Friday, December 26, 2014

TANGAZO TANGAZO





                                     RACHEL KAYUNI TANZANITEMOVIES BLOGGER.


Wapenzi naimani mmekula Chrismass vizuri, nawatakieni heri ya mwaka mpya, nimekuwa kimya kwa muda sasa na wengi wamekuwa wakinitumia msg kuniuliza mbona sipost, ningependa kuwatangazia kwamba kuna mambo nataka niongeze kwenye blog yangu kuanzia tarehe moja, nataka nipanue wigo wa habari zangu ili muwe mnaoption nyingi ya habari, kwa hyo kuanzia tarehe moja hii itakuwa sio TANZANITEMOVIES peke yake kutakuwa na mambo mapya zaidi.....


                                 ASANTENI KWA KUTEMBELEA TANZANITEMOVIES BLOG/



Saturday, December 20, 2014

HII NI KALI KULIKO, MCHEKI DEMU WA MBUNGE M TWO SUGU ALIVYOVAA PAMPERS SIKU YA BIRTHDAY YAKE,,




Kituko! Katika hali ya kushangaza, msanii wa filamu Faiza Ally ambaye amezaa na Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, aligeuka kituko baada ya kuingia ukumbini akiwa amevalia mavazi wavaayo watoto kuhifadhi haja zao maarufu kama ‘pempasi’





Tukio hilo lilitokea juzikati katika Hotel ya Sea Cliff iliyopo Masaki jijini Dar, ambako walialikwa watu wachache kwa ajili ya kula chakula cha jioni pamoja.
Wakati wageni waalikwa wakiwa tayari ukumbini huku wakifikiria jinsi mwenyeji wao atakavyotinga hotelini hapo, ghafla walimuona Faiza akiingia ukumbini akiwa ndani ya mavazi hayo yaliyosindikizwa na kishati kidogo alichovaa juu na kuwafanya waalikwa wote kuangua kicheko



“Nimefikiria sana kwa nini nianze kujipa gharama za nguo na nilipomuangalia mwanangu Sasha anavaaga pempasi na mimi nikasema ngoja nifanye hivyo,” alisema Faiza





Faiza na Sugu waliodumu katika uhusiano kwa miaka mingi na kufanikiwa kupata mtoto mmoja, Septemba, mwaka huu walimwagana na sasa kila mmoja amechukua hamsini zake






FAIZA ALLY NI MUIGIZAJI PIA NDO MAANA NIMEPOST HABARI HII.

EMBU CHEKI MTIRIRIKO WA PICHA ZA DIAMOND NA ZARI SIKU YA PARTY YA ZARI AMBAYO ILIKUWA NI PARTY AMBAYO HAIJAWAHI KUTOKEA KWENYE HISTORIA YA PARTY ZA ZARI UGANDA...



1


2
3


4


5
6


1971478_819810648080987_2025137741_n
10864893_374359276063658_1036335938_n
7


8
9
10857958_10153006148796015_2596023406209527585_n
IMG-20141219-WA0000


IMG-20141219-WA0001
IMG-20141219-WA0008


IMG-20141219-WA0012


IMG-20141219-WA0013
IMG-20141219-WA0014


IMG-20141219-WA0016
Screenshot_2014-12-19-01-28-34


Screenshot_2014-12-19-01-28-48


Unaambiwa siku ya juzi Uganda nzima ilizizima .... watu walikuwa hawana kingine wanachowaza zaidi ya party ya Zari ambayo Rais wa jamuhuri ya muungano wa bongo flavour DIAMOND PLATNUMZ alikuwa mgeni rasmi, kwanza kabisa wengi walijua party hii itabuma kwasababu siku hiyo hiyo kulikuwa na party classic ya mwanamziki wa Uganda Jose Chamillione, kilichotokea Jose mwenyewe hakuamini, unaambiwa nyomi iliyojaa kwenye party ya Zari ilikuwa ni balaa yani ukikanyaga sehemu ukinyanyuua tu mguu mwenzako unakuta kashakanyaga basi utajiju kama utauning'iniza mguu hewani au utamkanyaga mwenzako mpigane, unaambiwa mamia ya watu walishindwa kuingia ndani kwasababu watu waliokuwepo ndani ya club walikuwa ni wengi mno mpaka wamiliki wa club wakafunga milango kwa hyo mamia ya watu wakabaki nje wanasikilizia kwa mbali mambo yanavyoendelea ndani, halafu sasa, hapo Diamond alikuwa amealikwa kwenda kama mgeni tu na sio kukata mauno , sasa ndo angealikwa kwenda kutoa burudani siuwanja wa mpira ndo ingebidi utumike ili watu watoshe, YANI ZARI NEXT TIME UKIMUITA RAIS DIAMOND KWENYE PARTY ZAKO HAKIKISHA UNAFANYIA UWANJA WA TAIFA HABARI YA KUFANYIA CLUB MWISHO KUTA ZA CLUB ZITAVUNJIKA KWA KUSHINDWA KUHIMILI KUEGAMIWA NA UWINGI WA WATU,unaambiwa toka club hiyo ijengwe haijawahi kujaza watu kama walivyojaa juzi,  basi sasa, Josee sialikuwa na yeye na party yake unaambiwa alifanya fastaer faster party yake iishe ili na yeye akale bata kwenye party ya Zari, na yeye huyo akatimba ndani ya nyumba, basi ikawa ni amani imetawala magwiji wawili wamekutana gwiji mkubwa na gwiji motto ilikuwa burudani sana, MADAM RITA PALSEN nae ndani ya nyumba mwanangu, yani kuna watu wazalendo jamani unaambiwa akaona ya nini kujibana hela ninayo kitakachonifanya nijifungie ndani kusubiri picha nini? akatimba bwana, JACKIE PEMBA NAE NDANI YA NYUMBA UNAAMBIWA ALIMWAGA MIHELA KAMA WALE MAPEDEJEE WA KI NIGERIA .... mimi pia ndani ya nyumba(natania)


BASI HAYO NDO YALIYOJIRI SIKU YA JUZI KWENYE ZARI ALL WHITE CIROC PARTY.



















Tuesday, December 16, 2014

MUIGIZAJI SHILOLE ADAI KWAMBA KUNA WATU WANATAKA KUMUUA....INGIA USOME







MSANII wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ambaye pia anafahamika kama Shishi Baby, amesema baadhi ya watu wana chuki naye kiasi kwamba wanatamani kumtoa roho kwa kutopenda mafanikio yake
Akipiga stori na gazeti hili mara baada ya ziara yake ya kimuziki barani Ulaya, Shishi Baby alisema katika mitandao ya kijamii, alizushiwa kuwa alienda huko akiwa na mwanaume badala ya ukweli kwamba alifuata shoo katika miji tofauti.
“Yaani watu wana roho mbaya sana, wanatamani nikiwa nimepanda ndege waitungue nife na ndiyo maana wanazusha, namuomba Mungu sana maana maadui wanazidi kila kukicha kisa maendeleo yangu tu,” alisema


JAMANI MNAMKUMBUKA MUIGIZAJI AISHA WA MAMBO HAYO? NA LILI PIA? INGIA UMUONE MTOTO MKUBWA WA MR CHUZ

HUYU NI AISHA WA ENZI ZILE ZA MAMBO HAYO, MPINZANI WAKE MKUU ALIKUWAGA WARIDI, JAMANI MBONA TUNATAMANI HAWA WATU WACHEZE HATA MOVIE YA PAMOJA MAANA TUMEWAMISS....hapo Aisha yuko na mwanae ambaye alikuwa amehitimu kidato cha nne. Aisha hajabadilika yani yuko vile vile hazeeki



Na huyu ni Lili, nae alikuwaga kwenye kikundi cha mambo hayo, na hapo yuko kwenye graduation ya mwanae akiwa nae amehitimu kidato cha nne, eti naskia huyu motto wa Lili kumbe alizaa na Mr Chuz,

KWA WALE WAZEE WENZANGU MNAMKUMBUKA VAN DAMME? MKALI WA MOVIE ZA KUPIGANA ENZI HIZO... EMBU MCHEKI MWANAE WA KIUME ANAYEFUATA NYAYO ZAKE ALIVYO HANDSOME..

HUYU NDIE MTOTO WA KWANZA WA VAN DAMME, KIJANA HUYU NAE NI MUIGIZAJI WA MOVIE ZA KUPIGANA. ANAITWA KRISTOPHER VAN VARENBERG.



Hapa Kristopher akiwa kwenye movie aliyocheza na baba yake inaitwa SIX BULET, humu ndani Kristopher alicheza kama FBI AGENT,kwa ambao bado hamjaiona hii movie itafuteni ni bonge la movie kuna action za maana humu ndani.


wanasema motto wa nyoka ni nyoka, hapo ni kwenye red carpet Kristopher akiwa na baba yake Van damme akimuonyesha action kidogo

hii ni familia nzima ya Van damme,hakokabinti kenye tshirt nyeupe ni motto wa pili wa Van dame ambaye nae pia yuko kwenye movie ya SIX BULLET, ye amecheza kama mschana anayewateka mabinti na kuwauza .

HAPA NAONA JAMAA YUKO KWENYE PROJECT KAMA ZA DIAMOND.





MANGE KIMAMBI AWACHARUKIA TEAM ZARI......





Mie naonaga mtu akiwa anamsemasema ex wake it means bado anampenda….. Maana if you are happy where you are  huwezi kuwa na muda na ex wako hata siku moja….. Alafu Zari nae ana roho ngumu mie ningemuuliza “wewe baba ni nini kila siku unamwongelea ex wako? embu tuishi maisha yetu
Hata mie kabla sija move on from baba Bhoke nilikuwaga nna hasira kama hizi, muda wote nataka mtukana au nimseme vibaya but nilivyokuwa happy na jamaa mwingine tu uwiii nikawa nae rafiki kabisa yani hasira ziliisha ghafla, na mpaka leo sina hata baya nalolikumbuka kuhusu yeye…. So its safe to say Diamond bado haja move on hata robo. Yani roho yote bado iko kwa Wema. Mtu una girlfriend wako kwanini bado una time ya kumrushia madongo ex wako???? Siku akiweza kumpotezea Wema completely ndo tutajua ka move on ila kwa haya madongo jamaa bado yupo deep in love……hahahaha
Hivi ni kwanini wanaume wasio na pesa ya ndefu huwa wanapenda lalamikia sana wanawake wasio tengeneza pesa zao wenyewe? jamani kama huna kiburi ya take care mwanamke si uachie wenye nazo?
Hata Biblia inasema Mwanamke atazaa kwa uchungu na mwanaume atakula kwa jasho lake….. Which means mie nakuzalia watoto wewe katoe jasho ulete chakula home tule ila siku hizi wanawake tuna fosiwaje kubeba zege kama madume???? mtukome bwana, kuzaa tuzae sie na kubeba zege tuwasaidie, EBOOOOO….Tufanye kazi kwa kupenda wenyewe sio kufosiwa wajameni


Kama huwezi kulea mwanamke piga kimya achia wenzio wanaoweza, malalamiko ya nini jamani???? Mitz mijinga kweli eti Zari hardworking woman  sababu ya maduka yake anayoweka instagram, sasa si alikuwa na mume mwenye hela ndefu hata Wema alivyopata mwanaume mwenye pesa za kuchezea alifungua bonge la ofisi na kampuni  na angekuwa na pesa zaidi labda angefungua hata burea d’ change,,,,Jamani ukiwa na mwanaume tajiri utaweza fungua chochote utakacho cha maana utavi maintain years later??? Sasa uko na mwanaume mtaji anakupa milioni 5 hivi unafungua kitu gani kwa mfano???? Saa nyingine tuwage tunafikiria? tunamsema sana mtoto wa watu wakati hatujui ya ndani…EMBU WOTE TUPIGE KIMYA JAMANI
Mnao linganisha success ya Wema na Zari ni wapuuzi kabisa, huyo Zari hata yeye alipewa kila kitu na mwanaume hakuvitolewa jasho, someni story ya maisha yake kwanza. Na mnachekesha mno huyo Zari ni mzee kama kina Mange hapa alafu mnalinganisha na kibinti hata hakijui kichefuchefu cha mimba tena 10yrs younger??? Hata Wema kabla hajafika age ya Zari labda atakuwa kapata mwanaume wa kumfungulia hiyo miduka na yeye tukumbuke kumsifia kuwa ni hardworking woman sio tuanze msema tena ooh kafunguliwa tu, mara kapewa tu
Yani watz wajinga jamani ukiona wanavyotukana watz wenzao kwenye page za foreigners huko instagram yani ni aibu , watz wote tunaonekana majinga matupu. Hivi mshaona waganda wanamfollow Diamond na kumwita shemeji sijui ujinga kwani??? kwanini nyie watz ndo mnapenda drama? Ndo maana watz sie umaskini hauwezi kutuisha na ndo maana ni maskini wamwisho duniani ni sababu ya ujinga, mtu siku nzima unaspend kutukana watu huwajui on instagram, wamebaki kutagiana, “shoga umepita huku”, “shoga njoo huku”, “shoga nyoko fyoko”, yani wako shameless, sasa hao wanatukana au kutagiana aembu omba bank statement zao, shingi 10 hawana…. bloody fool , in Linda award winning designer’s voice….lol


HAYO NDO MANENO YA MANGE KIMAMBI KWENDA KWA TEAM ZARI.....

Wednesday, December 10, 2014

KUMBE MANGE KIMAMBI ANAMILIKI KIJIJI MBWENI ........KWELI MASHAUZI YANATAKA PESA....

                      MANGE KIMAMBI AKIWA NA MWANAE WA MWISHO.
HII HAPO CHINI NI PICHA YA KIJIJI ANACHOMILIKI MANGE KIMAMBI.


Unaambiwa hiki kijiji kilichopo mbweni ambacho nakibatiza jina labda tukiite KIMAMBI VILLAGE, kilivamiwa na watu wakajenga nyumba zipatazo 40 na bado mueneo umebaki ...




kama mnavyoona hapo ni wale watu waliouziwa vi pisi vya viwanja hapo KIMAMBI VILLAGE wakiendelea kujenga lakini inasemekana wanatakiwa waondoke haraka .


STORY IKO HIVI...... blogger Mange Kimambi alinunuliwa kijiji hiki na marehemu baba yake, kijiji hiki kipo mbweni, kwanza huko mbweni sasa hivi viwanja ni bei mno kwa hiyo kwa mtu kama Mange anayemiliki kijiji badala ya kiwanja nadhani mnajua hapo thamani yake ikoje, sasa bwana kwa bahati mbaya mlinzi waliyemuweka awalindie alipoona baba yake Mange amefariki akaanza kuuzia watu baadhi ya maeneo kwenye kijiji hicho cha KIMAMBI, sasa mahakama imetoa order wabomoe walivyovijenga ili Mange na wadogo zake wawili waanze kukitumia kijiji chao,


YANI NIKIONA HIVI NASIKIA UCHUNGU KWA WALE WAZAZI AMBAO WANAFANIKIWA KUWA NA KIPATO KWENYE MAISHA LAKINI WANAENDEKEZA STAREHE NA VIMADA WANASAHAU KUWAACHIA WATOTO WAO VITEGA UCHUMI, MATOKEO YAKE NDO UNAKUTA WATOTO WANAKUWA WAKUBWA MISINGI MIZURI HAWANA MAISHA MAGUMU WANAISHIA KUWA WAUZA UNGA, KAMA WANAWAKE WANAISHIA KUWA MACHANGUDOA LAKINI UKIFATILIA UNAWEZA KUKUTA WAZAZI WAO WALIKUWA NJEMA TU ILA HAWAKUKUMBUKA KUWAWEKEA VITEGA UCHUMI WATOTO WAO, yani naandika hivi nikiwa na uchungu mno maana najua jinsi watu wanavyohangaika kwa makosa ya wazazi wao mitaani, LAKINI MAREHEMU MZEE KIMAMBI NAMSIFU KWA KUKUMBUKA KUWAACHIA WANAE VITEGA UCHUMI KWA KIJIIJI HICHO TU CHA MBWENI WANAE WANAUHAKIKA WA KUISHI VIZURI MPAKA UZEENI...


na sisi vijana tuige mifano, tunapoanzisha familia tukumbuke kuewekeza kwa ajili ya watoto wetu tunaowazaa ili wasije kuhangaika baadae, yale mambo ya toa mwili upate kazi hayatatokea kwa watoto wetu kama tumewaachia misingi mizuri, kila tunapofanikiwa tukumbuke kuweka akiba na tukumbuke kuwa na asset ili ziwanufaishe watoto wetu, tusikalie kununua magari, pochi na viatu, na kuwa busy kila siku kwenye starehe badala yake tuwe busy kununua vijiji kama alivyofanya mzee wake Mange.

HEMBU CHEKI UMAFIA ULIVYOFANYIKA NYUMBANI KWA MUIGIZAJI WEMA SEPETU....






                                                                       WEMA SEPETU



JAMAA wawili, mmoja fundi umeme, Rashid Balazi na Juma Bushiri wanadaiwa kunusurika kifo baada ya kutekwa na kusulubiwa nyumbani kwa msanii wa sinema za Kibongo, Wema  Sepetu  wakituhumiwa kukwapua simu ya bei mbaya ya mpambe wa mwanadada huyo, Petit Man, Amani limeichimba kwa kina



TUJIUNGE NA MANUSURA
Wakielezea mkasa huo wa kutisha uliojiri mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwa Wema, Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar, manusura hao walisema siku ya tukio waliitwa nyumbani kwa Wema na mdogo wake aitwaye Bite kwa ajili ya kutengeneza mota ya kusukuma maji.Walisema walifika nyumbani hapo na kuangalia mota hiyo ambapo waligundua kwamba haikuwa na tatizo bali mushkeli ilikuwa kwenye bomba la maji.
WAOMBA FEDHA YA MANUNUZI
Walisimulia kwamba, baada ya kugundua hilo waliomba fedha kwa Bite kwa ajili ya kwenda kununua bomba, wakapewa shilingi elfu arobaini.“Lakini kabla hatujafika kunakouzwa mabomba tulipigiwa simu na Bite kwamba tunatakiwa kurudi kwa kuwa kuna tatizo

Tulirudi na kumkuta Petit Man akiwa na mlinzi. Petit Man alisema eti sisi tumemuibia simu yake ya bei mbaya aina ya Iphone 6, hivyo tunatakiwa tuirudishe. “Tulimwambia hatukuchukua simu lakini akasisitiza ni sisi, akasema tutairudisha tutake tusitake.
“Tulipoona tumevaa msala wa uongo tulimwambia atupeleke polisi, akasema atawaita makamanda wake ambao ni ‘mbwa mwitu’ waje watuoneshe kazi. Lakini kabla ya kuwaita makamanda wake, alimwita mganga wa kienyeji. “Mganga alifika akaangalia kwa darubini zake akasema simu  hatujaiba sisi, lakini Petit Man hakutaka kumwelewa.
“Wakati huo alikuwa bado ametufungia ndani tusitoke, ghafla wakafika hao makamanda wake, hatukuwahesabu lakini walikuwa wengi, wakatuteka na kutufunga kabla ya kuanza kutusulubisha wakidai wao ni ‘mbwa mwitu’. Jamaa walitupiga kipigo cha mbwa mwizi....”
SILAHA ZATUMIKA



Walikuwa wakitumia silaha mbalimbali kama viwembe, visu na fimbo kisha baadaye walitumwagia maji ya moto. Kimsingi walitufanya kama vibaka wanavyofanyiwa wakikamatwa.
“Kama hiyo haitoshi, Petit Man aliwaita mabaunsa wawili ambao walitutesa  na kutuvua nguo tukabaki kama tulivyozaliwa.
PETIT MAN MBARONI
“Kipigo kilipozidi majirani walisikia kelele na kuja kuchungulia ambapo walikimbilia kwa mjumbe wa nyumba kumi na kumpa taarifa, yeye akaja kutuokoa na kutupeleka polisi huku wakati huo difenda la polisi nalo likawa limeshafika na kumtia mbaroni Petit Man na baadhi ya watesaji hao na kwenda kuwasweka mbaroni kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ lakini wengine walikimbia

WEMA ATOKA
“Wakati zogo hilo linaanza, Wema alitoka na kumwambia Petit wawahi uwanja wa ndege (Julius Nyerere, Dar) kwani walikuwa na safari (walikuwa wanakwenda nchini Ghana).
“Wema na Petit Man waliondoka na kuamuru kwamba tuwasubiri hapohapo tusiondoke.”
KIPIGO SAA 6:00 MCHANA HADI 9:00 ALASIRI
“Walipofika uwanja wa ndege wakawa wamechelewa ndege, Wema hakurudi nyumbani ila Petit Man alirudi  ndipo tukaanza kupigwa kuanzia saa 6:00 mchana hadi saa 9:00 alasiri,” walieleza jamaa hao wakiwa hoi kwa kipigo cha shetani.
MAJERAHA
Katika tukio hilo, Juma alipata majeraha kibao mwilini ambapo anatembea na mkongojo huku Rashid akiwa amechanwa na kisu mgongoni, mguuni na mbavu moja ikiwa imepata ufa na wote hao walipelekwa kwenye Hospitali ya Sinza-Palestina, Dar.Baadaye Rashid alihamishiwa Mwananyamala kufuatia hali yake kuwa mbaya
WEMA ATINGA KITUONI NAYE ATUPWA LUPANGO
Siku ya kwanza Petit Man alilala kituoni ambapo kesho yake Wema alitinga, naye akatupwa lupango kisha kuchukuliwa maelezo kabla ya baadaye wote kuachiwa ambapo Petit Man alitoka kwa dhamana.
Hata hivyo, washitakiwa hao na walalamikaji walitakiwa kuripoti kituoni hapo Jumatatu iliyopita lakini walalamikiwa walikiuka amri ya polisi, hawakuonekana kwa madai kwamba wamesafiri kikazi kwenda nchini Ghana.
SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI
Kwa mujibu ya shitaka lililofunguliwa kituoni hapo, Petit Man anakabiliwa na tuhuma za kudhuru mwili katika jalada la kesi namba KJN/RB/11250/2014 na KJN/RB/11220/2014 -SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI


 MFANYAKAZI WA WEMA PETIT MAN

Walalamikaji hao walieleza kwamba katika kupigwa huko, Juma aliibiwa simu mbili na fedha taslimu shilingi laki tatu na themanini huku Rashid akiibiwa shilingi laki tatu ambazo alipewa na mteja wake kwa ajili ya kwenda kununulia vifaa.
MJUMBE AKIRI
Naye mjumbe wa eneo la tukio, Muharami Seif alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kukiri kuwaokoa jamaa hao wakiwa katika hali mbaya baada ya kupata taarifa kutoka kwa majirani hivyo Petit Man na Wema wanasubiriwa watue Bongo kukabiliana na mkono wa sharia

VAN VICKER WA GHANA ASIFIA KIPAJI CHA MUIGIZAJI WEMA SEPETU

                                    VAN VICKER NA WEMA SEPETU
Muigizaji kutoka Ghana Van Vicker leo amemsifia muigizaji wetu Wema kwamba anafanya vizuri kwenye kazi yake ya uigizaji, anajua anachokitaka and she is very passionate about what she want and she get it done......(nimeshindwa ku gaddem tafsiri hapo u know), movie hii ambayo Wema anacheza na Van Vicker inaitwa AFTER DEARTH, hii ni movie ya Van Vicker ambapo aliamua kumuita Wema Ghana ili akacheze nae kama kinara,


Wema hongera sana ninaamini baada ya movie hii utaanza kuitwa sana na ma producer wa huko nje ukacheze movie zao na jina lako litazidi kuwa kubwa, lakini ngoja niseme kaukweli hapo kidogo, unajua Wema anapogombanaga na Diamond huwa anakuwa serious na kazi na anapiga hatua , hii inaonyesha anakuwa kama anamuonyesha Diamond kwamba na mimi naweza kufanya jambo Fulani lakini inapotokea wamerudiana Wema anakuwa ameridhika anakuwa hana shida tena ya kumkomoa Diamond kwa kumuonyeshea maendeleo yake kwasababu wako pamoja na ameridhika, hii mentality inabidi aiache sasa, Diamond akurudie asikurudie wewe kuchapa kazi ni kitu cha lazima, kwasababu unapobweteka kisa upo na Diamond lazima Diamond achoke kwasababu hakuna mwanaume wa kisasa anayetaka demu asiye na malengo ya maisha, yani ye anasafiri akirudi anakukuta tu umekaa ndani hakuna kwenye maisha haya,  kabla ya kurudiana na Diamond Wema alishaka hela nyingi tu za C,  kwa hyo hakupaswa kabisa eti kusubiri Diamond ampe mtaji alitakiwa awe na hela zake afanye mambo yake Diamond akimpa iwe ni kama nyongeza tu kwasababu kwa hela alizokamata za C zilikuwa ni nyingi na zakumfanya awe stable financially na sio kumlalamikia Diamond hajampa mtaji, Diamond ni kijana mdogo kuhonga mamilioni hawezi kwanza anaipata hela yake kwa tabu hapumziki daily anasafiri kwenda kukata viuno stagini kwa hiyo kumtegemea aje amuhonge mtu mamillion its not possible hata ingekuwa mimi nisingeweza hela nizipate kwa tabu halafu nije nizihonge na sina uhakika kama zitazalisha,,,,
 ANYWAY  HAYO YAMESHAPITA TUNAMUOMBEA SWEETHEART WETU WA TANZANIA AFANIKIWE KWENYE KILA ANACHOKIFANYA NA MIMI NINAIMANI NAE SANA HUYU MSCHANA I DON KNOW WHY..... 

MUIGIZAJI MTUNIS ATOKA NAMNA HII




Filamu mpya ya Mtunis, mimi huyu kaka kwakweli huwa nazipenda sana story zake, huwa anastory za kitofauti zinazofundisha na zinazofurahisha.

JACKLINE WOLPER AFANYA JAMBO LA TOFAUTI .........






STAA Jacqueline Wolper Massawe, ambaye ni muigizaji mahiri wa filamu, amewapiku nyota wenzake wa tasnia hiyo baada ya kufanya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa Jumamosi iliyopita kwa namna tofauti kabisa, kwani badala ya kuita marafiki kwenye pati kubwa inayoambatana na vyakula na vinywaji, yeye alikwenda kuwatembelea wazee wanaolelewa katika Kanisa Katoliki la Msimbazi, jijini Dar
Katika kituo hicho kinachowalea wazee wa kike na kiume, Wolper aliyeambatana na rafiki yake Kajala Masanja na wale aliowatambulisha kama Wolper Family, muigizaji huyo alitoa zawadi ya mchele mifuko miwili ya kilo 50 kila moja, sukari mifuko miwili ya kilo 50, sembe kilo 50 pia, sambamba na mafuta ya kupikia madumu mawili, vitu ambavyo alikataa kutaja thamani yake
Siku hizi nimekuwa mtu mzima, nimeachana na mambo ya sherehe kwa sababu nimeona ninakuwa napoteza pesa kwa mambo yasiyo ya muhimu, ni jambo la heri kwangu kuwasaidia wazee kwani nawapenda na naamini hata wao wanatupa sapoti kubwa sana kwenye kazi zetu, japo kuna watu walitarajia waone nini kitafanyika kwenye siku yangu hii ya kuzaliwa kuhusu sherehe,”alisema Wolper




Marafiki zake kutoka Wolper Family walisema ni wao ndiyo waliomshauri staa huyo kufanya kitu hicho ili kuwa tofauti na wenzake ambao kumbukumbu ya kuzaliwa kwao hufanywa kwa matumizi makubwa ya fedha yasiyo ya lazima
Alitaka kufanya sherehe tukamshauri aachane na hilo suala tuliona atapoteza pesa kwa sababu angefanya sherehe watu wangekunywa pombe, wangevaa vinguo vya ajabu, kitu ambacho ni kama laana kwake, badala yake kwa hili alilolifanya atapata baraka na mambo yake yatamnyookea,” alisema mmoja wa mashabiki wake kutoka Wolper Family.
Baada ya kukabidhi msaada wa vyakula hivyo, mmoja wa wazee hao Bibi Rachel Christopher, alimpa somo Wolper kuwa ni vema wakaishi vizuri na mashabiki wao na kuachana na mavazi ya ajabu kwani yanawashushia hadhi zao

Mimi huwa naangalia sana filamu zao, ninawapenda na huyu leo katimiza miaka kadhaa tangu kuzaliwa kwake, tunamuombea uzima, afya tele na maisha marefu,” alisema bibi huyo ambaye pia aliwataka waigizaji wa kiume na wasanii kuacha kuvaa suruali kwa mtindo wa kata K