Thursday, February 13, 2014

MAPENZI YA WEMA NA DIAMOND KUELEKEA VILENTINE'S DAY










Wengi tunawajua watu hawa kwamba ndio mastar wanaowika sana Tanzania, mwanaume ni mwanamziki mkubwa anayeitwa Diamond na mwanamke ni muigizaji mkubwa anayeitwa Wema Sepetu, wawwili hawa wamekua wamenzi ambao mara nyingine wanaachana na kurudiana, wengi wa mashabiki wao wamekua wakipenda kuwaona watu hawa wakiwa pamoja, Wema alianza mahusiano na Diamond toka kipindi Diamond hana kitu, kipindi hiko Diamond alikua na nyimbo mbili ndo zimeanza kusikika na Wema alikua star tayari na pia alikua ndo kamaliza kipindi chake cha u miss Tanzania, baada ya Diamond kuwika na hela kuongezeka waschana wengi wakaanza kumuona na kumtamani na baadae mapenzi yake na wema yakayumba na hatimae kuachana. kila mmoja akaendelea na maisha yake na mpenzi mpya, lakini hivi sasa wawili hawa wamerudiana tena kwa nguvu zote, Diamond kawaacha wale warembo wote waliokua nae kisa umaarufu na pesa kamfwata mschana aliyempenda toka hana kitu na Wema kamuacha mpenzi wake aliyekua na pesa nyingi na kumrudia Diamond aliyemvumilia tangu akiwa hana kitu. japo hawa wote wanamapungufu yao lakini hapa wanatufundisha kwamba mapenzi si pesa wala urembo, kama ni pesa basi Wema angebaki na pedejee lake na kama ni urembo basi Diamond angebaki na Jokate, mwisho wa siku ni kwamba mapenzi ni kua na yule mtu ambaye ukiwa nae moyo wako ndo unakua na amani, yule mtu ambae unajua kakupenda UNCONDIONALY, siku hizi ni kazi sana kukutana na mtu mwaminifu lakini kwa msaada wa Mungu yote yanawezekana




                          SKUKUU NJEMA YA WAPENDAO HAPO KESHO.







No comments: