Friday, January 3, 2014

WEMA SEPETU BILA MANGE KIMAMBI TUSINGEMJUA TANZANIA

                                           MANGE KIMAMBI

                                                                      MANGE  KIMAMBI
 
                                              
WEMA SEPETU
 
 
WEMA SEPETU
 
Muigizaji wa hapa Tanzania anayeitwa Wema sepetu ndie muigizaji wa kike maarufu kupita wengine wote, umaarufu wake ulitokana na yeye kushiriki kwenye mashindano ya urembo wa Tanzania na hatimae kuibuka mshindi na kua miss Tanzania mwaka 2006, kitu watu wengi wasichokijua ni kwamba, Wema kuna mtu ambaye alimsukuma sana Wema ili ashiriki kwenye mashindano hayo, mtu huyo si mwingine ni mwanadada ambaye kwa wakati huo alikua ni muandaaji wa mashindano ya miss Dar city centre, dada huyo anaitwa MANGE KIMAMBI, huyo Mange alifanya kila awezalo kumshawishi mzazi wa Wema na Wema mwenyewe ili akubali kushiriki mashindano ya urembo, toka Wema alivyokua miss Tanzania mpaka leo umaarufu wake haujawahi kushuka zaidi ya kupanda kila siku, wamiliki wa magazeti hasa ya udaku wamejipatia hela sana kupitia habari za Wema kwani zikiwekwa tu front page lazima magazeti ya ishe, licha ya hao ma blogger kama sie pia ndo usiseme, habari ya Wema lazima iongoze kwa viewers kuliko nyingine, kwa hyo kila tunapomsifia Wema tusiache kumshukuru Mungu kwa kumtumia huyu dada MANGE KIMAMBI kumfanya Wema kua maarufu, Mange hivi sasa ni mama wa watoto wawili na anaujauzito wa motto wa tatu, ni mke na ni blogger na mjasiria mali anayeishi Marekani.

No comments: