfananisha Wema na Fulani au na Fulani, duniani kila mtu na uzuri wake lakini hata mkisimama wazuri mia moja mzuri mmoja akishinda ndo kashashinda yani mko chini yake, kwa wale mnaomchukia bila sababu leteni picha zenu za u miss Tanzania nizirushe, obviously hakuna mwenye nazo kwa hiyo WOTE KIMYAA in Wema's voice.
Just take a gud luk at her, ukiambiwa u define beauty jibu lake liko hapo juu, umbile zuri la kiafrika, mrefu, rangi nzuri, na moyo mzuri wa kusamehe ndo maana anapendwa sana na watu.

Mkimuona anajichanganya na watu ni kwasababu hapendi makuu huwa anakaa popote na kula chochote na kuongea na yeyote, lakini kama angeamua kunata na kuishi kuendana na hadhi yake, basi ma bibi na mabwana wengi mngekua mnamsikia kwenye vyombo vya habari tu na msingeweza hata kumsimanga na kujifananisha nae.
Ohhhhh Wema anapenda attention embu tuweni wa kweli nani hapendi attention anyoshe kidole? mwanadamu yeyote yule kupenda attention ni kawaidia lakini kwa bahati nzuri kwa upande wa Wema anapenda attention na anaipata kweli kweli hiyo attention sasa wengine hata wakipenda attention nani atawapa hiyo attention? no wannnnnn
Ohh Wema ni Malaya, hivi kuna Malaya yeyote anayeweza kumuacha mwanaume anayempa mamilioni na kumfwata mwanaume ambaye anampa mapenzi tu, sijawahi ona, kama Wema alimuacha yule jamaa aliyekua anampa mamilion na kamfwata CHIBU DANGOTE basi ujue huyu ni mschana mwenye mapenzi ya kweli. na naimani Chibu analiona hili kwamba huyu binti kampenda tangu Enzi za mbagala ndo kwanza akiwa kaanza kujilikana tena watu kipindi hicho walimkashifu sana Wema wakasema anatembea na Chibu sio hadhi yake leo hii Chibu kawa mr ngororo kila mtu macho up, Chibu mshike sana huyu binti aliyekupenda ukiwa huna kitu na aliyeacha mamilion na kuamua kutulia na wewe.


Ohhh Wema kaaribika ngozi kajichubua na kanenepeana sana, kwani hamjui kwamba unaweza kuacha kujichubua, na sasa karudia ngozi yake ya zamani, kuhusu kunenepeana, tena bora muombee asiamue kuingia gym manake siku akianza tu kupiga mazoezi basi mjini hapa patakua hapatoshi manake ile shape yake ya Enzi za u MISS TANZANIA ikirudi kutakua hakuna cha Fulani wala Fulani si mnajua wenyewe motto kaajaliwa umbile la haja, kupunguza unene ni kitu cha week moja tu, na hivi ngozi yake imerudi na akipungua kidogo lazima Lundenga amwambie mama njoo gombea tena u miss maana hawa vizazi vipya hakuna anayekupata. kingine, WATU WANAIBUKA WANAKUA MAARUFU NA KUPOTEA LAKINI MRS DANGOTE YUKO PALE PALE, BADALA YA KUMCHUKIA UNGENI TELA MUWE TEAM WEMA MANAKE KILA MNAVYOMCHUKIA NDO MNAVYOZIDI KUMUONGEZEA BARAKA MAISHANI MWAKE.

sina team yeyote na Wema sina ukaribu nae,hayo niliyoongea ni ukweli mtupu, blog inawahusu wasanii wa movie kwa hyo ni ruksa kwangu kueleza chochote ambacho ni cha kweli kuhusu msanii husika. byeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee 





11 comments:

Anonymous said...

nimekupenda bureeeee safi sana umeongea point chukua soda kwa mangi nitalipa

Anonymous said...

U sound very stupid I'm sorry for saying this

Anonymous said...

Yote uliyoongea ni kweli

kibela said...

Kuna watu mmebarikiwa busara looh....aana nmesoma mpk nimesisimka

Anonymous said...

Yaani ungekuwa karibu yangu ningekupa bonge la kiss maneno mazuri sana haya na wameyapata

Unknown said...

Nimekupenda bureeeee

Anonymous said...

ukiendelea hivi utapata umaarufu

Anonymous said...

Nimekupenda bureee blogger

Anonymous said...

Yah uliyosema yote ni kweli kabisa,love u na utagrow sana kwenye carrier yako

TANZANITE MOVIE said...

asante mpenzi, nashukuru sana kwa kunitia moyo.

Anonymous said...

hujielewi wewe sema yako basi