Sunday, January 5, 2014

WASOMALI WANAVYOTEKA NYARA MELI BAHARINI.... HII MOVIE INAONYESHA KILA KITU

hii movie inaitwa CAPTAIN PHILLISPS, ni movie nzuri sana, inaelezea jinsi wasomali wanavyotekaga meli huko baharini, kwa wengi sio jambo geni kusikia kwenye vyombo vya habari jinsi wasomali wanavyoteka meli za mizigo huko baharini, sasa movie hii inaonyesha kila kitu juu ya huo utekaji nyara, na walioigiza ni wasomali wenyewe na wanaotekwa ni wazungu manake meli hiyo ilikua inatokea Marekani kwenda Mombasa ndio ikatekwa, nilichokipenda kwenye hii movie ni kwamba, yani wale wasomali waliogiza kama watekaji nyara wameendana sana na nafasi zao, kuanzia mavazi mpaka jinsi walivyokua wamechafuka chafuka,

                                                                     cover la movie
 
 














huyu msomali unayemuona hapo chini kwenye movie ndie mkuu wa kikosi cha utekaji nyara, yani nataka umuone alivyo halafu uone picha zake  nyingine alizovaa suti jinsi alivyopendeza


na hizi picha zinazofuata ndo zinamuonyesha huyo msomali alivyopendeza tofauti na anavyoonekana kwenye movie, kweli wenzetu wanajua kuuvaa uhusika





Anaitwa BARKHAD ABDI, ni msomali lakini alizaliwa Marekani mwaka 1985 na kukulia Yemen na baadae kwenda kumalizia masomo yake Marekani,

No comments: