Wednesday, December 25, 2013

MANGE KIMAMBI NA SINTAH WAUNGANA NA KUMKOSOA STELLA TILYA.

Mange Kimambi na muigizaji mwenye lips nzuri bongo Sintah, kwa nyakati tofauti kupitia blog zao wameungana katika hoja inayomuhusu msanii wa movie Kajala Masanja, Mange na Sintah ni mahasimu wakubwa na mara nyingi huwa wanapingana sana kwenye post zao. sasa basi kwa mara ya kwanza wameungana na kumtetea Kajala Masanja anayetuhumiwa kuiba mwanaume wa mwenzie.

                                                           MANGE KIMAMBI


                                                      SINTAH
 
 Hiki kisa kilianza hivi, Kajala alionekana katika picha akiwa na jamaa anaesemekana ni boyfriend wake, sasa kuna mschana mmoja anayekaa Marekani anaitwa Stella au kama anavyopenda kujiita Chaga Barbie, huyu stella kupitia mtandao wake wa instagram, aliweka picha ya Kajala na kuanza kulalamika kwamba kajala kaiba mwanaume wa rafiki yake, basi hii habari ikadakwa na Sintah na Mange, ambao japo wenyewe hawapatani lakini pia hawapatani kabisa kabisa na huyo Chaga Barbie, kwa hyo Sintah na Mange wakaanza kumnanga huyo chaga Barbie kwamba kakosa heshima kuanika mambo mitandaoni.

 
 
huyu ndie Kajala mwenyewe anayetuhumiwa kuiba mwanaume wa watu, ninachompendea Kajala huwa hapendi majibizano na mtu, huwa ni mpole hana makuu na hapendi magazeti,kwa hyo sakata hili Kajala hajajibu kitu, hali iliyomfanya chaga Barbie aonekane mjinga.
KAJALA MASANJA


Na hii picha ya hapa chini ndie STELLA au chaga Barbie mwenyewe, ni mwanamke mzuri ambaye haishi vituko kwenye mitandao, pia ni blogger, wachangiaji wengi wa Mange na Sintah wamemtuhumu huyu chaga Barbie kwa kumwambia yeye ndie kinara wa kuchukua waume za watu na mambo mengine mengi
 
MIMI NAUNGANA NA MANGE NA SINTAH. KWANZA KABISA HUYO ANAYELALAMIKA KAIBIWA MWANAUME SI MKE NI DEMU MTU, SASA KAMA JAMAA HAJAKUOA, NA ALIKUA NA WEWE SIKU ZOTE, ILA SASA KAAMUA KUA NA MWINGINE, UNALALAMIKA NINI? HII MANAKE NI KWAMBA HUYO JAMAA KAKUONA UNAMAPUNGUFU NDO MAANA KAENDA KWA MWINGINE AMBAYE WATAENDANA KITABIA, WASCHANA WENGI WAMEKUA WAKIWATESA MA BOYFRIEND ZAO, KUWANYANYASA NA KUWADHARAU,TENA IKITOKEA KAMZIDI KIPATO JAMAA NDO USISEME ATATAKA MPAKA ANAWISHWE MIGUU, HALAFU KAMA MWANAUME KAONA HAUFAI KUA MKE WAKE UTAMLAZIMISHA AKUOE JAMANI, SI LAZIMA ATAFUTE WA KUOA,  NDO MAANA MWANAUME PINDI ANAPOPATA MSCHANA ATAYEMUHESHIMU ANAAMUA KUHAMISHA MAJESHI, WE UNASHINDA KWENYE KOCHI UNAANGALIA TV, MWANAUME ATOKE KWENYE MIHANGAIKO JIONI KACHOKA, NDO AINGIE JIKONI APIKE, WE DEMU UMEKAA MGUU JUU, MWANAUME ASAFISHE NYUMBA, AJIFULIE NGUO, WE DEMU MCHANA KUTWA UMEKAA TU, HALAFU MWANAUME AKIMPATA WA KUMFULIA NA KUMPIKIA TENA MWANAMKE BOMBA ZAIDI YAKO UNAANZA KUPIGA KELELE NA KUITA MAJESHI YAKUSAIDIE. MIMI NAKEMEA TABIA YA KUTEMBEA NA MUME WA MTU TU, LAKINI SIO DEMU TU AMBAE TENA HUNA HATA URAFIKI NAE ANALALAMIKA UMEMUIBIA BOYFRIEND, KAMA ALIVYOSEMA MANGE, MBAYA NI KUMCHUKUA BOYFRIEND WA RAFIKI YAKO, LAKINI BOYFRIEND WA STRANGER?  ULIYEIBIWA NA KAJALA JICHUNGUZE, KAMA ULIKUA UNAJIFANYA WEWE NDO KIDUME NDANI YA NYUMBA NA KUMFANYA MWANAUME WAKO KAMA HOUSEBOY WA KUKUFANYIA USAFI NA KUKUPIKIA NDO HAYO KAJALA KANYANG'ANYA TONGE MDOMONI.

No comments: