HAPA KWENYE PICHA NI MUIGIZAJI GABRIELLA UNION WA MAREKANI AKIWA NA MUMEWE MCHEZA BASKET DWAYN WADE AMBAPO WAMEFUNGA NDOA JUMAMOSI HII BAADA YA KUKAA KWENYE UHUSIANO KWA MUDA WA MIAKA MITANO.
Kuna mtu kaniuliza hivi ni kwanini wasanii wa bongo movies hasa waschana hawakai kwenye ndoa zao na wengine hawaolewi kabisa, mimi kwa maono yangu kidogo niliyonayo ninachoona labda ni neon SUPESTAR ndo linavunja ndoa, wengi wa mabinti wanapokua mastar wanashindwa kutofautiisha maisha ya ustar na maisha ya kua mke, na sio kwamba wanajitakia kua hivyo hapana hata wenyewe hawaelewi inahitaji utulivu na nidhamu ya hali ya juu ukiwa mschana mdogo, mzuri na star kuweza kujua kwamba nikiwa kwa mume wangu mimi ni mke na sio star hivyo natakiwa nifanye yale yote mke anayotakiwa kufanya akiwa ndani ya nyumba,
NEWLYWED ANGELINA JOLIE AND BRAD PITT
Kuna mambo mengi mschana mdogo ambaye ni super star anatakiwa ayajue kabla ya kuingia kwenye ndoa ili idumu, kwanza anatakiwa kujua huyo anayemuoa ni MUME NA SI BUZI, wengi wa masuper star wanapenda kuolewa na wanaume wenye pesa na wakishaingia kwenye ndoa wanapenda kutumia hizo pesa za mume kwa kujionyesha kwa wenzake na kwa mashabiki, mfano utamuona anabadilisha magari ya gharama bila sababu, nywele nguo na viatu vya gharama ilimradi tu masuper star wenzake wamkome lakini anasahau kwamba pesa anayotumia ingeweza kuwajengea maisha mazuri zaidi hapo baadae yeye na mumewe na kama akiwa mshauri mzuri kwa mumewe na kuweza kubana matumizi basi pesa hiyo inaweza kumfanya akawa super star mkubwa duniani na si Tanzania pekee kwani ataitumia kwa malengo, sasa kwa atayetumia pesa ya mumewe bila malengo ndo unakuta mume anaishiwa na superstar anaanza kuchuna mabuzi nje na ndoa kuvunjika wakati yeye ndo aliyesababisha mume kuishiwa kwa kutumbua hovyo.
TANZANITEMOVIES BLOGGER RACHEL KAYUNI
Sababu nyingine inayowafanya masuperstar wa kike kutokudumu kwenye ndoa ni kuleta ustar nyumbani, yani superstar anatakiwa kujua vile ambavyo mashabiki wanamchukulia nje akiwa nyumbani hatakiwi kua hivyo, anatakiwa abadilike awe mtu mwingine kabisa, mfano utakuta mtu kwasababu ni star basi akiwa nyumbani hataki kufanya usafi, hataki kumuandalia mume wake mahitaji muhimu kisa yeye ni star, hataki kuangalia watoto na nyumba kwa ujumla kisa yeye ni star, sasa kwa maisha ya namna hiyo hakuna mwanaume atakayevumilia, mwanaume kakuoa kwasababu kakupenda wewe na si ustar hivyo anataka uishi kama wewe ukiwa nae na si uishi kama star ukiwa nae,
Kingine ni kwamba mastar wengi wa kike wakiolewa huwa hawasikii la mume, yani yeye kama alikuwaga wa kujirusha kwenye ma club na kwenda kwenye vigodoro au vibao kata basi hata akiolewa atataka afanye hivyo hivyo kitu ambacho si sahihi na hakuna mume atakayeweza kuvumilia hata huyo mume akiwa LIL WAYN na uchizi wake hawezi vumilia,
SABABU INAYOWAFANYA MASTAR WASIOLEWE kwanza ni jinsi wanavyojiweka kwenye jamii, utakuta star mzuri tu lakini mapicha anayoyaweka kwenye mitandao ya kijamii MARA KABINUA MAKALIA, MARA ANAKULA GAMBE MACHO MEKUNDUU, MARA ANAVUTA MISIGARA, MARA AMEKUMBATIANA NA MWANAUME HUKU MWANAUME KAMUWEKEA MIKONO KWENYE MAKALIO kwa mwendo huo hata uwe mzuri vipi mwanaume hawezi kukuchukulia serious atakuchezea tu,
Mara nyingine ni ngumu kumuoa star kwasababu ya style ya mavazi, hukatazwi kuvaa nguo fupi ila ukivaa kaa kiheshima,tembea kiheshima na ongea kiheshima, wapo wakina Nancy Sumari wanavaa nguo fupi lakini wanaongea kiheshima na kuishi kiheshima huwezi kukuta mtu atamsema nguo aliyovaa, lakini mtu anavaa nguo fupi , anajipiga picha kajibinua makalio, au katandaza miguu jamani hapo lazima uschezewe, mwingine style za nywele yani mtu anaweka minywele kama shetani ina mirangi rangi imechanuka hovyo na ma make up makali na makope marefuuu makucha ndo usiongee mareefuuu mpaka unawaza hivi huyu mtu anaweza kujinawisha kweli, sasa kwa mwendo huo hakuna atakayekupenda kwa dhati, kwanza atakupeleka wapi kichwani umeweka nywele kama jogoo kasimama wazazi wake si watamuachia laana, kucha zimechachamaa kama shetani utamsalimia mama mkwe kweli, weka style nzuri za nywele kama wakina GENEVIEVE NNAJI, OMOTOLA, KIM KARDASHIAN, weka kucha nzuri na zisiwe na urefu wa majini ziwe na urefu wa wastani, unapokaa sehemu kaa na ongea kiheshima hujui nani anakuangalia maana mtu kwa kumuangalia mtu hata kwambali tu utajua huyu boga na huyu kifaa,
Unakuta mtu anajirecord kwenye INSTAGRAM ameweka mziki halafu anaimba kimahaba huku anatoa ulimi anaulamba lamba mara anabusu, yani hivi mtu na akili zake akikuona mschana mzuri unafanya hivyo si anakuona hauna kazi, kwanza wewe STAR unatakiwa uwe busy usiwe na muda wa kulambalamba ulimi kwenye isntagram videos, yani kitendo cha kupata muda kama huo tu unaonekana hamnazo, hatukatai kujirecord ila jirecord basi ukiwa unafanya tukio sio kujilamba ulimbi huku unaimba kimahaba no one will take u serious hata wakicomment wakawa wanakusifia ni wanakudanganya star anasifiwa kazi aliyoifanya ikampa ustar sio kujilamba ulimi,
NGOJA NIISHIE HAPO WAPENZI KAMA KUNA MWENYE NYONGEZA ANAKARIBISHWA HILA HAYO NI MACHACHE TU YAPO MENGI MNO YA KUREKEBISHANA NA HAIMAANISHI KWAMBA MIMI NIKO PERFECT HATA MIMI NA MABAYA PIA ILA NAJIFUNZA KWENYE MAISHA YA KILA SIKU NA NAONA MIFANO YA WATU,
No comments:
Post a Comment