Thursday, December 12, 2013

JACKLINE WOLPER NA MAJANGAZ


Hivi karibuni iliripotiwa kwamba muigizaji wa Tanzania Jackline Masawe Wolper amegonga magari yake wakati anayasogeza kuyaosha, inasemekana kwamba alikua anasogeza moja ya gari lake na bahati mbaya ikatokea akakanyaga mafuta badala ya break ndo hilo gari likaenda kugonga gari lake linguine dogo na pia akagonga ma tank ya maji na ma bomba.


                                          JACKLINE WOLPER




 


 
Hii picha hapo juu ndio magari ya Wolper na ma tank ya maji yalivyogongwa. Kwa kumbukumbu zangu, ndani ya mwaka huu, Wolper alipata majanga kadhaa yanayohusiana na magari, majanga hayo ni kama Wolper kupata matatizo na lile BMW lake mpaka likachukuliwa kwa kosa la kutokulipiwa ushuru, pia gari la Wolper liliwahi kutaka kuungua moto ilisemekana kuna mtu alirusha kitambaa chenye moto kwenye gari hilo lililokua limepark ndani ya nyumba ya msanii huyo.

No comments: