Wednesday, December 10, 2014

HEMBU CHEKI UMAFIA ULIVYOFANYIKA NYUMBANI KWA MUIGIZAJI WEMA SEPETU....






                                                                       WEMA SEPETU



JAMAA wawili, mmoja fundi umeme, Rashid Balazi na Juma Bushiri wanadaiwa kunusurika kifo baada ya kutekwa na kusulubiwa nyumbani kwa msanii wa sinema za Kibongo, Wema  Sepetu  wakituhumiwa kukwapua simu ya bei mbaya ya mpambe wa mwanadada huyo, Petit Man, Amani limeichimba kwa kina



TUJIUNGE NA MANUSURA
Wakielezea mkasa huo wa kutisha uliojiri mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwa Wema, Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar, manusura hao walisema siku ya tukio waliitwa nyumbani kwa Wema na mdogo wake aitwaye Bite kwa ajili ya kutengeneza mota ya kusukuma maji.Walisema walifika nyumbani hapo na kuangalia mota hiyo ambapo waligundua kwamba haikuwa na tatizo bali mushkeli ilikuwa kwenye bomba la maji.
WAOMBA FEDHA YA MANUNUZI
Walisimulia kwamba, baada ya kugundua hilo waliomba fedha kwa Bite kwa ajili ya kwenda kununua bomba, wakapewa shilingi elfu arobaini.“Lakini kabla hatujafika kunakouzwa mabomba tulipigiwa simu na Bite kwamba tunatakiwa kurudi kwa kuwa kuna tatizo

Tulirudi na kumkuta Petit Man akiwa na mlinzi. Petit Man alisema eti sisi tumemuibia simu yake ya bei mbaya aina ya Iphone 6, hivyo tunatakiwa tuirudishe. “Tulimwambia hatukuchukua simu lakini akasisitiza ni sisi, akasema tutairudisha tutake tusitake.
“Tulipoona tumevaa msala wa uongo tulimwambia atupeleke polisi, akasema atawaita makamanda wake ambao ni ‘mbwa mwitu’ waje watuoneshe kazi. Lakini kabla ya kuwaita makamanda wake, alimwita mganga wa kienyeji. “Mganga alifika akaangalia kwa darubini zake akasema simu  hatujaiba sisi, lakini Petit Man hakutaka kumwelewa.
“Wakati huo alikuwa bado ametufungia ndani tusitoke, ghafla wakafika hao makamanda wake, hatukuwahesabu lakini walikuwa wengi, wakatuteka na kutufunga kabla ya kuanza kutusulubisha wakidai wao ni ‘mbwa mwitu’. Jamaa walitupiga kipigo cha mbwa mwizi....”
SILAHA ZATUMIKA



Walikuwa wakitumia silaha mbalimbali kama viwembe, visu na fimbo kisha baadaye walitumwagia maji ya moto. Kimsingi walitufanya kama vibaka wanavyofanyiwa wakikamatwa.
“Kama hiyo haitoshi, Petit Man aliwaita mabaunsa wawili ambao walitutesa  na kutuvua nguo tukabaki kama tulivyozaliwa.
PETIT MAN MBARONI
“Kipigo kilipozidi majirani walisikia kelele na kuja kuchungulia ambapo walikimbilia kwa mjumbe wa nyumba kumi na kumpa taarifa, yeye akaja kutuokoa na kutupeleka polisi huku wakati huo difenda la polisi nalo likawa limeshafika na kumtia mbaroni Petit Man na baadhi ya watesaji hao na kwenda kuwasweka mbaroni kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ lakini wengine walikimbia

WEMA ATOKA
“Wakati zogo hilo linaanza, Wema alitoka na kumwambia Petit wawahi uwanja wa ndege (Julius Nyerere, Dar) kwani walikuwa na safari (walikuwa wanakwenda nchini Ghana).
“Wema na Petit Man waliondoka na kuamuru kwamba tuwasubiri hapohapo tusiondoke.”
KIPIGO SAA 6:00 MCHANA HADI 9:00 ALASIRI
“Walipofika uwanja wa ndege wakawa wamechelewa ndege, Wema hakurudi nyumbani ila Petit Man alirudi  ndipo tukaanza kupigwa kuanzia saa 6:00 mchana hadi saa 9:00 alasiri,” walieleza jamaa hao wakiwa hoi kwa kipigo cha shetani.
MAJERAHA
Katika tukio hilo, Juma alipata majeraha kibao mwilini ambapo anatembea na mkongojo huku Rashid akiwa amechanwa na kisu mgongoni, mguuni na mbavu moja ikiwa imepata ufa na wote hao walipelekwa kwenye Hospitali ya Sinza-Palestina, Dar.Baadaye Rashid alihamishiwa Mwananyamala kufuatia hali yake kuwa mbaya
WEMA ATINGA KITUONI NAYE ATUPWA LUPANGO
Siku ya kwanza Petit Man alilala kituoni ambapo kesho yake Wema alitinga, naye akatupwa lupango kisha kuchukuliwa maelezo kabla ya baadaye wote kuachiwa ambapo Petit Man alitoka kwa dhamana.
Hata hivyo, washitakiwa hao na walalamikaji walitakiwa kuripoti kituoni hapo Jumatatu iliyopita lakini walalamikiwa walikiuka amri ya polisi, hawakuonekana kwa madai kwamba wamesafiri kikazi kwenda nchini Ghana.
SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI
Kwa mujibu ya shitaka lililofunguliwa kituoni hapo, Petit Man anakabiliwa na tuhuma za kudhuru mwili katika jalada la kesi namba KJN/RB/11250/2014 na KJN/RB/11220/2014 -SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI


 MFANYAKAZI WA WEMA PETIT MAN

Walalamikaji hao walieleza kwamba katika kupigwa huko, Juma aliibiwa simu mbili na fedha taslimu shilingi laki tatu na themanini huku Rashid akiibiwa shilingi laki tatu ambazo alipewa na mteja wake kwa ajili ya kwenda kununulia vifaa.
MJUMBE AKIRI
Naye mjumbe wa eneo la tukio, Muharami Seif alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kukiri kuwaokoa jamaa hao wakiwa katika hali mbaya baada ya kupata taarifa kutoka kwa majirani hivyo Petit Man na Wema wanasubiriwa watue Bongo kukabiliana na mkono wa sharia

No comments: