Friday, September 5, 2014

MAREHEMU JOAN RIVER PICHA ZAKE ZA UJANANI NA SASA HIVI

Jana dunia imepata mshtuko baada ya comedian na host wa kipindi cha FASHION POLICE anayeitwa JOAN RIVER kuaga dunia, umauti ulimkuta katika hospitali ya MOUNT SINAI alipokua anafanyiwa upasuaji wa koromeo, Joan amefariki akiwa na umri wa miaka 81 na ameacha motto wa kike anayeitwa MELISSA RIVER ambaye ni producer pia wa show ya FASHION POLICE inayoonyeshwa kwenye station ya E.

                      HAPA JOAN AKIWA BINTI
 
 
 
Moja ya vitu ambavyo Joan amekua akijatania mwenyewe ni jinsi alivyofanyiwa upasuaji wa kujirekebisha sura yake mara nyingi, kuna wakati aliwahi kusema kua ANAHOFIA HATA AKIFA MUNGU HATAMGUNDUA KUTOKANA NA SURA YAKE ILIVYOBADILIKA, picha za chini ni sura za Joan tofauti tofauti
 
PICHA YA CHINI NA YA JUU NI JOAN AKIWA NA MWANAE MELLISA
 
Joan pamoja na umri wake kua mkubwa yani ni bibi kabisa, lakini hakuwahi kuachwa nyuma ya wakati, yani kila karne inavyobadilika na yeye anabadilika, kilichokua kinanifurahisha kwake ni jinsi alivyokua anawajua mastar wote wakubwa duniani yani mpaka wale wenye umri sawa na vitukuu vyake na anajua na habari za mamboyao ya kila siku, kitu ambacho si cha kawaida kwa bibi wa miaka 81 kujua yote hayo. NTAENDELEA KUWALETEA MAMBO TOFAUTI KUHUSU MAREHEMU JOAN RIVER
 

No comments: