Tuesday, January 14, 2014

USHIRIKINA WAIMALIZA SANAA YA TANZANIA.






Katika pitapita zangu nilikutana na habari inayomuhusu muigizaji Monalisa, alikua anazungumizia jinsi anavyoogopa kulogwa kwenye kazi zake hivyo inambidi awe anaficha baadhi ya mambo yake kama mwaka na tarehe ya kuzaliwa, lakini licha ya hili, pia siku za nyuma msanii mwingine wa kiume wa bongo movie aliwahi kunukuliwa akisema wasanii wanalogana sana na kutumia nyota za wenzao, pia wasanii wamekua wakilalamika kwamba inapotokea mtu akavuma kwenye sanaa basi wengine watenda kwa mganga ili afifie na wengine watachukua nyota yake.
HIVI JAMANI, SASA HII SANA INAKWENDA WAPI? KAMA INAFIKIA HATUA MTU ANAOGOPA KUFANYA KAZI KWA KUHOFIA KULOGWA TUTAFIKA KWELI? KWANZA IKIWA UNAAMINI KULOGWA KILA DAKIKA BASI HAKIKA MAENDELEO HUTAYAFANYA, WOTE TUNAJIFUNZA KUTOKANA NA MAKOSA NADHANI NI VYEMA BONGO MOVIE NAO WAKAJIFUNZA NA KUANZA KUMUAMINI MUNGU NA KIPAJI WALICHOPEWA WAKITUMIE VIZURI NA SI KUCHANGANYA ULEVI NA MAPENZI KWENYE KAZI.



No comments: