Mama wa aliyekua movie star namba moja Tanzania STEVEEN KANUMBA anatarajia kutengeneza movie ya kumuenzi Kanumba, movie hyo itaelezea maisha ya Kanumba toka mdogo mpaka alipofikia wakati wa kifo chake, kwa kweli STEVEEN KANUMBA naweza kusema ndo alikua changamoto kwa waigizaji wote Tanzania, mpaka sasa hakuna hata muigizaji mmoja anayeweza kufanya aliyofanya Kanumba, hata Ray ambaye wengi walidhani ni mshindani wa Kanumba hajafanya chochote toka Kanumba afariki, hii inatishia tasnia ya filamu kushuka hasa ukizingatia tulifika mbali kidogo kwenye swala Zima la uigizaji, hivi sasa ukiona msanii wa filamu anazungumziwa basi ujue ni kwa ajili ya kashfa za mapenzi na mambo mengine yasiyo ya msingi lakini marehemu STEVEEN KANUMBA alikua anaitangaza Tanzania sana kupitia movie zake, movie zake alikua anajitahidi kuzitangaza kimataifa, kijana wa watu alikua hatulii leo utamsikia yuko kesho huku ili tu movie zake zijulikane,
STEVEEN KANUMBA
COVER LA MOVIE YA KANUMBA ALIYOMSHIRIKISHA RAMSEY NOUH WA NIGERIA.
MAMA KANUMBA
Huyu ndo mama yake na Kanumba, mama huyu ndie aliyeamua kumuenzi mwanae kwa kutengeneza movie itakayohusu maisha ya mwanae toka utoto mpaka ukubwani.
KANUMBA AKIWA NA MWANAMZIKI 2FACE.
KANUMBA AKIITANGAZA MOVIE YAKE YA DEVIL KINGDOM NIGERIA
KANUMBA AKIWA NA MWANADADA MTANGAZAJI WA TV GHANA
KANUMBA AKIITANGAZA KAZI YAKE GHANA
TUSEME UKWELI JAMANI, MPAKA LEO, NI NANI ALIYEWEZA KUFANYA YOTE HAYA KWENYE SEKTA YA SANAA YA MAIGIZO, MI NAONA KWENYE VYOMBO VYA HABARI MARA RAY KAGOMBANISHA MADEMU, MARA WEMA KANYANG'ANYWA GARI, MARA WOLPER KANYANG'ANYWA GARI, MARA HUYU HIVI NA YULE HIVI, YANI SIJAWAHI KUONA MTU AKASEMA MSANII FULANI KAFANIKIWA KUIPELEKA MOVIE YAKE NCHI FULANI, AU MSANII FULANI KACHEZA MOVIE NA MTU FULANI, KWA KWELI TANZANIA MNASIKITISHA, YANI SIKU ZOTE MNATAKA MUISHIE HUMU HUMU KWENYE MAGAZETI YA SHIGONGO BASI LAKINI KUFANYA VITU VYA MAANA HAPANA, INASIKITISHA SANA, INASIKITISHA SISI WAANDISHI TUNAPOANDIKA HABARI ZA SKENDO TU NA SI ZA MAMBO MAZURI YANAYOFANYWA NA HAWA WASANII. EMBU BASI KANUMBA MWINGINE AIBUKE JAMANI, AFANYE MAMBO MAKUBWA ILI WAKINA RAY WASILALE WAMUIGE NAO WAPANDE KISANII. NI HAYO TU
No comments:
Post a Comment