Thursday, February 27, 2014

JOKATE MWEGELO AKITIRIRIKA JUU YA KUMUOMBA MSAMAHA WEMA. KWA AMBAO HAMKUONA






Wote tulikua tunajua kuna BEEEEEF kati ya waigizaji ambao zamani walikua mamis WEMA SEPETU na JOKATE MWEGELO, Jokate alimuibia Wema mpenzi, wakagombana wee, magazeti nayo yakauza wee, hivi sasa mambo tambarare kabisa, kama mnavyomjua Wema hanaga kinyongo, ukimuomba msamaha huwa anasamehe na kusahau,

WEMA SEPETU, MANGE KIMAMBI, OMOTOLA JELADE NA MIRIAM ODEMBA. HEBU JIKUMBUSHENI HILI TUKIO KIDOGO






kipindi hicho kama sikosei mwaka jana, Wema Sepetu  akiwa kajipanga vizuri kwenye kazi zake, alimleta msanii wa movie wa Nigeria OMOTOLA JELADE IKINDE ili azindue movie yake iliyokua inaitwa SUPER STAR, mpaka leo movie hyo haijatua mikononi mwa wananchi na wanachi wameisubiri mpaka wameisahau. WENGI WAMEKUA WAKITOA MAONI NA KUMTAKA MREMBO HUYU KUANZA KUZIACHIA MOVIE ZAKE KWANI NI KIPINDI KIREFU HAJAONEKANA KWENYE MOVIE

Tuesday, February 25, 2014

JACKLINE WOLPER ACHACHAMALIWA BALAAA






Uwiii yani watu wamemchachamali Jackilne Wolper ambaye ni msanii wa maigizo nchini. Wolper alitundika picha zikimuonyesha anafanyiwa massage, na kuelezea kwamba kaenjoy sana, watu wacha wachachamae, watu wakaanza kucomment kwamba Wolper mbona mshamba, yani kitu kama massage tu ndo unaanika ili kila mtu ajue, wengine wakaanza kusema ni ulimbukeni, wengine wakaanza kusema anataka tu magazeti yamuandike maana kaona hajaandikwa siku nyingi, anyway, WEWE UNAONAJE?

RAIS AKUMBWA NA KASHFA NZITO....( NI RAIS WA SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIA.)


                                                                  BATULI



                                      MWAKIFAMBA


Eti inasemekana kwamba rais wa shirikisho la filamu Tanzania Simon Mwakifamba anamahusiano na muigizaji wa kike ambaye si mkali sana kwenye sanaa japo ni mzuri sana kimuonekano anayeitwa Batuli, Kashfa hiyo imekuja baada ya Mwakifamba kumteua Batuli kwenda nae Dodoma bungeni kwani wasanii walialikwa huko kwenye bunge la katiba na Mwakifamba akiwa kama rais wa shirikisho akaacha kuwachagua wakina Tea, Monalisa, akamuchagua Batuli msanii mchanga kabisa.


                         NI KWA MUJIBU WA GAZETI MOJA HIVI.

MUIGIZAJI LULU NA STEVE NYERERE KASHFA NZITO





PICHA: Tazama picha za waigizaji Lulu Michael na Steven Nyerere walipokuwa kwenye kipindi cha mboni show.
huyo mwenye miwani na suruali nyeusi ndio STEVE NYERERE


eti inasemekana kwamba muigizaji LULU na STEVE NYERERE wanaukaribu sana, chanzo kikiwa ni kwamba, eti Steve  ni kuwadi wa Lulu, eti ndie anayemuunganisha Lulu kwa mabwana.




SI MANENO YANGU NI YA GAZETI TU.

JACKLINE WOLPER ANAHIFADHI NGUO HUMU





huyu ni muigizaji wa Bongo movies anaitwa JACKLINE WOLPER, na hicho ndo chumba chake anachohifadhia nguo.

Friday, February 21, 2014

ALIYEMBAKAGA SHILOLE HUYU HAPA


Kama Shilole ambaye ni msanii wa movie na mziki alivyotoaga historia yake kwamba alibakwa akiwa na umri mdogo na kupata ujauzito na aliyembaka akamuoa kutokana na ugumu wa maisha ilibidi akubali kuolewa nae, inasemekana huyo anayeonekana kwenye picha akiwa na Shilole ndio muhusika.


GENNEVIEVE NNAJI, WEMA SEPETU NA OMOTOLA JELADE NGOMA DROO

GENEVIEVE NNAJI

OMOTOLA JELADE

OMOTOLA JELADE

WEMA SEPETU

                                                           WEMA SEPETU




Omotola na Genevieve ni wasanii wakubwa sana Nigeria, wasanii hao walianza kazi ya kuigiza kwa pamoja na mpaka sasa ni vinara huku wenzao wakifwata kwa nyuma, Wema ni msanii wa movie za Tanzania ambaye alianzia kwenye u miss na baadae kuingia kwenye sanaa ya maigizo na yeye hivi sasa ndie msanii aliye juu kuliko msanii yeyote wa kike, wasanii hao kutokana na ukubwa wa hadhi zao hivi sasa wamekua wakiwacharge ma producer wa movie hela nyingi ikiwa ni malipo yao ya kucheza movie, kutokana na hali hiyo ma producer wamekua wanapata wakati mgumu kuwachezesha kutokana na kua na budget ndogo, sasa kutokana na hilo wasanii hawa wameamua ni bora kutokucheza movie kuliko kucheza movie na kulipwa malipo yasiendana na hadhi yao, inasemekana Genevieve na Omotola mara ya mwisho kurecord movie ni kama miaka miwili iliyopita na Wema hajaonekana kwenye movie siku nyingi na akionekana basi ujue yeye ndo kaiproduce, ni hayo tu

Wednesday, February 19, 2014

IRINE UWOYA ASHAURIWA HIVI




Kutokana na muigizaji aliyejipatia sifa nyingi nchini IRINE UWOYA kupotea kwenye sanaa ya maigizo na kujikita kwenye utangazaji kumewafanya mashabiki wake wamkumbuke na wengi kutoa maoni ya kwamba binti huyu atapoteza kipaji chake, wengi wamemtaka kuendana na hali ya maisha inavyokwenda kwani hivi sasa ni kawaida kumuona msanii wa maigizo akifanya kazi zaidi ya mbili, Irine alitakiwa kufanya kazi zote na sio kufanya moja ya utangazaji na kusahau uigizaji, NI HAYO TUUUU.



Tuesday, February 18, 2014

INI EDO WA NIGERIA AWA MPYA

huyu ni msanii wa maigizo Nigeria anaitwa INI EDO ni hii picha hapa chini yuko na mume wake





hii picha ya hapa chini ndio INI EDO anavyoonekana baada ya kufanya diet ya nguvu.


Sunday, February 16, 2014

WASCHANA BONGO MOVIE WAPEWA MAKAVU LIVE.




Waschana wa Bongo movie wameshauriwa kufwata nyao za mwanadada mkenya anayetikisa Hollywood anayeitwa LUPITA NYONG'O, kwanza kabisa wameshauriwa kutokukata tama na kazi zao kwa kuhisi labda hawatafika mbali na pia kutokata tama na kipato chao mpaka kufikia hatua ya kuanza maisha ya kujiuza na hatimae kukumbwa na skendo mbalimbali magazetini, Lupita ni mschana kama wao, anajiheshimu na amefika mbali tena kwenye nchini kubwa kama Marekani, wanatakiwa pia kutokujiaribu mionekano yao kwa kujichubua na kunenepeana hovyo kwa kujishindilia mi bia na minyama kwani muonekano pia ni chachu ya wao kufika mbali, moja ya vitu vinavyowavutia wengi kuhusu muigizaji huyu Lupita ni muonekano wake wa asili, hizo hapo juu ndo picha za LUPITA NYONG'O.

NA HAWA HAPA CHINI NDO WASANII WETU WA BONGO MOVIE



Saturday, February 15, 2014

WASTARA ANYWA SUMU?








kwa mujibu wa gazeti inasemekana Wastara ambaye ni muigizaji alikunywa sumu kutokana na matatizo mengi kumuandama, anyway wengine huwa hatuamini sana kinachooandikwa magazetini ila tunamuombea huyu dada kwasababu kapitia mengi kwenye maisha

Friday, February 14, 2014

SAA YA DIAMOND KWA TONTO DIKEH

Click for Full Image Size


Hii ndio saa ya Diamond aliyopewa msanii wa maigizo wa Nigeria Tonto Dikeh kama zawadi ya Valentine na mpenzi wake.

AGNESS MASOGANGE, KAJALA NA WEMA SEPETU NANI ZAIDI ?



Wema Sepetu na Kajala Masanja ni wasanii walioumbika kiAfrica hasa, sasa leo nataka tuangalie nani kaumbika kati ya Wema, Kajala na mschana anayesifikaga kwa wowowo Agnes Masogange.





Pembeni ni WEMA SEPETU na pembeni kwingine ni KAJALA MASANJA



Huyu hapa chini ni AGNESS MASOGANGE, au kama anavyojiitaga FINE A....... GIRL.











haya wakati huko kwa wenzetu wanatumia mapesa mengi kua hivi, hawa wameumbwa hivi toka kuzaliwa kwao no fake a, yani hawa wakitua Hollywood, Kim Kardashian na J lo lazima wakimbie.

