basi leo nakuletea director wa hii hizi movie, movie hizi kwa kweli ni tishio mpaka leo, huyu director kwa kazi nzuri aliyoifanya miaka hiyo ya 70 mpaka yeye mwenyewe anajiogopa kwamba hivi sasa asije aka direct movie isiyo na kiwango ikamshushia heshima yake aliyojijengea kwenye THE GOD FATHER NA APOCALYPSE.
FRANCIS FORD COPPOLA
Coppola alizaliwa April 7 mwaka 1939. ni mmarekani mwenye asili ya Italy. Baada ya Coppolo kuhitimu masomo yake, alifunga ndoa na Eleanor, kipindi hicho Coppola alikua na umri wa miaka 22 tu. week chache baada ya kuoa ambapo Coppola anakiri kwamba alioa akiwa hana kitu yani hana hela, lakini baada ya week chache ndipo alipoanza kupata kazi za ku direct movie.
COPPOLO AKIWA LOCATION
Coppola alijizolea umaarufu na kujijengea heshima duniani pale alipodir ect movie ya THE GOD FATHER 1 NA THE GOD FATHER 2. inasemekana kwamba ma producer kadhaa walikataa kudirect movie hiyo, Paramount studio ambao ndo waliopruduce movie hiyo waliamua kumfwata Coppola a direct THE GOD FATHER huku sababu ikiwa ni u asili wake wa Italia, kutokana na movie ya God father kuhusisha mambo ya Italy basi Paramount waliona Coppola ndo director sahihi kabisa wa movie hiyo.
Coppola alikubali kazi ya kudirect THE GOD FATHER na movie ikatoka mwaka 1972 ambapo ilikua tishio na ilimfanya Coppola kupata tuzo nyingi, mwaka 1974 Coppola alitoa GOD FATHER part 2, kabla ya kutoa part two alikua anahofia mapokeo ya watu yatakuwaje naalikua anahisi watu wanaweza wakawa wameshatosheka na part one. Movie hii ya THE GOD FATHER ilitokana na novel ya THE GOD FATHER iliyoandikwa na muitaliano Mario Puzo ambayo ilikua ikielezea maisha ya familia ya familia ya kimafia ya kiitaliano.
Coppola ni mume wa Eleanor Coppola na pia ni baba wa watoto watatu ambapo mmja alifariki mwaka 1986 katika ajali ya boat.
Gian carlo coppola ni motto wa kwanza wa Francis coppola ambaye alizaliwa mwaka 1963 na kufariki mwaka 1986. kijana huyu katika kipindi cha uhai wake alikua anafwata nyayo za baba yake za kudirect na ku act movies. kwenye movie ya THE GOD FATHER aliigiza kama motto wa Robert Duvall. Wakati anafikwa na mauti alikua na mchumba aliyeitwa Jacqui de la fontaine ambaye alikua na ujauzito wa miezi miwili, ambapo mwaka 87 motto wa kike wa marehemu Gian carlo coppola alizaliwa na kupewa jina la Gian Carla coppola .
Roman Coppola kama unavyomuona hapo juu upande wa kushoto, yeye ni motto wa pili wa Francis Coppola, alizaliwa mwaka 1965, na yeye pia ni director na ni actor, pia alikuwepo kwenye movie ya THE GOD FATHER 2 na aliigiza kama Santino Corleone akiwa mdogo. kwa kifupi ni kwamba director Francis Coppola alihakikisha pia watoto wake nao wanashiriki kwenye movie ya THE GOD FATHER.
Sofia Coppola ndie binti wa motto wa mwisho na binti wa pekee wa Directo Coppola, yeye alizaliwa mwaka 1971, pia kama ilivyokua kwa kaka zake na yeye amefwata nyayo za baba yake za u director na uigizaji wa movie, binti huyu pia amecheza movie ya baba yake iliyojizolea umaarufu ya THE OUTSIDER.
Gian amezaliwa mwaka 1987. Hamjui baba yake kwani wakati anazaliwa baba yake alikua ameshafariki. Kama ilivyokua kwa aunt yake, uncle pamoja na babu yake, na yeye pia ni director anayekuja kwa kasi kabisa huko Hollywood.
HII NDO FAMILIA NA MAISHA YA DIRECTOR FRANCIS FORD COPPOLA, JINSI ALIVYOTINGISHA DUNIA KWA MOVIE ZAKE ZINAZOTAZAMWA BILA KUCHOKA TOKA MIAKA YA 70 MPAKA SASA. NA JINSI FAMILIA YAKE YOTE INAVYOFUATA NYAYO ZAKE NA KUA TISHIO HUKO HOLLYWOOD.
No comments:
Post a Comment