VAN VICKER NA WEMA SEPETU
Muigizaji kutoka Ghana Van Vicker leo amemsifia muigizaji wetu Wema kwamba anafanya vizuri kwenye kazi yake ya uigizaji, anajua anachokitaka and she is very passionate about what she want and she get it done......(nimeshindwa ku gaddem tafsiri hapo u know), movie hii ambayo Wema anacheza na Van Vicker inaitwa AFTER DEARTH, hii ni movie ya Van Vicker ambapo aliamua kumuita Wema Ghana ili akacheze nae kama kinara,
Wema hongera sana ninaamini baada ya movie hii utaanza kuitwa sana na ma producer wa huko nje ukacheze movie zao na jina lako litazidi kuwa kubwa, lakini ngoja niseme kaukweli hapo kidogo, unajua Wema anapogombanaga na Diamond huwa anakuwa serious na kazi na anapiga hatua , hii inaonyesha anakuwa kama anamuonyesha Diamond kwamba na mimi naweza kufanya jambo Fulani lakini inapotokea wamerudiana Wema anakuwa ameridhika anakuwa hana shida tena ya kumkomoa Diamond kwa kumuonyeshea maendeleo yake kwasababu wako pamoja na ameridhika, hii mentality inabidi aiache sasa, Diamond akurudie asikurudie wewe kuchapa kazi ni kitu cha lazima, kwasababu unapobweteka kisa upo na Diamond lazima Diamond achoke kwasababu hakuna mwanaume wa kisasa anayetaka demu asiye na malengo ya maisha, yani ye anasafiri akirudi anakukuta tu umekaa ndani hakuna kwenye maisha haya, kabla ya kurudiana na Diamond Wema alishaka hela nyingi tu za C, kwa hyo hakupaswa kabisa eti kusubiri Diamond ampe mtaji alitakiwa awe na hela zake afanye mambo yake Diamond akimpa iwe ni kama nyongeza tu kwasababu kwa hela alizokamata za C zilikuwa ni nyingi na zakumfanya awe stable financially na sio kumlalamikia Diamond hajampa mtaji, Diamond ni kijana mdogo kuhonga mamilioni hawezi kwanza anaipata hela yake kwa tabu hapumziki daily anasafiri kwenda kukata viuno stagini kwa hiyo kumtegemea aje amuhonge mtu mamillion its not possible hata ingekuwa mimi nisingeweza hela nizipate kwa tabu halafu nije nizihonge na sina uhakika kama zitazalisha,,,,
ANYWAY HAYO YAMESHAPITA TUNAMUOMBEA SWEETHEART WETU WA TANZANIA AFANIKIWE KWENYE KILA ANACHOKIFANYA NA MIMI NINAIMANI NAE SANA HUYU MSCHANA I DON KNOW WHY.....
No comments:
Post a Comment