Thursday, February 13, 2014

MAPENZI YA WEMA NA DIAMOND KUELEKEA VILENTINE'S DAY










Wengi tunawajua watu hawa kwamba ndio mastar wanaowika sana Tanzania, mwanaume ni mwanamziki mkubwa anayeitwa Diamond na mwanamke ni muigizaji mkubwa anayeitwa Wema Sepetu, wawwili hawa wamekua wamenzi ambao mara nyingine wanaachana na kurudiana, wengi wa mashabiki wao wamekua wakipenda kuwaona watu hawa wakiwa pamoja, Wema alianza mahusiano na Diamond toka kipindi Diamond hana kitu, kipindi hiko Diamond alikua na nyimbo mbili ndo zimeanza kusikika na Wema alikua star tayari na pia alikua ndo kamaliza kipindi chake cha u miss Tanzania, baada ya Diamond kuwika na hela kuongezeka waschana wengi wakaanza kumuona na kumtamani na baadae mapenzi yake na wema yakayumba na hatimae kuachana. kila mmoja akaendelea na maisha yake na mpenzi mpya, lakini hivi sasa wawili hawa wamerudiana tena kwa nguvu zote, Diamond kawaacha wale warembo wote waliokua nae kisa umaarufu na pesa kamfwata mschana aliyempenda toka hana kitu na Wema kamuacha mpenzi wake aliyekua na pesa nyingi na kumrudia Diamond aliyemvumilia tangu akiwa hana kitu. japo hawa wote wanamapungufu yao lakini hapa wanatufundisha kwamba mapenzi si pesa wala urembo, kama ni pesa basi Wema angebaki na pedejee lake na kama ni urembo basi Diamond angebaki na Jokate, mwisho wa siku ni kwamba mapenzi ni kua na yule mtu ambaye ukiwa nae moyo wako ndo unakua na amani, yule mtu ambae unajua kakupenda UNCONDIONALY, siku hizi ni kazi sana kukutana na mtu mwaminifu lakini kwa msaada wa Mungu yote yanawezekana




                          SKUKUU NJEMA YA WAPENDAO HAPO KESHO.







Wednesday, February 12, 2014

MENGI NA FAMILIA YAKE




Najua hawausiani na mambo ya movie lakini nimeona ni share na nyie hii picha maana imeninoga sana.

Monday, February 10, 2014

BEYONCE NA JAY ZEE WA AFRICA




Hawa ni waigizaji ambao mapenzi yao yamekua mvuto kwa watu wengi na wengi wamekua wakiyafananisha na ya Beyoncé na Jay, huyu kaka anaitwa Jim Iyke ni muigizaji wa Nigeria na dada anaitwa Nadia buari ni muigizaji wa Ghana.

Friday, February 7, 2014

KWA WALIOKOSA SHOW YA WEMA SEPETU HII HAPA, CHUKUA POP CON NA PEPS TAZAMA


INI EDO MUIGIZAJI WA NIGERIA AMWAGIWA TINDI KALI







Ni tindikali ya kwenye movie, yani alikua anaigiza kama binti aliyemwagiwa tindi kali, na hapo ni make up artist kamtengeneza mpaka inaonekana kama ni kweli ni mtu aliyeathirika na tindikali, 

WASANII WA MOVIE NAIGERIA NI NOMARRR.


kushoto hapo ni KETY HENSHAW, RITA DOMINIC, STEPHANIE OKEREKE na OMOTOLA JELADE,






Wasanii wa movie wa Nigeria hasa wa kike sasa hivi wanajitambua mchango wao ni wakina nani kwenye jamii na wamekua wakiheshimika na makampuni na mashabiki wao pia, ni jambo la kawaida hivi sasa kwa wasanii hawa kusaini mikataba minono ya hela kwa kua mabalozi wa makampuni mbalimbali, wamefikaje hapo, kwanza kwa kua na heshima na kazi zao na kuishi maisha yanayoeleweka, mavazi na shule pia,  kwa hapa kwetu msanii ambao tunaweza kuthubutu kusema alijitahidi ni KANUMBA tu.

Wednesday, February 5, 2014

SINTAH MATATA SANA










I love this woman, hana makuu, kwa wasiomjua unaweza kujua kwamba anajishaua kutokana na picha anazopiga na maneno anayoyaweka kwenye blog, lakini when u get the chance to meet her in person, she is so different, she is very kind and open, sio mchoyo wa maendeleo,  yani huyu mtu unaweza ukamuona leo na leo hiyo hiyo mkawa mtu na dada yake.  yani sina maneno mengi ya kumuelezea. hizi picha sura yake iko kama alivyozaliwa, yani kitu bila make up.