Monday, September 29, 2014

KWA AMBAO HAWAJAONA PICHA ZA BITRHDAY FUNGA MWAKA YA WEMA SEPETU NA ZAWADI ZA MAGARI MAWILI ALIYOPEWA PITA HAPA....






























HILI GARI NI NISSAN MURANO KUTOKA KWA DIAMOND KWENDA KWA WEMA






NA HILO BMW NI ZAWADI KUTOKA KWA MARTIN KADINDA AMBAYE NI MENEGER WA WEMA SEPETU.





Sunday, September 28, 2014

MANENO KUTOKA KWA DIAMOND KWENDA KWA WEMA SEPETU EMBU INGIA UYASOME...






Laiti kama Maneno yangelikuwa ni sumu basi amini, Penzi letu lingekuwa lishazikwa na Kuoza...Maana sjui ni kipi hakijazungumzwa.....vya furaha, Chuki, shangwe, fitina, Vita, majungu, Misukosuko na mabalaa ya kila aina....lakini siku zote tumekuwa tukipendana na kuthaminiana kama tumeanzana jana, kwakuwa tulijua si kosa lao, ni hawajui tu niwapi tulipotokea...to the world, you may be one person...But to me, you are the world, My Beautiful World...na kama kukupenda ni uwendaazimu basi ni bora Nikabaki kwenye uchizi wangu kuliko kupata Ufahamu....i may not be physically present to stand by you while you cut your cake, but you’ll be in my thoughts the whole day! Happy birthday Darling....mmeo niko nahangaika, bt i will be coming home soon....Love you mama!!

Saturday, September 27, 2014

YAWEZEKANA KUKAWA NA BONGE LA PARTY LA MSANII WEMA SEPETU SIKU YA KESHO.... HEBU INGIA NDANI KUJUA ZAIDI





Kesho muigizaji anayependwa kuliko waigizaji wote bongo Wema Sepetu atatimiza miaka kadhaa, marafiki zake tangu asubuhi ya leo wamekua wakipost picha zake na kuelezea kwamba kesho ni birthday ya binti huyo, kwa jinsi post hizo zinavyopostiwa na marafiki zake inaonekana HIYO SIKU YA KESHO KUTAKUA NA SHEREHE YA KUKATA NA SHOKA, NA PIA WENGI WANASUBIRI KUONA KAMA MCHUMBA WA WEMA AMBAYE NI DIAMOND ATAMFANYIA NINI MPENZI WAKE HASA IKIZINGATIWA KWAMBA DIAMOND AMEPANGUA TUHUMA ZA KWAMBA ANAMAHUSIANO NA MENINAH, DIAMOND AMESEMA YEYE NA WEMA BADO NI WAPENZI. haya mi nasubiri mapicha ili niwaletee ....

BONGE LA HARUSI KUFANYIKA KESHO HUKO VENICE ITALY...NI LA BONGE LA MOVIE STAR DUNIANI.

MWENYE NGUO NYEKUNDU NDO BIBI HARUSI MTARAJIWA NA BWANA HARUSI HUYO HAPO JUU




BIBI HARUSI MTARAJIWA MWENYE NGUO NYEKUNDU

MJI WA VENICE UMEJENGWA JUU YA MAJI KWA HIYO HUKO NI MWENDO WA BOAT TU MAGARI HAKUNA,

BIBI HARUSI MTARAJIWA












Picha hizo hapo juu ni za rehearsal ya harusi ya muigizaji bei mbaya wa Hollywood anayeitwa GEORGE CLOONEY. harusi itafanyika kesho kwenye mji uliopo juu ya maji wa Venice nchini Italy, bibi harusi ni raia wa uingereza na ni mwanasheria pia, George huwa anajulikana kwa kua na ma girlfriend tu na alikuwaga aliulizwa kwenye vyombo vya habari alkuwaga anasema hatarajii kuoa leo wala kesho licha ya umri wake kuzidi kukimbia, lakini safari hii ampatikana kwani muda mfupi tu baada ya kuanzisha mahusiano na mwanasheria huyo anayeitwa Amal , George mara moja alijikuta akitangaza ndoa,





Thursday, September 25, 2014

MENINA APASUA YA MOYONI KUHUSU KUTEMBEA NA DIAMOND........




                                                         MENINAH

Yaani sijui hata nianzie wapi kuzungumzia hili la kutaka kufunga ndoa na Diamond, naomba niseme ukweli kwamba nashangaa, kwanza sijui chochote, nimekuwa nikiandikwa mara kwa mara lakini taarifa hizo wala hazina ukweli wowote.
“Mimi na Diamond ni tofauti kabisa, sijawahi kuwa na ukaribu naye. Kwanza naumia sana na kutokwa na machozi kuendelea kusikia taarifa hizi kuwa naolewa naye kitu ambacho hakipo kabisa, hata yeye mwenyewe akisikia hivi anaweza kumtafuta mtu ambaye anasemwa kuwa anatoka naye jambo ambalo si la kweli.”
“Wema namheshimu kama dada yangu, mtu ninayemjua kwenye tasnia ya filamu Bongo, kwanza wote tunafanya sanaa japokuwa kwa upande wake anafanya filamu na mimi muziki. Hizo taarifa juu ya kuniwinda sijui na sijazisikia. Kiukweli zimenishtua sana






KWA HIYO NAONA KUTOKANA NA MAELEZO HAYO YA MENINAH NI WAZI HAKUNA MAHUSIANO KATI YAKE NA DIAMOND, NA KAMA DIAMOND NA WEMA WAMEACHANA BASI NI KWA MATATIZO YAO TU YA KAWAIDA KAMA ILIVYO KWENYE MAHUSIANO YA WATU WENGINE, KUGOMBANA KUPO, LAKINI PIA KUPATANA KUPO.

Monday, September 22, 2014

LUCY KOMBA ALALAMIKIWA NA MASHABIKI



14


Muigizaji Lucy Komba ambaye amefunga ndoa takatifu na mumewe mwenye asili ya Canada amelalamikiwa na mashabiki kwa kitendo cha kunung'unika mno toka ndoa hiyo ifungwe, kama inavyojulikana ukiwa star kusemwa na kukosolewa lazima kuwepo, lakini kwa Lucy imekuwa tabu kwani kila mitandao inapomkosoa yeye amekua akocopy na kurusha kwenye page yake ya insta, isipokua hivyo amekua akiwapiga vijembe kila kukicha wale waliokua wanachukia yeye kufunga ndoa, mpaka imefika hatua ma funs wake wamekua wakimsihi aache kulalamika yeye anachotakiwa ni kumshukuru Mungu kwa kumpa mume mwema na hayo mengine yalishapita agange yajayo.

Sunday, September 21, 2014

MY SUNDAY ............

Photo: With Shamsa Ford

                                            ME NA SHAMSA FORD MUIGIZAJI MWENYE SMILE YA NGUVU
Photo

                                                                      MIMI RACHEL KAYUNI
Photo

                                                 MIMI RACHEL KAYUNI





 



Friday, September 19, 2014

WEMA SEPETU NA KAJALA MAPEDEJEE WA KIKE

                        KAJALA MASANJA                                      WEMA SEPETU


Wakati  muigizaji Kajala Masanja akifanya kufuru ya pesa ndani ya band ya yamoto band baada ya week nae muigizaji Wema Sepetu alifanya kufuru ya pesa ndani ya skylight band, inasemekana wadada wote hao walimwaga zaidi  tano kwa kuwatunza wanamziki wa band hizo,


JAMANI NAWAOMBA WASCHANA WENZANGU ZITUNZENI HIZO HELA WENGINE HATUNA TUKIONA MNAZIMWAGA VILE MPAKA DAMU INASISIMKA, YANI UKIONA MISIMBAZI IMETAPAKAA CHINI KAMA CARPET LAZIMA USISIMKE NA KUANZA KUWAZA SHIDA ZINAZOKUKABILI ZINAZOHITAJI UTATUZI WA FEDHA, ila mwisho wa siku kila mtu anauhuru wa kufanya analotaka na hela yake.

Thursday, September 18, 2014

AUNT LULU EMBU INGIA UMTIZAME PICHA ZAKE








Aunt LULU ni msanii mwenye skendo nyingi kuliko kazi, ni mzuri wa sura na umbile lakini anahitaji kulifanyia kazi umbo lake ili liwe dogo la lenye muonekano mzuri, pia anahitaji kupaka mafuta mazuri yatakayoendana na ngozi yake, baada ya hapo anahitaji kuvaa mavazi ya heshima na kuwa na tabia njema kwenye jamii, akizangatiia hayo basi atafikia malengo.....






HUWA NIKIANGALIA MTU AMBAYE AMESHAKUA MAARUFU HALAFU ANASHINDWA KUTUMIA UMAARUFU WAKE KUTENGENEZA PESA NAHUZUNIKA SANA, WASANII HUU NIWAKATI WA KUAMKA, PESA MNAZOHONGWA HUWA HAZIKAI HATA MIAKA MIWILI ZINAWAISHIA, HAZINA BARAKA NDO MAANA ZINAISHA, KUWENI NA MIKAKATI YA MAISHA NA MFANYE KAZI NA MTAHESHIMIKA.

DIVA WA CLOUDS FM NA MUHESHIMIWA ZITO KABWA WAOMBWA RADHI..






KATIKA Gazeti la Amani Toleo Namba 829 la Septemba 11-17, 2014, kulichapishwa habari ukurasa wa mbele iliyosomeka: “DIVA: ZITTO NI MUME WANGU.” Ikikolezwa na dondoo ‘Adai ni mke anayetambulika kisheria’ na ‘Asema hayuko tayari kuachana naye kirahisi,’ ambayo uongozi wa gazeti umekusudia kwa nia njema kutoa ukweli juu ya habari hiyo
Ufafanuzi huu unalenga kumaliza mkanganyiko uliojitokeza hasa baada ya kuwepo kwa madai kutoka kwa mhusika ambaye ni Loveness Malinzi (Diva) kuwa, hakuzungumza na gazeti kile kilichoandikwa na kwamba alikuwa anazushiwa; madai haya aliyawasilisha chumba cha habari kwa njia ya simu na sehemu kuyaweka kwenye ukurasa wake wa kijamii wa Instagram.
Kama hilo halitoshi, Diva alikana kuzungumza na mwandishi wa habari hiyo  ambapo alisema mazungumzo yao yalihusu mwaliko wa Kipindi cha Global TV Online ambacho kinarushwa na mtandao unaoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers inayomiliki pia Gazeti la Amani na si vinginevyo.
Malalamiko haya ya Diva yalikuja muda mchache baada ya gazeti kutoka likiwa na habari hiyo ambapo jopo la wahariri wa Amani kabla ya kuchapisha habari hiyo walijiaminisha kuwa ni ya kweli kutokana na taarifa pamoja na vielelezo vya rekodi ya sauti ya mazungumzo alivyoviwasilisha mwandishi kwenye dawati kuthibitisha kuwa alifanya mazungumzo na mhusika kuhusiana na msingi wa habari nzima iliyoandikwa
Kama tulivyoeleza, baada ya habari hiyo kutoka na kipande cha sauti kuingizwa  kwenye Tovuti ya Global Publishers, ndipo yalipoibuka madai hayo huku baadhi ya wasomaji wakieleza kuwa ile siyo sauti ya Diva; hapo ndipo uongozi wa gazeti ulipoamua kufuatilia ukweli na kubaini yafuatayo.
Pamoja na ukweli kuwa Mheshimiwa Zitto Kabwe (Mbunge wa Kigoma Kaskazini) na Diva wana ukaribu, mazungumzo kati ya mwandishi na mwanadada huyo kuhusiana na kauli yake ya: “Zitto ni Mume Wangu,” hayakufanyika na kwamba mwandishi alipika habari na kutengeneza sauti ya Diva kwa lengo la kuwahadaa wahariri kwa nia mbaya!
Kwa msingi huo sisi kama chombo cha habari makini, kinachosimamia weledi, kulinda na kuheshimu haki za binadamu; tunachukuwa nafasi hii kumuomba radhi Diva, Mheshimiwa Zitto, sanjari na jamii kwa ujumla kwa usumbufu wowote uliosababishwa na habari hiyo.
Aidha, uongozi unapenda kuutangazia umma kuwa, hatua kali za kinidhamu zimeshachukuliwa dhidi ya mwandishi husika sambamba na onyo kwa viongozi wote wa gazeti kwa udhaifu uliojitokeza katika habari hiyo
Tunaomba jamii ielewe kwamba Global Publishers siku zote inasimamia UKWELI na kamwe hairuhusu kabisa habari za uongo kuandikwa katika magazeti yake.
Jamii iendelee kutuamini na kushirikiana nasi katika kusimamia weledi wa uandishi wa habari. Milango ya kukosolewa iko wazi, hivyo kwa mwenye malalamiko yoyote juu ya habari zetu, iwe ni uongo au kutotendewa haki, asisite kuwasiliana na viongozi kwa hatua zaidi. Ndimi, Mhariri Kiongozi, Magazeti Pendwa



