Movie hii inayotarajiwa kutoka july mwakani, imeandikwa na Chriss Morgan na director wake ni James Wan. Mwezi huu wa tisa ndio movie hii wameanza kui shoot, humo ndani watakaokuwepo ni Vin Diesel, Paul Walker, Dwayne Johnson, Tyrese Gibson, Jason Stantham na Lucas Black.
hapo kwenye hii picha anaonekana vin Diesel na Justin Beaber, wengi walijiuliza kulikoni Justin awepo kwenye trailer ya Fast n furious 7? jibu ni kwamba hyo trailer sio official, Justin hatokuwepo kwenye hii movie, ila Justin kwa jinsi anavyotuhumiwa kukimbiza magari yake huko Marekani angependeza sana kukimbiza magari na kwenye hii movie pia.
Hapo chini ni picha ya muigizaji kutoka India ( Bollywood) anaitwa Deepika Padukone, huyu kwenye fast n furious six alikuwepo lakini kwenye 7 hatokuwepoo kutokana na kua na ratiba ya kucheza movie na Shuhrukh Khan inayoitwa Happy new year, kutokana na fast nn furious 7 kurekodiwa haraka yani haijapishana sana na fast n furious 6 ndo maana imemuwia vigumu Deepika kuwepo.
Kwa mnaompenda Jason Stantham basi naye safari hii atakuwepo kajaa tele, jamaa huyu naye mkali sana wa movie za action
kama kawaida police lazima awepo kulinda amani, huyu ni Dwayne Johnson huwa ana act kama police nafasi anayoimudu vilivyo. Jamaa kapanda halafu kajazia balaa yani jambazi akaimuona tu anasalim amri mwenyewe
hawa kwenye movie huwa wanaukaribu sana majina yao ya kwenye movie ni Bryan na mwenye upara ni Torreto ila majina yao halisi ni Paul Walker na wa upara ni Vin Diesel
PAUL WALKER NA VIN DIESEL
LUDACRISS NA TYRESE GIBSON
Ludacriss na Tyrese kwa wale wasiofahamu ni wanamziki pia.
No comments:
Post a Comment