Sunday, September 15, 2013

MOVIE STAR WA WEEK

Kila mwisho wa week na katikati ya week nitakua nawaletea wasifu wa muigizaji, tanzanite blog ni blog ambayo inajumuisha kila kitu kinachohusu sanaa ya maigizo duniani, hivyo waigizaji nitakaokua na waletea humu si kutoka Tanzania peke yake bali ni dunia nzima. leo tunaanza na muigizaji mrembo kutoka marekani nae ni.

                    GABRIELLE UNION.
 
Mdada huyu kwanza kabisa umri wake ni tofauti na anavyooneka, hapo alipo ni mwanamke mwenye miaka 40. ila hajazaa na wala hajaolewa, lakini pia ukimuangalia unaweza ukasema anamiaka 25 kwa jinsi alivyoweza kujitunza. Gabrielle alizaliwa oct 29 mwaka 1972 huko Omaha Nebraska nchini Marekani. mwanadada huyu licha ya kazi yake uigizaji pia alikua model. Gabrielle inasemekana alipokua na umri wa miaka 19 aliwahi kuvamiwa akiwa anatoka kazini na kubakwa ambapo baadae mbakaji huyo aliamua kujisalimisha na sasa anatumikia kifungo cha miaka 33 jela. Gabrielle mpaka sasa ameshacheza movie nyingi zilizomletea umaarufu na mafanikio mengi aliyonayo hivi sasa.
 
Huyo ni Gabrielle Union akiwa na boyfriend wake mcheza basket Dwyane Wade
 
Dwyane Wade ni mdogo sana kiumri kwa Gabrielle, ambapo inasemekana Dwyane alizaliwa mwaka 1982 na Gaby mwaka 1972 kwa hyo mwanamke kamzidi mwanaume miaka kumi hapo. wapenzi hawa walianza mapenzi yao muda mrefu ambapo mpaka sasa hajafikia maamuzi ya kufunga ndoa hasa kutokana na kwamba Dwyane alikua na mke na watoto hivyo wamekua na matatizo ambayo mpaka ilifikia hatua ya kupelekana mahakamani na mama watoto wake.

No comments: