WEMA SEPETU
PRODUCER WA ENDLESS FAME CHIDY CLASSIC
Basi bwana katika pitapita zangu nikainyaka hii habari, kwamba inasemekana muigizaji wa bongo Wema Sepetu hawalipi wafanyakazi wake mIshahara, Hii habari imetokana na tuhuma alizopewa producer wa kampuni ya Wema inayoitwa ENDLESS FAME, producer huyo anayeitwa Chidy alipewa tuhuma kwamba kageuza magari ya Wema gest, na inavyosemekana Wema akaamua kumsimamisha kazi, baada ya kusimama kazi Chidi akaamua kueleza kwamba amesimama kazi kwasababu hakuwahi kupewa mshahara wake pale kwenye kampuni, maelezo ambayo yamepingwa vikali na kaka meneja Martin Kadinda, sasa sisi hatujui kama ni kweli au la, ila maoni ya watu wanasema inawezekana ni kweli ikizingatiwa kwamba kampuni ya Wema mpaka sasa haijaingiza movie yoyote sokoni, mimi kama mimi, kwasababu nawajua wote hawa watatu, ningependa kuwasihi tu wakae wayamalize kwani wametoka mbali, wasiyafaidishe magazeti, kila mmoja amemvumilia mwenzake sana mpaka kufika hapo walipofikia, tungependa kuona kampuni inaingiza movie sokoni ili wapenzi wa Wema tukazinunue na pia wapenzi wa Chidi wapate kuona mambo makubwa anayoyafanya chidi nyuma ya camera. NI HAYO TU.
No comments:
Post a Comment