Sunday, March 2, 2014

LUPITA NYONG'O NA BEEF ZITO




Muigizaji wa Hollywood mwenye asili ya Kenya Lupita Nyong'o ameingia kwenye mgogoro mzito na mwanamziki wa Nigeria mwenye asili ya Cameroon anayeitwa Dancia, mwanamziki huyo anayeongoza kwa kujichubua Africa, hivi sasa ana cream yake kwa ajili ya kujichubua yani bleeching cream ambayo anaiuza na inanunulika sana kutokana na ile dhana potofu ya wa Africa kwamba weupe ndo uzuri. sasa bwana, lupita alikua akitoa speech huko Marekani alikoshinda tuzo ya movie na aliamua kutoa barua aliyoandikiwa na fan wake akimsifu kwa jinsi alivyompa motisha kwasababu na yeye ni mweusi kama yeye na alikua anataka kwenda kununua dancia bleeching cream ili ajichubue lakini alivyoona mschana kama Lupita ni mweusi mwenzake tena mzuri na kapata mafanikio makubwa amefarijika sana na sasa yuko proud na ngozi yake.




basi mgogoro huo umeibua vita na huyo mschana hapo juu ambaye ndio dancia mwenyewe, picha ya pembeni ndo alivyokuwaga na weusi wake na hiyo nyinine baada ya kujichubua, dancia kaanza kutweet mambo kibao ya kumkashifu Lupita kwamba anaharibu biashara yake, eti kwanza ye hamjui Lupita ni nani kitu ambacho ni uongo, basi mgogoro huo umemfanya mschana huyu bingwa wa kujichubua kuonekana mjinga hasa ikizingatiwa anagombana na mschana anayejiamini na ngozi yake sio yeye aliyejibadilisha na kua kama mzungu.

No comments: