Monday, September 30, 2013

THE EXPENDABLE MOVIE IPO JIKONI

Ile movie inayojumuisha wakali wa movie za action duniani THE EXPENDABLE 3 ipo mbioni kukamilika,

 
hii movie imeandikwa na SYLVESTER STALLON au kama wengi wanavyomfahamu kwa jina Rambo. na director wa movie hii ni PATRIC HUGHES.
 
 
  hii picha hapa chini inawaonyesha wakali wa movie hii ambao ni tishio kwa movie za action duniani. wa kwanza hapo ni DOLPH LUNDGREN, SYLVESTER STALLON au Rambo, ARNOLD SCHWARZENEGGER au kibongobongo (shosniga) na wa mwisho ni JEAN CLAUD au kama anavyofahamika na wengi kwa jina la Van Dame.
 
 
                                              SYLVESTER STALLON (RAMBO)
 
Huyu ndie muandshi wa story ya hii movie.

Sunday, September 29, 2013

AISHWARYA BATCHAN NDIE MOVIE STAR WETU WA WEEK

Aishwarya ni muigizaji wa Bollywood kwa wale msiomjua.


                                                AISHWARYA RAI BATCHAN
 
Aishwarya alizaliwa mwaka 1973 huko Mangalore nchini India.
 
 

 
 
Kabla Aishwarya hajaingia rasmi kwenye movie, alikua ni binti anayetaka kusomea mambo ya medicine, lakini aliamua kuanza kufanya modeling akiwa na umri mdogo hivyo kujikuta akiwa zaidi kwenye mdeling na sio kwenye medicine, baada ya hapo Aishwarya alipata nafasi ya kua miss India na baadae akawa miss World mwaka 1994. baada tu ya kupata taji la miss World, Aishwarya alianza mialiko ya kucheza movie mbalimbali na hayo ndo yakawa maisha yake mpaka sasa. Zipo movie nyingi ambazo ameshacheza mpaka sasa huko Bollywood mfani ni Devdas ilimpa umaarufu sana pamoja na Khake.
 
 
                                             AISHWARYA NA MUMEWE ABHISHEK BATCHAN siku ya harusi
 
Mwaka 2007 Aishwarya alifanikiwa kufunga ndoa na muigizaji mwenzake Abhishek Batchan, Abhishek ni motto wa muigizaji mkongwe nchini India Amitah batchan.
 
 
                                            Aishwarya akichekelea baada ya kua mrs Batchan
 
Aishwarya na mumewe wameshacheza movie pamoja, baadhi ya movie hizo ni kama SARKAR, hii movie na Amitah alikuwepo pia, movie ya BUNT&BABLY ambayo pia Amitah alikuwepo na Kuch na kaho waliyocheza wenyewe wawili tena kama wapenzi.
 
 
 
                hapa AISHWARYA NA ABHISHEK wakiwa kwenye private jet wakienda honey moon



                                               Aishwarya na mumewe na mzee mwenye miwani ndio AMITAH BATCHAN baba wa ABHISHEK.
 
 
 
 Hapa Aishwarya akiwa na mumewe pamoja na wazazi wake
 
 
 
                              AISHWARYA AKIWA NA MTOTO WAKE WA PEKEE
Aishwarya alifanikiwa kupata motto wake wa kwanza mwaka mmoja uliopita na kumpa jina la AARADHYA.
 
 
                        Aishwaria akiwa kwenye red carpet huko Hollywood, pembeni yake namuona EVA LONGORIA.
 Licha ya kua ni muigizaji wa india lakini pia Aishwarya ameshacheza movie kama tano hivi za Hollywood.
 
 

Saturday, September 28, 2013

HAPPY BDAY WEMA SEPETU

 Naipenda sana hii picha kwasababu huwezi kuikuta sehemu nyingine yoyote zaidi ya hapa.

NAPENDA SANA NIKIONA MTU KAVAA NGUO INAYOITANGAZA TANZANIA.

Msanii wa movie  kutoka Ghana Van Vicker akiwa Tanzania.


                                                            VAN VICKER

inapendeza kwakweli hasa ukiangalia si mtanzania lakini anaitangaza nchi yetu kupitia jezi ya Taifa stars.



       Hapa chini ni picha ya mdau mzuri sana wa movie za Bongo Biko Molteni.

                                                               BIKO MOLTENI
 
Biko Molteni  ni kijana mwenye asili ya Italy, na pia ni director na producer wa movie mtarajiwa,
 
 
Kinachonifurahisha ni jinsi wadau hawa wa movie ambao sio watanzania lakini wanaonyesha uzalendo kwa nchi yetu.

Friday, September 27, 2013

MOVIE MPYA YA BEN AFFLECK NA JUSTIN TIMBERLAKE

Movie mpya ya RUNNER RUNNER ambayo imechezwa na wakali wa movie Hollywood Ben Affleck pamoja na Justin Timberlake inatarajiwa kuzinduliwa rasmi siku ya tarehe 4 oct 2013.


                                                    COVER LA MOVIE
 
Movie hii imeandikwa na Bryan Coppelman na David Levian, na director wake ni  Brad Fulman, waliokuwepo ndani ya movie hii ni Ben Affleck, Justin Timberlake na Gemma Arterton,
 
 
 
                                            JUSTIN TIMBERLAKE, BEN AFFLECK
 
 
Hii picha hapa chini Ben akiwa kwenye hiyo movie

 



                                             Justin na Ben kwenye movie
 
 
PRODUCER WA HII MOVIE PIA NI MOVIE STAR MKALI DUNIANI LEONARDO DICAPRIO,
  Dicaprio kwa wale mliomsahau au wale msiomjua ndie aliyecheza movie maarufu duniani ya TITANIC.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Thursday, September 26, 2013

MOVIE YA KEEPING MY MAN YA RUKKY SANDA IPO TAYARI

Ile movie iliyokua inazungumziwa mara kwa mara na mitandao mingi ya kinaigeria ya Rukky Sanda sasa ipo tayari, Rukky Sanda amezindua movie yake hii inayoitwa KEEPING MY MAN huko Lagos kwenye hotel wheatbaker.


                                                          RUKKY SANDA
Movie hii inahusu maisha ya ndoa na migogoro yake, yani kwa ujumla imeelezea mapenzi hasa kwa wanandoa. Ndani ya movie kali kuna mastar wanaotambulika Africa kama Ini Edo, Ramsey Noah na Monalisa Chinda.


                                 picha hii inamuonyesha Rukky Sanda akiwa na Ini Edo wakiact hii movie
 
 
 
                                   picha hii ya chini inamuonyesha Monalisa Chinda akiwa anact hiyo movie pia.


                                         na hii picha inamuonyesha Ramsey Noah akiwa anaigiza hiyo movie.
 
MONALISA CHINDA

Monalisa ameshacheza movie nyingi na ni maarufu kwa hyo kucheza kwake kwenye hii movie kutaifanya hii movie iwe na msisimko.


                                                       RAMSEY NOAH NA INI EDO
 
 
Hawa ndo wenyewe hawa yani ukiwakuta tu kwenye movie kaa uiangalie lazima hiyo movie itakua bomba, sasa kwenye hii movie watakuwepo,  Ramsey nae umri unamtupa mkono lakini anajitahidi kuaendana na wakati unaweza kufikiri anamiaka 30, na Ini Edo nae ndo sina cha kusema kwasababu nampenda kupita maelezo.

Wednesday, September 25, 2013

WAIGIZAJI HAWA WANAVYOPENDEZA NA NGUO ZA KIAFRIKA

Hapo juu ni Wema Sepetu kutoka bongo movie, yeye kavalia vazi lililoshonwa na kitambaa cha kimasai.
 
                                                       JACKIE WOLPER
 
Wolper hapo juu kavalia vazi la kitenge.
 
                                            GENEVEIVE NNAJI
 Geneveive yeye katokelezea na vazi la kinaija zaidi,
                                       
                                                   OMOTOLA JELADE IKINDE
 Bidada Omosex nae katokelezea na kitenge chake na yeye ni muigizaji kutoka Nigeria

                                                        JACKIE APPIAH
Jackie nae ametokelezea na kitenge chake, yeye ni muigizaji kutoka Ghana.
 
 
                                            NADIA BUARI
Nadia kutoka Ghana nae katokelezea na kitenge kwenye red carpet.
 
Hawa ni wasanii maarufu Afrika ambao huwa wanapendeza sana lakini nimeona wakivaa kiafrika wanapendeza zaidi, nilitamani kukuletea wa Hollywood lakini too bad hawana mavazi ya asili, kweli waafrica tunabahati sana

MOVIE DIRECTOR ALIYETIKISA DUNIA HUYU HAPA.

Unaijua movie ya THE GOD FATHER na APOCALYPSE NOW?
 basi leo nakuletea director wa hii hizi movie, movie hizi kwa kweli ni tishio mpaka leo, huyu director kwa kazi nzuri aliyoifanya miaka hiyo ya 70 mpaka yeye mwenyewe anajiogopa kwamba hivi sasa asije aka direct movie isiyo na kiwango ikamshushia heshima yake aliyojijengea kwenye THE GOD FATHER NA APOCALYPSE.
                                                          
                                                  FRANCIS FORD COPPOLA
 Coppola alizaliwa April 7 mwaka 1939. ni mmarekani mwenye asili ya Italy. Baada ya Coppolo kuhitimu masomo yake, alifunga ndoa na Eleanor, kipindi hicho Coppola alikua na umri wa miaka 22 tu. week chache baada ya kuoa ambapo Coppola anakiri kwamba alioa akiwa hana kitu yani hana hela, lakini baada ya week chache ndipo alipoanza kupata kazi za ku direct movie.



                                           COPPOLO AKIWA LOCATION
Coppola alijizolea umaarufu na kujijengea heshima duniani pale alipodir ect movie ya THE GOD FATHER 1 NA THE GOD FATHER 2. inasemekana kwamba ma producer kadhaa walikataa kudirect movie hiyo, Paramount studio ambao ndo waliopruduce movie hiyo waliamua kumfwata Coppola a direct THE GOD FATHER huku sababu ikiwa ni u asili wake wa Italia, kutokana na movie ya God father kuhusisha mambo ya Italy basi Paramount waliona Coppola ndo director sahihi kabisa wa movie hiyo.
 
                                                  FRANCIS COPPOLA AKIWA KIJANA
 
Coppola alikubali kazi ya kudirect THE GOD FATHER na movie ikatoka mwaka 1972 ambapo ilikua tishio na ilimfanya Coppola kupata tuzo nyingi, mwaka 1974 Coppola alitoa GOD FATHER part 2, kabla ya kutoa part two alikua anahofia mapokeo ya watu yatakuwaje naalikua  anahisi watu wanaweza wakawa wameshatosheka na part one. Movie hii ya THE GOD FATHER ilitokana na novel ya THE GOD FATHER iliyoandikwa na muitaliano Mario Puzo ambayo ilikua ikielezea maisha ya familia ya familia ya kimafia ya kiitaliano.
 
                                                          FRANCIS COPPOLA NA MKEWE ELEANOR
Coppola ni mume wa Eleanor Coppola na pia ni baba wa watoto watatu ambapo mmja alifariki mwaka 1986 katika ajali ya boat.
 
                                                   GIAN CARLO COPPOLA
Gian carlo coppola ni motto wa kwanza wa Francis coppola ambaye alizaliwa mwaka 1963 na kufariki mwaka 1986. kijana huyu katika kipindi cha uhai wake alikua anafwata nyayo za baba yake za kudirect na ku act movies. kwenye movie ya THE GOD FATHER aliigiza kama motto wa Robert Duvall. Wakati anafikwa na mauti alikua na mchumba aliyeitwa Jacqui de la fontaine ambaye alikua na ujauzito wa miezi miwili, ambapo mwaka 87 motto wa kike wa marehemu Gian carlo coppola alizaliwa na kupewa jina la Gian Carla coppola .
 
 
 pichani hapa chini wa kwanza ni motto wa Coppola anayeitwa Roman coppola na baba yake na dada yake pamoja na mama yao.
Roman Coppola kama unavyomuona hapo juu upande wa kushoto, yeye ni motto wa pili wa Francis Coppola, alizaliwa mwaka 1965, na yeye pia ni director na ni actor, pia alikuwepo kwenye movie ya THE GOD FATHER 2 na aliigiza kama Santino Corleone akiwa mdogo. kwa kifupi ni kwamba director Francis Coppola alihakikisha pia watoto wake nao wanashiriki kwenye movie ya THE GOD FATHER.
 
                                            FRANCIS COPPOLA NA BINTIYE SOFIA COPPOLA
 
Sofia Coppola ndie binti wa motto wa mwisho na binti wa pekee wa Directo Coppola, yeye alizaliwa mwaka 1971, pia kama ilivyokua kwa kaka zake na yeye amefwata nyayo za baba yake za u director na uigizaji wa movie, binti huyu pia amecheza movie ya baba yake iliyojizolea umaarufu ya THE OUTSIDER.
 
 
                          huyu ni mjukuu wa Coppola ambaye baba yake ndo motto wa kwanza wa Coppola aliyefariki na kumuacha mchumba wake akiwa na ujauzito. Binti huyu anaitwa Gian Carla Coppola
 
Gian amezaliwa mwaka 1987. Hamjui baba yake kwani wakati anazaliwa baba yake alikua ameshafariki. Kama ilivyokua kwa aunt yake, uncle pamoja na babu yake, na yeye pia ni director anayekuja kwa kasi kabisa huko Hollywood.
 
HII NDO FAMILIA NA MAISHA YA DIRECTOR FRANCIS FORD COPPOLA, JINSI ALIVYOTINGISHA DUNIA KWA MOVIE ZAKE ZINAZOTAZAMWA BILA KUCHOKA TOKA MIAKA YA 70 MPAKA SASA. NA JINSI FAMILIA YAKE YOTE INAVYOFUATA NYAYO ZAKE NA KUA TISHIO HUKO HOLLYWOOD.

Monday, September 23, 2013

FAST AND FURIOUS 7 INATOKA MWAKANI, UNAJUA NANI ATAKUWEPO NA NANI HATOKUWEPO?

Naimani kwa wale wapenzi wa movie mmeshaona movie za fast and furious, zipo part one mpaka six, hii six ndo ilitoka mwaka huu na ikawa gumzo midomoni mwa watu. sasa FAST AND FURIOUS 7 ipo jikoni.
Movie hii inayotarajiwa kutoka july mwakani, imeandikwa na Chriss Morgan na director wake ni James Wan. Mwezi huu wa tisa ndio movie hii wameanza kui shoot, humo ndani watakaokuwepo ni Vin Diesel, Paul Walker, Dwayne Johnson, Tyrese Gibson, Jason Stantham na Lucas Black.


hapo kwenye hii picha anaonekana vin Diesel na Justin Beaber, wengi walijiuliza kulikoni Justin awepo kwenye trailer ya Fast n furious 7? jibu ni kwamba hyo trailer sio official, Justin hatokuwepo kwenye hii movie, ila Justin kwa jinsi anavyotuhumiwa kukimbiza magari yake huko Marekani angependeza sana kukimbiza magari na kwenye hii movie pia.

 
Hapo chini ni picha ya muigizaji kutoka India ( Bollywood) anaitwa Deepika Padukone, huyu kwenye fast n furious six alikuwepo lakini kwenye 7 hatokuwepoo kutokana na kua na ratiba ya kucheza movie na Shuhrukh Khan inayoitwa Happy new year, kutokana na fast nn furious 7 kurekodiwa haraka yani haijapishana sana na fast n furious 6 ndo maana imemuwia vigumu Deepika kuwepo.
 
                                                      DEEPIKA PADUKONE
 
Kwa mnaompenda Jason Stantham basi naye safari hii atakuwepo kajaa tele, jamaa huyu naye mkali sana wa movie za action

 
kama kawaida police lazima awepo kulinda amani,  huyu ni Dwayne Johnson huwa ana act kama police nafasi anayoimudu vilivyo. Jamaa kapanda halafu kajazia balaa yani jambazi akaimuona tu anasalim amri mwenyewe
 
                                                       DWAYNE JOHNSON

hawa kwenye movie huwa wanaukaribu sana majina yao ya kwenye movie ni Bryan na mwenye upara ni Torreto ila majina yao halisi ni Paul Walker na wa upara ni Vin Diesel

                                                      PAUL WALKER NA VIN DIESEL
 
 
 Ma meen Ludacriss nae kama kawaida ndani ya nyumba na kwenye sekta ya uongeaji pumba na vichekesho vya hapa na pale kama kawaida Tyrese Gibson kajaa tele.

                                          LUDACRISS NA TYRESE GIBSON
 
Ludacriss na Tyrese kwa wale wasiofahamu ni wanamziki pia.

Sunday, September 22, 2013

STAR WA WEEK HII NI NADIA BUARI MUIGIZAJI KUTOKA GHANA



                                                            NADIA BUARI
 
Nadia Buari alizaliwa mwaka 1982 nchini Ghana, ni binti wa mwanamziki mkongwe wa nchini humo Alhaji Sidiku Buari. Nadia ana degree ya BFA aliyoipata katika chuo kikuu cha Legon nchini Ghana.


 
Nadia alianza fani hii ya maigizo katika tamthilia iliyokua ikirushwa nchini humo iliyokua ikiitwa Games people play. movie yake ya kwanza inaitwa Mummy's daughter. Mpaka sasa Nadia ameshacheza movie zaidi ya 20.
 
NADIA NA MAMA YAKE MZAZI


Nadia amekua akionekana mara kwa mara na mama yake kuliko baba yake na hii ni kutokana na kwamba wazazi wake hawa walitengana.


                                            NADIA AKIWA NA MAMA PAMOJA NA BABA YAKE WA KAMBO
 
Licha ya Nadia kuwa maarufu nchini kutokana na kazi yake ya uigizaji, lakini pia familia yake nzima ni ya watu maarufu, Nadia anaye mdogo wake ambaye alikua Miss Ghana mwaka 2002 anaitwa Shaida Buari na pia anaye kaka yake ambaye ni mcheza mpira maarufu Ghana anayeitwa Malik Buari.
 
 
                    NADIA AKIWA NA BABA YAKE SIDIKU BUARI PAMOJA NA MDOGO WAKE SHAIDA BUARI.
 
 
huyu ni kaka yake na Nadia anaitwa Malik Buari

 
Hata hivyo nadia amekua akihusishwa na story mbalimbali za mapenzi ambapo inasemekana alikua na uhusiano na muigizaji mwenzake ambaye nae pia ni maarufu sana Africa Van Vicker.
 
NADIA NA VAN VICKER

 
 
                                                 NADIA BUARI NA JIM IYKE
 
Nadia hivi sasa ni girlfriend wa muigizaji maarufu wa nchini Nigeria Jim Iyke.