Sunday, December 29, 2013

WINNIE MANDELA

hii ni picha ya cover la movie iliyochezwa na wamerekani Janefer Hudson na Terrence Howard wakiigiza maisha ya mke wa aliyekua baba wa Africa mzee Nelson Mandela, movie hii inaonyesha maish aya Winnie Mandela toka alivyozaliwa mpaka sasa. ni nzuri sana hii movie u need to watch this. u can see how strong this woman is, she went through a lot in life.


picha ya cover la movie kwa nyuma

na huyu pia ni mMarekani anaitwa TERRENCE HOWARD ndie aliyecheza kama NELSON MANDELA

huyu mwanadada anaitwa JANEFER HUDSON ndie aliyeigiza kama WINNIE MANDELA ni mmarekani
 
 na hii ni picha ya kwenye movie wakiigiza Mandela alipoachiwa huru

hii ni picha halisi ya Mandela siku aliyoachiwa huru akiwa na Winnie


Hii picha ya walioigiza kama Winnie na Mandela

hii ni picha halisi ya WINNIE NA NELSON MANDELA

Hii ni picha ya kwenye movie wakiigiza harusi ya Winnie na Nelson Mandela
 
 hii hapa chini ni picha halisi ya harusi ya WINNIE NA NELSON MANDELA

hii ni picha ya kwenye movie hapa Winnie akipata mateso baada ya kufungwa gerezani

Friday, December 27, 2013

SHILOLE NA STEVE NYERERE JAMANI

Shilole ni mschana mzuri ambaye ni muigizaj wa bongo movie, huwa ni kawaida kwake kuandikwa magazetini ikizingatiwa yeye ni maarufu, amekua akiandikwa kupitia kazi zake na pia kupitia skendo za mapenzi, ila hii sasa naona inavuka mpaka, yani kwa mujibu wa gazeti moja, eti habari iliyowekwa kuhusu Shilole ni yeye kuibiwa simu, jamani nani anataka kusoma habari inayoelezea kua Shilole kaibiwa simu, yani inamaana Shilole kila kinachotokea kwake hata kama sio news anakipeleka kwa waandishi, jamani shilole jitahidi kutujulisha kuhusu kazi zako kupitia magazeti na sio vitu kama umeibiwa simu, inamaana kila anayeibiwa simu aandike gazeti sasa si kutakua hakuna nafasi za habari nyingine manake kuibiwa simu ni jambo la kawaida mjini.

 
SHILOLE
 
STEVE NYERERE
 
Huyu pia ni muigizaji na yeye habari iliandikwa kuhusu yeye ni kuibiwa Ipad na si habari za maana kama katoa movie mpya n.k

Thursday, December 26, 2013

DIAMOND NA WEMA SEPETU MAMBO INOGILE


                                                   WEMA NA DIAMOND


Fununu zinasema Diamond ameachana na aliyekua girlfriend wake Pen na karudi kwa girlfriend wake wa miaka yote muigizaji Wema Sepetu. kiukweli ninachopenda kwenye huu uhusiano ni jinsi Wema alivyompenda Diamond toka hana kitu Enzi hizo ndo anaanza kuwika, na kila mtu alikua anamdharau Wema na kumsema atatembeaje na motto wa kiswazi, ila walisahau kwamba mapenzi si hela, KAMA SWALA NI HELA UNGANENI MTAFUTE WOTE, CHA MSINGI NI MTU MWENYE TABIA NZURI.

                             TUWAACHE WALALE

Wednesday, December 25, 2013

MANGE KIMAMBI NA SINTAH WAUNGANA NA KUMKOSOA STELLA TILYA.

Mange Kimambi na muigizaji mwenye lips nzuri bongo Sintah, kwa nyakati tofauti kupitia blog zao wameungana katika hoja inayomuhusu msanii wa movie Kajala Masanja, Mange na Sintah ni mahasimu wakubwa na mara nyingi huwa wanapingana sana kwenye post zao. sasa basi kwa mara ya kwanza wameungana na kumtetea Kajala Masanja anayetuhumiwa kuiba mwanaume wa mwenzie.

                                                           MANGE KIMAMBI


                                                      SINTAH
 
 Hiki kisa kilianza hivi, Kajala alionekana katika picha akiwa na jamaa anaesemekana ni boyfriend wake, sasa kuna mschana mmoja anayekaa Marekani anaitwa Stella au kama anavyopenda kujiita Chaga Barbie, huyu stella kupitia mtandao wake wa instagram, aliweka picha ya Kajala na kuanza kulalamika kwamba kajala kaiba mwanaume wa rafiki yake, basi hii habari ikadakwa na Sintah na Mange, ambao japo wenyewe hawapatani lakini pia hawapatani kabisa kabisa na huyo Chaga Barbie, kwa hyo Sintah na Mange wakaanza kumnanga huyo chaga Barbie kwamba kakosa heshima kuanika mambo mitandaoni.

 
 
huyu ndie Kajala mwenyewe anayetuhumiwa kuiba mwanaume wa watu, ninachompendea Kajala huwa hapendi majibizano na mtu, huwa ni mpole hana makuu na hapendi magazeti,kwa hyo sakata hili Kajala hajajibu kitu, hali iliyomfanya chaga Barbie aonekane mjinga.
KAJALA MASANJA


Na hii picha ya hapa chini ndie STELLA au chaga Barbie mwenyewe, ni mwanamke mzuri ambaye haishi vituko kwenye mitandao, pia ni blogger, wachangiaji wengi wa Mange na Sintah wamemtuhumu huyu chaga Barbie kwa kumwambia yeye ndie kinara wa kuchukua waume za watu na mambo mengine mengi
 
MIMI NAUNGANA NA MANGE NA SINTAH. KWANZA KABISA HUYO ANAYELALAMIKA KAIBIWA MWANAUME SI MKE NI DEMU MTU, SASA KAMA JAMAA HAJAKUOA, NA ALIKUA NA WEWE SIKU ZOTE, ILA SASA KAAMUA KUA NA MWINGINE, UNALALAMIKA NINI? HII MANAKE NI KWAMBA HUYO JAMAA KAKUONA UNAMAPUNGUFU NDO MAANA KAENDA KWA MWINGINE AMBAYE WATAENDANA KITABIA, WASCHANA WENGI WAMEKUA WAKIWATESA MA BOYFRIEND ZAO, KUWANYANYASA NA KUWADHARAU,TENA IKITOKEA KAMZIDI KIPATO JAMAA NDO USISEME ATATAKA MPAKA ANAWISHWE MIGUU, HALAFU KAMA MWANAUME KAONA HAUFAI KUA MKE WAKE UTAMLAZIMISHA AKUOE JAMANI, SI LAZIMA ATAFUTE WA KUOA,  NDO MAANA MWANAUME PINDI ANAPOPATA MSCHANA ATAYEMUHESHIMU ANAAMUA KUHAMISHA MAJESHI, WE UNASHINDA KWENYE KOCHI UNAANGALIA TV, MWANAUME ATOKE KWENYE MIHANGAIKO JIONI KACHOKA, NDO AINGIE JIKONI APIKE, WE DEMU UMEKAA MGUU JUU, MWANAUME ASAFISHE NYUMBA, AJIFULIE NGUO, WE DEMU MCHANA KUTWA UMEKAA TU, HALAFU MWANAUME AKIMPATA WA KUMFULIA NA KUMPIKIA TENA MWANAMKE BOMBA ZAIDI YAKO UNAANZA KUPIGA KELELE NA KUITA MAJESHI YAKUSAIDIE. MIMI NAKEMEA TABIA YA KUTEMBEA NA MUME WA MTU TU, LAKINI SIO DEMU TU AMBAE TENA HUNA HATA URAFIKI NAE ANALALAMIKA UMEMUIBIA BOYFRIEND, KAMA ALIVYOSEMA MANGE, MBAYA NI KUMCHUKUA BOYFRIEND WA RAFIKI YAKO, LAKINI BOYFRIEND WA STRANGER?  ULIYEIBIWA NA KAJALA JICHUNGUZE, KAMA ULIKUA UNAJIFANYA WEWE NDO KIDUME NDANI YA NYUMBA NA KUMFANYA MWANAUME WAKO KAMA HOUSEBOY WA KUKUFANYIA USAFI NA KUKUPIKIA NDO HAYO KAJALA KANYANG'ANYA TONGE MDOMONI.

MERRY CHRISSMASS TO YU ALL



Monday, December 23, 2013

WEMA SEPETU AWA MU AFRICA



Hapa kuna picha inayomuonyesha muigizaji namba moja, nasema namba moja kwasababu yeye ndo muigizaji pekee wa kike anayeuza magazeti, yani habari ya huyu dada ikitoka lazima isomwe hata kama utafumba macho bado utaisoma tu, haya nirudi kwenye mada, hii ni cover ya magazine ya hapa Bongo inayoitwa VIBE, na toleo jipya wamemtoa Wema Sepetu, kwa wanaomjua Wema, wengi tunajua anarangi ya mwili kama ya mzungu yani ni mweupe sana, lakini kwenye hii picha wamemfanya Wema kua mweuzi kama mnavyoona, na pia hawajampigisha pamba, wamemvisha kanga, vazi la kinamama wa kiafrica na majani majani, wengi wametoa maoni yao na kusifu picha hii japo wengine wamesema u fake ulizidi sana.

HAYAWI HAYAWHI SASA YAMEKUA

Muigizaji mahiri wa Marekani GABRIELLE UNION na mcheza mpira wa kikapu DWYANE WADE wanatarajia kufunga ndoa hivi karibuni, Gabrielle ni mwanamama mwenye miaka 41 lakini hana motto na hana mpango wa kuzaa kwa sasa, na huyu kijana anamiaka 31, kwa hiyo mwanamke kamzidi mwanaume miaka 10.

                                             PICHA YA PETE YA ALMSI ALIYOVISHWA GABI
 
 
                                             GABRIELLE UNION na DWYANE WADE    
 
 
 Dwyane aliwahi kuoa hapo kabla, na kuzaa watoto wa wawili wakiume, baadae akatofautiana na mkewe huyo wa zamani ndo akaanzisha mahusiano na Gabrielle, hao watoto wa kiume wawili ni watoto wa Dwyane na mmoja ni mpwa wake
 
 
                                                     

inasemekana kwamba eti Dwyane alisaidiwa na hao watoto wake ku propose kwa Gabrielle,

Friday, December 20, 2013

WASTARA WA SAJUKI AMKUMBUKA MUMEWE


Wastara ni muigizaji aliyekua akipendana sana na mumewe mpenzi Sajuki, na yeye pia alikua muigizaji, lakini kwa bahati mbaya Sajuki sasa ni marehemu, hii picha inamuonyesha Wastara alivyokwenda kulitembelea kaburi la marehemu mumewe Sajuki.

BABY MADAHA KIBOKO



Hivi hizi style za nywele makucha na ma make huwa naziogopa manake haziendi na hali yetu halisi mwisho wa siku unakosa mume au wakwe wanakukataa kwa kukuona muhuni.

WEMA SEPETU ASHAURIWA KUA KAMA JOKETI MWEGELO

Hivi karibuni, miss Tanzania namba 2 wa mwaka 2006, alifanikiwa kufungua saloon kubwa ya wanawake, ikiambatana na clothing line yake inayoitwa KIDOTI, pia nywele yani weavs, mwanadada huyo anayeitwa Jokate Mwegelo, amekua hasimu mkubwa wa miss Tanzania namba 1 mwaka huo huo 2006 kutokana na mambo kadhaa, kwanza kabisa ni kitendo cha Wema kua namba moja na yeye kua namba 2 kwenye kinyang'anyiro cha u miss Tanzania, lakini kikubwa ni kitendo cha Joketi kutembea na aliyekua boyfriend wa Wema kwa kipindi hicho mwanamziki/muigizaji DIAMOND PLATNUMZ,
                                                                    WEMA SEPETU
 
WEMA SEPETU
 

 
                                  WEMA SEPETU NA MANAGER WAKE MARTIN KADINDA
 

Mashabiki wa Wema wamemuomba Wema angalau awe na vitega uchumi hasa katika kipindi hichi magazeti yanapomsema kwamba anaanza kufilisika, Wema ni star namba moja anayependwa sana na watu hivyo mashabiki hao wakawa wakitoa ushauri kwamba ikiwa Wema atafungua saloon kubwa au duka la nguo basi ataweza sana kupata wateja kutokana na jinsi anavyopendwa na watu, na pia wamemshauri hivyo kufwatia mpinzani wake Jokate kuonekana akifanya sana mambo ya maendeleo kuliko Wema ambaye wanamtuhumu sana kwa kutumia hela kwa mambo yasiyo ya msingi kama shoping ya mbwa wake kufanyika china, mara kukodi ndege kwenda Arusha, mara kuwatunza wanamziki hela nyingi sana majukwaani, wengi wamemuomba Wema kuanza kuweka vitega uchumi kwani uzuri unamwisho, na pia umri unaenda, hivi sasa ndo kipindi cha yeye kuwekeza,
 
 
       HII NI PICHA YA JOKATE MWEGELO MPINZANI MKUBWA WA WEMA


Hii ni saloon ya Jokate iliyofunguliwa hivi karibuni
 
                                      saloon ya Jokate
 

 

Thursday, December 19, 2013

WOLPER JACKLINE NA ZAMARADI MKETEMA BEEF ZITO

Eti inasemekana kwamba, muigizaji mwenye macho mazuri nchini Jackline Wolper anabeef na mtangazaji wa kipindi cha movie kinachoitwa TAKE ONE cha Clouds Tv anayeitwa Zamaradi Mketema, sababu ya beef ni nini? eti Wolepr hataki jinsi Zamaradi anavyozungumzia ishu zake kwenye kipindi chake, mfano ishu ya yeye kubadili dini kua muislam kwasababu ya pesa za dalas na kadhalika.
                                                             

                        JACKLINE WOLPER

                                 ZAMARADI MKETEMA
Sasa jamani, Zamaradi yeye anafanya kazi yake, inamaana anavyozirushaga movie zenu na kuzitangaza mbona hamchukii, yani pale mnapokosea pia ni lazima mkosolewe, wasanii wa Tanzania hasa wa movie kwakweli huwa wanawapa wakati mgumu sana watangazi na waandishi, yani wenyewe wanapenda waandikwe kwa mazuri tu, wakati mazuri wanayofanya ni machache, wamejaa skendo kila kukicha, mara huyu kahongwa gari, mara huyu kafumaniwa, mara huyu anatembea na mume wa mtu mara huyu hivi, sasa watu kama wakina zamaradi wasipoelezea na mabaya yenu basi vipindi vyao vitakua havina maana.

WAPENDANAO

Hawa ni wapenzi wanaovutia watu wengi hiko Nigeria, huyo jamaa ni muigizaji wa Nigeria anayeitwa Jim Iyke na huyo mschana ni mpenzi wake ambaye ni muigizaji wa Ghana anaitwa Nadia Buari

Wednesday, December 18, 2013

RAY KIGOSI NA LULU MMMHHHHH........

Ray Kigosi nampongeza sana kwa kuhakikisha anakua na mwili wa star, yani sio minyama uzembe na kitambi, zamani alikua kibonge sana lakini hivi sasa Ray kajipunguza na ni jambo la kumpa pongezi, tunae katoto ketu ka bongo movie LULU, nasema katoto kwasababu ni kweli katoto ka  miaka kumi na nane tu japo mambo yake makubwa, ka Lulu bwana na kenyewe kameamua kuachana na ulaji mbovu na uvivu kameamua kuingia gym ili kawe na mwonekano mzuri na afya bora.

                                                      LULU

                                      LULU (hapo katika mambo ya selfie)
 
 
                                             RAY KIGOSI
 

 
          Na hapa chini ni picha ya Ray baada ya kupungua

WEMA SEPETU AFILISIKA......NI KWELI? AU UZUSHI?

Kama tunavyojua si kila kinachooandikwa kwenye magazeti ya udaku kina ukweli, kuna hii habari nimekutana nayo kwenye gazeti moja ya kwamba Wema Sepetu msanii wa Bongo movie amefilisika, kwa mujibu wa gazeti hilo eti Wema ameshaanza kuuza magari yake na siku hizi kapunguza kujirusha, kuuza magari kuna mawili, inawezekana kaona haina sababu ya kua na magari matatu wakati moja linamtosha, na kuhusu kutoka wengi tunajua Wema si mtokaji sanalabda kuwe na event maalum,

 
 
IKIWA NI KWELI WEMA YUKO KWENYE KIPINDI KIGUMU KIFEDHA BASI TUNAMUOMBEA KWA MUNGU ILI AMPITISHE KWENYE HII HALI, JAMBO HILI SI LA KUCHEKA KWANI NI HALI INAYOWEZA KUMKUTA YOYOTE NA SI YA KUDUMU KWANI MTOAJI NI MUNGU HIVYO KESHO TU UNAWEZA KUMKUTA KAFANIKIWA MARA MBILI YA SASA.