wema sepetu. miss Tanzania wa mwaka 2006
Wema ni muigizaji mwenye mafanikio makubwa sana kwenye tasnia hii ya filamu. Wema mpaka sasa amefanikiwa kufungua kampuni yake ya movie na ameshaproduce movie zisizopungua tano na ameshacheza movie nyingi sana.
Irine uwoya. miss Tanzania namba 5 mwaka 2006.
Irine Uwoya pia amepata mafanikio makubwa sana kupitia sanaa hii ya maigizo, ameweza kujizolewa maelfu ya mashabiki Africa mashariki na kati, pia ameshatengeneza movie zake mwenyewe kadhaa. irine ni mke wa mcheza mpira wa Rwanda Hamad Ndikumana, na pia hivi sasa Irine anatamba na reality show yake inayorushwa na kituo cha Clouds tv.
AISHWARYA RAI BATCHAN miss world mwaka 1994
Hivi sasa mwanamama huyu ndie anayeshika namba tatu kwa kupokea mshiko mkubwa kwenye uigizaji. pia ameolewa na muigizaji mwenzie Abhishek Batchan mototo wa Amitah Batchan na wanamtoto mmoja wa kike.mwanamama huyu ameshacheza movie nyingi sana lakini iliyovutia wengi ni ile aliyocheza na mumewe abhishek, movie hiyo inaitwa Kuch na kha ho.
PRIYANKA CHOPRA miss world 2000.
binti huyu ndie muigizaji wa kike anayeeongoza kwa kulipwa pesa ndefu huko Bollywood. lakini alianza fani hiyo baada ya kupita kwanza kwenye mashindano ya urembo.
Siku hizi kumekua na malalamiko hapa Bongo kwamba waschana wanaotoka kwenye fani za urembo wanavamia fani ya uigizaji. sasa sijui kwa huko Bollywood kama na kwenyewe kuna malalamiko hayo hasa ukizingatia waigizaji wa kike wanaong'aa zaidi duniani wa huko Bollywood wengi wamepitia mashindano ya urembo.
No comments:
Post a Comment