RACHEL KAYUNI TANZANITEMOVIES BLOGGER
Okayyyy. mimi ni mpenzi sana wa kupika pika na Mungu amenijalia mama aliyenifundisha kupika mapishi mengi mno sio tu ya kibongo bali na ya nje pia. .
STRUDEL
hii inaitwa strudel, ni kitafunwa kizuri mno , unaweza ukala na chai, ukala na juice au soda au pia unaweza ukala hivi hivi tena kinawafaa wale wanaopenda kula kula, maana ukikipika unakikatakata unakiweka zako kwenye kikontena unahifadhi kwenye frige hata mwezi kinakaa, we ukipita ndani mwako huna shobo na mtu kila saa unatafunatafuna , mgeni akija uimkariisha soda au juice basi kwenye kisaani unamuwekea tuvipande twake, motto akienda shule nae unampakia tuvipande twake na ka juice kake, we mwenyewe ukienda kazini kama kawa unajipakia zako kazini muda wa chai unajisonsomola sio kila siku unywe chai na mimaandazi na michapati meno yanachoka shuti uyape meno nafasi ya kuexperience vitu vipya. basi hii strudel ni nzuri na tamu maana ina jam pia juu yake.
PIZZA YA SOUSAGE
mimi ni mpenzi mno wa Pizza, ila huwa siendi kununua kwenye restaurant maana wanabania malighafi nyingi mara wabanie nyanya mara wabanie cheese basi mi hizo kero sizitaki, mi nataka nikila pizzabasi iwe pizza kweli, kwa hiyo namshukuru Mungu kanipa ujuzi wa kuipika basi huwa najipikia mwenyewe nyumbani na nitam kuliko zile ziazouzwa huko kwigine kwasababu mi sipiki kibiashara kwa hyo sina haja ya kubania kitu najiweka cheese nyingi mwenyewe basi pizza inakuwa mwake, asikudanganye mtu PIZZA NI CHEESE BILA CHEESE BASI HIYO SIO PIZZA HUO NI MKATE sasa ndo maana nikiona pizza inauzwa halafu imewekwa cheese kidogo sili ni bora nile mkate ieleweke moja kuliko kula mfano wa pizza.
RACHEL TANZANITEMOVIES BLOGGER NIKIWA JIKONI NIMESHAMALIZA KUPIKA
OKAY, NAJUA WENGI WENU MTAKUWA MMEVUTIA NA HAYO MAPISHI YANGU, MAANA KWANZA SIO MAPISHI TUNAYOPIKA SIKU ZOTE KWENYE NYUMBA ZETU ZA KITANZANIA, SASA KAMA UNATAKA NIJE KUKUFUNDISHA KUPIKA KITU CHA TOFAUTI NYUMBANI KWAKO BASI NIPIGIE SIMU 0713 608524, NTAKWAMBIA BEI YANGU YA KUKUFUNDISHA KUPIKA CHOCHOTE KILE CHA KITOFAUTI KASORO MAPISHI YA KIHINDI NA KIARABU TU NDO SIYAJUI NA YA KICHINA, LAKINI ULAYA HUKO HAINA TABU KABISA, NTAKWAMBIA BEI ZANGU NA NTAKUFUNDISHA, NITAKUCHARGE KWASABABU NIKIKUFUNDISHA NAJUA TAYARI NTAKUPA UJUZI WA MILELE NA WEWE UTAFUNDISHA MPAKA WAJUKUU ZAKO, KWA HYO USIONE UBAILI KUTOA HELA KIDOGO YA KUFUNDISHWA PISHIAMBALO UKIFNDISHWA MARA MOJA HUTALISAHAU MILELE, AU KAMAHUPENDI KUPIKA UNAWEZA KUNIAMBIA NIKAKUPIKIA MWENYEWE THEN NIKAKULETEA NYUMBANI KWAKO VYOTE NA FANYA NI WEWE TU NAMFUKO WAKO. USIONE UBAILI KWENYE MAPISHI HASA WANAWAKE KUMBUKENI MUME SIKU ZOTE HUPENDA KUPIKIWA VIZURI NA VITU TOFAUTI SIO KILA SIKU UGALI NA WALI TU. NIPIGIE SIMU NIKUFUNDISHE ,
No comments:
Post a Comment