NADIA BUARI
Nadia Buari alizaliwa mwaka 1982 nchini Ghana, ni binti wa mwanamziki mkongwe wa nchini humo Alhaji Sidiku Buari. Nadia ana degree ya BFA aliyoipata katika chuo kikuu cha Legon nchini Ghana.
Nadia alianza fani hii ya maigizo katika tamthilia iliyokua ikirushwa nchini humo iliyokua ikiitwa Games people play. movie yake ya kwanza inaitwa Mummy's daughter. Mpaka sasa Nadia ameshacheza movie zaidi ya 20.
NADIA NA MAMA YAKE MZAZI
Nadia amekua akionekana mara kwa mara na mama yake kuliko baba yake na hii ni kutokana na kwamba wazazi wake hawa walitengana.
NADIA AKIWA NA MAMA PAMOJA NA BABA YAKE WA KAMBO
Licha ya Nadia kuwa maarufu nchini kutokana na kazi yake ya uigizaji, lakini pia familia yake nzima ni ya watu maarufu, Nadia anaye mdogo wake ambaye alikua Miss Ghana mwaka 2002 anaitwa Shaida Buari na pia anaye kaka yake ambaye ni mcheza mpira maarufu Ghana anayeitwa Malik Buari.
huyu ni kaka yake na Nadia anaitwa Malik Buari
Hata hivyo nadia amekua akihusishwa na story mbalimbali za mapenzi ambapo inasemekana alikua na uhusiano na muigizaji mwenzake ambaye nae pia ni maarufu sana Africa Van Vicker.
NADIA NA VAN VICKER
Nadia hivi sasa ni girlfriend wa muigizaji maarufu wa nchini Nigeria Jim Iyke.
No comments:
Post a Comment