Wednesday, September 3, 2014

MNAIKUMBUKA HII TAMTHILIA? TAMTHILIA ILIYOWAFANYA WATANZANIA WAWE WANAACHA KAZI ZAO KILA IKIFIKA SAA TATU USIKU.


Kibongobongo tunaiita ni tamthilia ya MARICHUI, lakini inaitwa CUIDADO CON EL ANGEL, ni tamthilia ya nchini MEXICO iliyopendwa sana TANZANIA hasa kutokana na uhandsome wa kinara wake wa kiume anayeitwa WILLIAM LEAVY lakini kwenye hii tamthilia alikua anaitwa JUAN MIGEL, mbali na Juan Migel pia kinara wa kike nae alikua gumzo mpaka watu kuamua kujipachika jina lake naye anaitwa MAITE PERON ila kwenye hii tamthilia alikua anaitwa MARICHUI, sasa ukiibamba hii tamthilia kwenye station za kwenye king'amuzi zile STVE1 yani ni mahabat ya kufa mtu hakikatwi kitu ila tu ukiangalia baba awe mbali maana akiwa karibu mahabat ya kianza mwenyewe utaanza mara kujikunakuna, mara kuangalia angalia ukuta, mara kusuguasugua kochi, na mama hakawii nae kusema hebu badilisha station halafu baada ya dakika moja utaskia hebu rudisha kwenye marichui, basi kama unavidogo vyako hapo vitaanza kuwaza kwanini mama alisema station ibadilishwe halafu baada ya dakika moja tena akasema turudishe kwenye marichui basi lazima kuna kitu BASI KESHO NA VYENYEWE VIDOGO VYAKO VIKIONA MAMA NA BABA WAKO KAZINI NA WEWE UKO CHUO VINAKAA MCHANA VINASUBIRIA MARUDIO YA MARICHUI IKIFIKA ZILE SEHEMU MLIZOKUA MNABADILISHA STATION NDO VINAKODOA MACHO NA KUJIONEA LIVE BILA CHENGA JINSI MARICHUI NA JUAN MIGEL WANAVYO MALOVEYDAVIKA.
 
Wiliam Leavy alizaliwa mwaka 80 huko Cuba na baadae kwenda kuishi Marekani na kusoma huko then alivyomaliza wakaenda kuishi Mexico na akaanza kazi ya u model, ambayo ikampeleka kwenye kuigiza tamtthilia na sasa anaigiza mpaka movie huko kwao Mexico na Hollywood pia.
 
William kama mnavyomuona hapo chini yuko na mkewe, anamke na watoto wawili
 
picha ya chini ni William, mkewe na watoto wao wawili
 
Mama Kardashian nae hakua nyuma kumualika William kwenye show yake, ila huyu mama haaminiki anapenda ujana sana mke wa William inabidi achunge abiria wake.
 
Jlo nae kama kawa mnamjua kwa dogodog handsome, hakua nyuma kumchukua William ili atokee kwenye video yake ya IM IN TO U. baada ya hii video tu JLO na mumewe wakaachana basi watu wakasema ehhhhhh William kafanya mambo, kumbe ni kakijana kengine kadancer kake kenye miaka 22.
 
 William Leavy pia ameshacheza movies mbalimbali moja wapo ni SALSA aliyocheza na mke wa muigizaji WILL SMITH anayeitwa JADA PINKED SMITH kama mnavyomuona hapo juu kwenye picha.


Maite Peron au kama wengi wanavyomfahamu kwa jina la MARICHUI ni mzaliwa wa MEXICO na amezaliwa mwaka 1982, Marichui licha ya kua yeye ni muigizaji lakini pia yeye ni mwanamziki anayefanya vizuri tu kwenye mziki nchini Mexico.
 
 
 
 
 
Maite Perroni in red
 
 


Na hizo picha za mahaba hapo juu ni mwanadada MARICHUI akiwa na mpenzi wake wa sasa anayeitwa KOKO STAMBUK
 

No comments: