RACHEL KAYUNI
tanzanitemovies blog is a blog that gives you the chance to know everything that happens in the movie industry. rahelimacdonald@gmail.com 0713-608524
Wednesday, April 30, 2014
MAHOJIANO YA KAJALA KWENYE TAKE ONE
KAJALA MASANJA
KAJALA NA ZAMARADI
PAULA MTOTO WA KAJALA
Yani kwa yeyote aliyepata nafasi ya kusikiliza mahojiano ya Kajala na mwanae kwenye kipindi cha take one cha Zamaradi atakua kajisikia vibaya sana, kwa kweli Kajala kaniumiza sana moyo, huwa namjua ni mpole lakini sikujua pia kama mambo ya ugomvi yanamuumiza sana kiasi hiki jamani, Kajala amekataa kwamba hajamchukulia Wema bwana, hivi ni kitu gani kilichowagombanisha manake hakuna anayesema kati ya Wema wala Kajala, je? au ni kitu kikubwa kuliko kuchukuliana bwana, au pengine ni kidogo na cha kijinga ambacho hakina maana hata kuelezeka kwenye vyombo vya habari? NAWAOMBEA TU WAPATANE JAMANI MANAKE NAWAPENDA WOTE.
Monday, April 28, 2014
SINTAH, MANGE KIMAMBI NA LINDA BEZUIDENHOUT
Tunaanza na Linda, nimemuweka humu kwasababu ni dada wa muigizaji Richard Bezuidenhout, Linda kama mnavyomuona, ni mama wa watoto wanne lakini ni mzuri kupita kiasi, yani ukiambiwa yeye amekamilika kila idara,SURA, MIGUU, SHAPE, RANGI YA MWILI, NYWELE, na nyongeza yake ni SMILE yake ya kukata na shoka. Ni mwanamke mchapakazi sana na anaishi Marekani, kwa wanaopenda mambo ya mitindo basi huyu ni mfano wa kuigwa.
LINDA BEZUIDENHOUT
Nawapenda wote hao wanawake hapo juu, wote ni mfano wa kuigwa japo wanamapungufu yao lakini wote ni wachakarikaji hawajajibweteka hata kidogo,
JE? WEWE WAMPENDA NANI KATI YA HAWA?
LINDA BEZUIDENHOUT
Anaitwa Mange Kimambi, ni mama wa watoto watatu, mrembo, yupo makini na malengo yake, ni chanzo cha mastaa kadhaa wanaosumbua jiji, mmoja wa mastar hao ni WEMA SEPETU, yani huyu ndo aliyesababisha magazeti ya udaku yauze sana kwasababu kwa kumtoa kwake Wema Sepetu na kumsimamia mpaka akawa miss Tanzania, kumemfanya Wema kua star anayeuza sana kwenye kila kitu hasa magazeti kwa hiyo chanzo cha yote ni Mange ashukuriwe kwa hilo, Mange ni chapakazi sana na anajua sana kutangaza biashara, yani kwenye marketing tu Nampa mia kwa mia, anaishi Marekani kwa sasa.
MANGE KIMAMBI
Na huyu hapa chini ni my girllll SINTAH, huyu ni muigizaji, ni muigizaji alipitia mikononi mwa waigizaji hasa yani ni zao la wale waigizaji wakongwe ambao wengi hawapo hapa duniani tena, kwa hyo Sintah akiamua kuigiza HAUZI SURA KWENYE CAMERA BALI ANAJUA NINI ANAFANYA MBELE YA CAMERA, Sintah ni mwanamke aliyemudu kubaki kwenye umaarufu mpaka sasa japo kazi iliyomfanya awe maarufu kaicha kwa sasa, muda mwingi hajaigiza lakini bado yuko midomoni mwa watu tofauti na wenzake wengi walioacha kuigiza wamesahaulika, ni mama wa motto mmoja na ni mama mzuri sana tofauti na wengi wanavyofikiria au tofauti na wengi wanavyomsoma kwenye mitandao, Sintah anajua madhara ya media kwa watoto ndo maana kamwe hapendi kumuweka mwanae kwenye media, ni kama wasanii wengi wa nje wamekua wakiwaprotect watoto wao na mambo ya media na wengine wamekua wakikataa hata watoto wao wasipigwe picha na vyombo vya habari, MADHARA YA MTOTO WA MTU MAARUFU KUONEKANA KWENYE VYOMBO VYA HABARI AU MITANDAO NI MAKUBWA KULIKO WATU MNAVYOFIKIRI, MFANO NI MTOTO WA MUIGIZAJI KAJALA ANAVYOANDAMWA KWA KOSA LISILOMUHUSU NA WATU BILA HURUMA WANAISHIA KUMTUKANA HADI MTOTO MDOGO, KWA SINTAH NAFIKIRI ALIONA MBALI LAKINI MITAANI MUDA MWINGI UTAMUONA NA MWANAE. pia Sintah ni blogger, na mfanyabiashara, ni mwanamke ambaye hana makuu kabisa ni mwepesi mno kumzoea mtu.
SINTAH
JE? WEWE WAMPENDA NANI KATI YA HAWA?
Sunday, April 27, 2014
WANAOMUIGA JOTI MDEBWEDO SASA BASI JAMANI
Joti na kundi lake la ze comedy nafikiri ndo walifanya kitendo cha mchekeshaji kuvaa nguo za kike kishamiri kama zamani walikuwepo basi miaka ya hivi karibuni joti ndo kashamirisha zaidi. TATIZO LINAKUJA HAPA....................hivi, wachekeshaji wengine na wenyewe hawawezi kubuni jamani kitu kingine zaidi ya wenyewe pia kuvaa nguo za kike na kujiremba na kuanza kuchekesha, kwa Joti ilikua inachekesha, sasa walivyovamia wengine imekua si kichekesho tena bali ni kero, kila mchekeshaji utamuona kavaa nguo za Kike halafu anakua anatangaza taarifa ya habari, JAMANI? hii kali na inachosha, HAYA SASA WAKINA JOTI KAZI KWENU KUBUNI KITU KIPYA ILI MUWEZE KUWAVUTIA WATAZAMAJI WENU. NA KWA WALE WANAOWAIGA BADILIKENI ILI TUVUTIWE NA STYLE ZENU NYINYI KAMA NYINYI LA SIVYO MKIENDELEA KUIGA HAKUNA MTU ATAKAYE WAPA ATTENTION .
Saturday, April 26, 2014
ME AND HER.
Mimi na mbwa wangu anayeitwa DIAMOND, ni jike hilo, yani mbwa huyu jinsi akiniona anavyonipenda jamani, na wanadamu wangekua hawana mapenzi ya kinafki ingekua raha sana, mara nyingine mtu unasema ni bora niunde urafiki na mbwa wangu Diamond manake najua hata mwizi akija atanilinda kuliko na watu ambao ukigeuka wengine wanakuonea wivu, wengine kukusengenya tabu tupu.
RACHEL KAYUNI
DIAMOND ANAVYOJIVUNIA KUWA NA WEMA SEPETU
NASIBU Abdul ‘Diamond’ amefunguka kuwa anajivunia kuwa na binti mzuri Wema Sepetu ambaye kila kukicha anazidi kupewa vyeo.
Diamond alifunguka hayo juzikati baada ya Wema kutangazwa mshindi wa Shindano la Ijumaa Sexiest Girl lililoandaliwa na Gazeti la Ijumaa.“Wema ni kifaa, nilimkubali na nitaendelea kumkubali,” alisema Daimond juzikati Dar.
MCHUMBA HALALI WA DIAMOND CHIBU DANGOTE.
MH HII INAMLENGA NANI?????
MSANII wa flamu za Kibongo, Tiko Kulungu amewaasa wenzake kuwa waepuke tabia ya kubadili dini kwa kufuata maslahi ya kifedha.
MSANII wa flamu za Kibongo, Tiko Kulungu amewaasa wenzake kuwa waepuke tabia ya kubadili dini kwa kufuata maslahi ya kifedha.
Mh kwa haraka haraka Wolper ndo msanii aliyebadiligi dini, sasa sijui huyo dada alikua anamlenga msanii gani, ila Wolper alishakataaga alisema hakubadili dini kwa ajili ya pesa. MJINI KUNA MAMBO.
Friday, April 25, 2014
JACKLINE WOLPER BEFORE AND AFTER
INSPIRED BY LADY GAGA hapo chini.
Picha za chini ni jinsi anavyotengeneza nywele zake sasa hivi LOVELY.
hii picha ya nywele fupi mimi huwa naipenda kweli yani hizi nywele zinampendeza sana alionekana mdogo sana.
SLIM OMARY BONGO MOVIE NZIMA ANAKIMBIZA KWA MAONI YA WATU.
Anaitwa SLIM OMARY, nilipotoa ile post ya ma handsome wa Bongo movie nimetumiwa msg nyingi watu wakilalamika kwanini nimemuacha huyu, nilimsahau jina wadau ila nilitaka sana kumweka. HUYU NDO NAMBA MOJA WA MAHANDSOME BONGO MOVIE NZIMA NA HANA MASIFA MAGAZETINI.
Thursday, April 24, 2014
DIAMOND PLATNUM NA LULU MICHAEL AKILI SAWA
Hizo picha hapo juu ni Diamond mchumba halali wa muigizaji Wema Sepetu nasema mchumba kwasababu Diamond alishamvisha pete ya uchumba Wema na sijawahi kusikia Diamond kumvisha pete ya uchumba mwanamke yeyote yule hapa duniani zaidi ya Wema, anyway niende kwenye mada, kwa hyo kama mnavyomuona kidume hapo juu yuko na mama yake na kamshikia pochi mama yake kitu ambacho ni nadra kwa vijana wengine kufanya, sasa kwa kumpenda na kumsikiliza huku mama yake kweli kijana ataacha kufanikiwa? HONGERA SANA DIAMOND
Picha za hapo juu ni Lulu akiwa na mama yake na juu kabisa ni nyumba anayojenga Lulu, huyu binti hata miaka 20 hajafika lakini amefanikiwa kujenga Nyumba kitu ambacho wengine ukisikia redioni au wanajenga wakifika hata 40, sijui mapato aliyojengea nyumba yametokana na nini ila najua ni mcheza movie na anallipwa manake najua tu humu sasa hivi watu mtaanza oooh kahongwa, kinacho matter ni kwamba kajenga wengine wamecheza movie wee, wamehongwa magari ya kifahari, lakini wanamiliki pochi na viatu tu, naimani ukaribu wa Lulu na mama yake ndio uliomfanya
Lulu kufika hapo alipo.
NI HAYO TU........ BYE BYEEEEEEE
BONGO MOVIE MAHABA NIUE MAHABA NIPOTEZE KAMA NDEGE YA MALEYSIA MAHABA ..................
Hawa ndo homa ya jiji nadhani wengi wanawafahamu, penzi lao limebarikiwa mpaka na watoto wadogo wasiojua hata mapenzi ni nini lakini ukiwauliza mchumba wa DIAMOND nani wanakwambia WEMAAAAA.
Subscribe to:
Posts (Atom)