NIMEMUWEKA DIVA KWASABABU NI RAFIKI WA MUIGIZAJI WEMA SEPETU, MAANA NAJUA ITASHANGAZA KWANINI DIVA NIMEMUWEKA HUMU WAKATI YEYE SI MUIGIZAJI.

Wednesday, September 17, 2014

THESE ARE THE HOT MAMAS IN BONGO MOVIES INDUSTRY......

Photo: Helw @#Nawatakia cku njema @#Wapendwa


                                                KAJALA MASANJA ...hapo juu huyo ni Kajala, nimemuweka namba moja kwasababu yeye anamtoto mkubwa ambaye wakiwa pamoja ni kama mtu na dada yake lakini hiyo haijamfanya Kajala kujiachia na kua kwenye kundi la mama.com, Kajala anawaka na anakwenda sambamba na wale ambao hawajazaa na wengine kawapita kabisa, hongera dada.


IRENE UWOYA


 IRINE UWOYA...............hapo juu kama mnavyomuona ni Irine, yeye pia ni mama lakini pamoja na kuzaa mpaka sasa bado yuko vile vile kama zamani, kama humjui unaweza kufikiri hajazaa bado.





SHAMSA FORD.... huyu ni mama wa motto mmoja, yeye kwanza licha ya uzuri na kutokujiachia, Shamsa anasmile moja matata sana Bongo movies nzima hakuna, pia anarangi nzuri na hajawahi kuhangaika kujichubia,






NAJUA WAPO WENGINE NTAKUA NIMEWASAHAU LAKINI HAWA WATATU NI MOJA YA WASANII AMBAO NI WAMAMA LAKINI BADO WANASUMBUA KWA UZURI.

Tuesday, September 16, 2014

MONALISA CHINDA WA NIGERIA AANGUSHA BONGE LA PARTY INGIA UTAZAME MAPICHA YANAVYOJIELEZA.

                         WA KATI NDO MONALISA NA MWENYE NJANO NI LIZ BENSON MUIGIZAJI ANAYEHESHIMIKA KULIKO WAKINA GENEVIEVE
MONALISA NA LIZ BENSON,bwana Liz akiigiza uchawi unaweza usilale usiku.
















        LIZ BENSON THE QUEEN OF NOLYWOOD

MONALISA NA UTI NWACHUKWU WA BIG BROTHER








Mwanadada ambaye ni muigizaji wa Nigeria anayeitwa MONALISA CHINDA juzi alifanya bonge la birthday party akiwa anatimiza miaka 40, ( yani sikuhizi watu miaka 40 bado waschana kabisa inanipa moyo labda na mimi nikakufikisha ntakua hivyo) , basi party hiyo ilihudhuriwa na ndugu jamaa na marafiki pamoja na waigizaji wenzake .