Tuongee ukweli, Bongo movie stars wengi hawajui kuvaa, si kosa, kila kitu kinamtaalam wake, ikiwa kama umeamua kua msanii na unataka kufika mbali, kitu cha kwanza kabisa kuuza kazi zako ni muonekano, kama huna utaalam na mambo ya kupangilia mavazi, siku hizi kuna watu maalamu kwa ajili ya kuwapangia nguo mastar, ili anapotoka aweze kua na muonekano wa ki star. Nigeria, Ghana sasa hivi wasanii wao wanajua hasa kutokelezea kwasababu wanawatu maalum wa kuwafanya wapendeze. Leo mfano ni kwa msanii mkubwa wa Tanzania Ray Kigosi.
RAY (VINCENT) KIGOSI
Bwana Ray anatuangusha liapokuja swala la fashion, to be honest sijui anavaa nini . Kwanza this guy is realy realy handsome, ana muonekano wa ki star kuliko msanii yoyote wa kiume, licha ya hivyo, ni star anayeongoza kwa mauzo nchini wanachuana na JB.
Msanii yoyote wa hapa Tanzania ni lazima anandoto za kujulikana Africa nzima na hatimae Hollywood, sasa lets say, mtu akitaka kujua kuhusu msanii mkubwa wa hapa Bongo watu watamtaja Ray, lakini atakapoona Ray akiwa kavaa kama hivyo anavyoonekana kwenye hizo picha, nani atamchukulia serious?
Tatoos, hair style, nguo, vyote ni BIG NO.
Huyu hapa chini ni msanii wa Nigeria anaitwa Ramsey Nouh, kwanza muangalie anavyopangilia kila anapotoka, japo Ray ni handsome zaidi yake lakini kaka lazima achukuliwe serious kwa kila anachokifanya kutokana na yeye anavyouza kupitia muonekano wake tu. Ukimsimamisha Ramsey na Idris Elba wote unaweza kusema wasanii wa Hollywood,
RAMSEY NOUH
Ramsey msafi, kila kitu kwake kipo on point. hata movie zake ni lazima utamani kuziangalie ili umuone yeye tu.
RAY KWA KUA TUNAMPENDA NA KUMTEGEMEA AITANGAZE NCHI KUPITIA FILAMU ZAKE ZENYE UBORA, TUNGEMUOMBA ATILIE MKAZO SWALA LA MUONEKANO, LITAMFANYA MA KAMPUNI MBALIMBALI YAMTUMIE KAMA BALOZI WAO, ANAPOONEKANA NCHI NYINGINE ATAWAVUTIA WASANII WA HUKO KUTAKA KUFANYA NAE KAZI, PIA KAZI ZAKE ZITAONEKANA ZENYE UBORA ZAIDI KWANI UBORA SI TU KUTUMIA VIFAA VYA KISASA, BALI HATA MAVAZI PIA. KILA UNAPOTOKA UJIJUE WEWE SASA NI STAR HIVYO MATENDO NA MAVAZI YAKO NI MUHIMU SANA KWA KILA ANAYEKUTAZAMA.
NI HAYO TU KWA KAKA YETU LEO.
No comments:
Post a Comment