Sunday, March 16, 2014

DIAMOND AMZABA KIBAO WEMA SEPETU. PATA MKANDA WOTE HUMU......

huyu binti ni muigizaji Wema Sepetu, na kijana hapo ni mpenzi wake mwanamziki Diamond.

kama mnavyojua tena watu hawa ndo wasanii pekee Tanzania wanauza na attention yote iko kwao. walianza mapenzi miaka mine iliyopita lakini ndani ya miaka mine kumekua na kuachana na kurudiana na wakati mwingine kila mtu kua na mpenzi mwingine, mashabiki wengi wanaipenda hii couple,   sasa bwana kwasababu Diamond hivi sasa yuko mbali kimziki mabinti nao hawako nyuma kumganda ila mwisho wa siku Wema ndo moyo wake, nataka nikupashe tu yaliyotokea siku mbili hizi na kufanya mji uzizimE.


                                DIAMOND NA VICTORIA KIMANI

Sasa bwana, hivi majuzi juzi Diamond alienda kurecord wimbo uliowashirikisha wasanii 20 wa Africa, na huko kukawa kuna mambo ya photo shoot kama hivi unavyoona hii picha walipiga wakiwa South na pia kukawa kuna mambo ya kufahamiana na kuombana mambo ya corabolation, baada ya kazi kuisha basi tukasikia kuna wimbo utafanywa na Diamond, Ommy dimpoz na mwanadada Victoria, muda si mrefu Victoria ambaye yeye ni mwanamziki wa Kenya akatua nchini kwa ajili ya kurecord wimbo na wakina Diamond,



basi katika kurecord huko Wema akaanza kuona wivu mpenzi wake anavyoshinda studio sana na Victoria manake Victoria ni mrembo na anaweza kutishia amani ya mwanamke yeyote, sasa bwana naskia juzi Diamond akaondoka nyumbani na kumdanganya Wema kwamba anaenda kumuona mama yake, kumbe anaenda studio kuendelea kurecord na Victoria, basi kwa bahati mbaya naskia Ommy Dimpoz alipost picha zikiwaonyesha wako studio na Wema kuziona, basi Wema alifunga safari mpaka studio, wacha aangushe varangati, nakwambia ilikua mshikemshike,





basi timbwili hilo likaisha Wema akarudi nyumbani huku akiwa kakosana vibaya mno na Diamond manake naskia ilifikia hatua Diamond akamzaba Wema kibao. basi sasa jamani hiyo habari ilivyosambaa, huko instagram kuna page inaitwa tim....na.... yani mwenye hiyo page alifurahia Wema kugombana na Diamond, alifurahi na kuanza kusambaza habari kwamba Diamond na Victoria ni wapenzi, yani akawa analazimisha mambo jamani, basi ikafika kesho yake asubuhi Wema wacha akomeshe watu akatupia picha ya Diamond, kuonyesha kwamba pamoja na kwamba yeye na Diamond walikua na ugomvi lakini waliyamaliza na hawajaachana , picha hiyo alipost Wema iliambatana na ujumbe wa kuwaambia watu wawaache na mapenzi yao, wakigombana ni wao na wakipatana ni wao, haikupita muda shemeji Diamond nae akaachia picha ya Wema na yeye mwenyewe kwenye account yake ya Isnta na kuachia maneni yanayosema SHIIIIIIIII BADO TWALALA.


       WEMA NA DIAMOND ENZI HIZO DIAMOND AKIWA HANA KITU

No comments: