Wednesday, December 18, 2013

WEMA SEPETU AFILISIKA......NI KWELI? AU UZUSHI?

Kama tunavyojua si kila kinachooandikwa kwenye magazeti ya udaku kina ukweli, kuna hii habari nimekutana nayo kwenye gazeti moja ya kwamba Wema Sepetu msanii wa Bongo movie amefilisika, kwa mujibu wa gazeti hilo eti Wema ameshaanza kuuza magari yake na siku hizi kapunguza kujirusha, kuuza magari kuna mawili, inawezekana kaona haina sababu ya kua na magari matatu wakati moja linamtosha, na kuhusu kutoka wengi tunajua Wema si mtokaji sanalabda kuwe na event maalum,

 
 
IKIWA NI KWELI WEMA YUKO KWENYE KIPINDI KIGUMU KIFEDHA BASI TUNAMUOMBEA KWA MUNGU ILI AMPITISHE KWENYE HII HALI, JAMBO HILI SI LA KUCHEKA KWANI NI HALI INAYOWEZA KUMKUTA YOYOTE NA SI YA KUDUMU KWANI MTOAJI NI MUNGU HIVYO KESHO TU UNAWEZA KUMKUTA KAFANIKIWA MARA MBILI YA SASA.

No comments: