tanzanitemovies blog is a blog that gives you the chance to know everything that happens in the movie industry. rahelimacdonald@gmail.com 0713-608524
Thursday, January 23, 2014
HONGERA DIAMOND PLATNUMZ
Diamond ni muigizaji pia ni mwanamziki, nikijana mdogo aliyezaliwa mwaka 89, kwa muda wa miaka michache aliyofanya kazi za sanaa, amepata mafanikio makubwa sana na sasa ni mmoja wa wasanii wakubwa sana Tanzania asiyeshuka bali anapanda kila siku, kijana huyu amekua pia akifanya mambo mengi yakujijenga na kuwasaidia wengine, Diamond kawekeza sana kwenye kujenga nyumba zake binafsi na biashara, Diamond sio kijana mpenda starehe bali amekua akifanya sana kazi yani huwa hata kama ni skukuu kuliko kula bata na wenzake huwa yuko radhi ajiandalie tamasha yeye mwenyewe limuingizie kipato, haya yote nimeongea kwasababu ya kufurahishwa na jambo hili, hizo picha unazoziona hapo juu, Diamond yupo katika shule ya EAST AFRICA INTERNATIONAL iliyopo mikocheni akiwaandikisha watoto ambao sio ndugu zake bali kajitolea kuwasomesha, kwa kweli anastahili kupongezwa, kitendo cha mtu kujitolea kumpa elimu mwanao ni kikubwa sana, wasanii wengine wangekua hivi basi wangefika mbali sana, manake hizi ndo Baraka zenyewe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment