Tunaanza na Linda, nimemuweka humu kwasababu ni dada wa muigizaji Richard Bezuidenhout, Linda kama mnavyomuona, ni mama wa watoto wanne lakini ni mzuri kupita kiasi, yani ukiambiwa yeye amekamilika kila idara,SURA, MIGUU, SHAPE, RANGI YA MWILI, NYWELE, na nyongeza yake ni SMILE yake ya kukata na shoka. Ni mwanamke mchapakazi sana na anaishi Marekani, kwa wanaopenda mambo ya mitindo basi huyu ni mfano wa kuigwa.
LINDA BEZUIDENHOUT
Anaitwa Mange Kimambi, ni mama wa watoto watatu, mrembo, yupo makini na malengo yake, ni chanzo cha mastaa kadhaa wanaosumbua jiji, mmoja wa mastar hao ni WEMA SEPETU, yani huyu ndo aliyesababisha magazeti ya udaku yauze sana kwasababu kwa kumtoa kwake Wema Sepetu na kumsimamia mpaka akawa miss Tanzania, kumemfanya Wema kua star anayeuza sana kwenye kila kitu hasa magazeti kwa hiyo chanzo cha yote ni Mange ashukuriwe kwa hilo, Mange ni chapakazi sana na anajua sana kutangaza biashara, yani kwenye marketing tu Nampa mia kwa mia, anaishi Marekani kwa sasa.
MANGE KIMAMBI



Na huyu hapa chini ni my girllll SINTAH, huyu ni muigizaji, ni muigizaji alipitia mikononi mwa waigizaji hasa yani ni zao la wale waigizaji wakongwe ambao wengi hawapo hapa duniani tena, kwa hyo Sintah akiamua kuigiza HAUZI SURA KWENYE CAMERA BALI ANAJUA NINI ANAFANYA MBELE YA CAMERA, Sintah ni mwanamke aliyemudu kubaki kwenye umaarufu mpaka sasa japo kazi iliyomfanya awe maarufu kaicha kwa sasa, muda mwingi hajaigiza lakini bado yuko midomoni mwa watu tofauti na wenzake wengi walioacha kuigiza wamesahaulika, ni mama wa motto mmoja na ni mama mzuri sana tofauti na wengi wanavyofikiria au tofauti na wengi wanavyomsoma kwenye mitandao, Sintah anajua madhara ya media kwa watoto ndo maana kamwe hapendi kumuweka mwanae kwenye media, ni kama wasanii wengi wa nje wamekua wakiwaprotect watoto wao na mambo ya media na wengine wamekua wakikataa hata watoto wao wasipigwe picha na vyombo vya habari, MADHARA YA MTOTO WA MTU MAARUFU KUONEKANA KWENYE VYOMBO VYA HABARI AU MITANDAO NI MAKUBWA KULIKO WATU MNAVYOFIKIRI, MFANO NI MTOTO WA MUIGIZAJI KAJALA ANAVYOANDAMWA KWA KOSA LISILOMUHUSU NA WATU BILA HURUMA WANAISHIA KUMTUKANA HADI MTOTO MDOGO, KWA SINTAH NAFIKIRI ALIONA MBALI LAKINI MITAANI MUDA MWINGI UTAMUONA NA MWANAE. pia Sintah ni blogger, na mfanyabiashara, ni mwanamke ambaye hana makuu kabisa ni mwepesi mno kumzoea mtu.
SINTAH
Nawapenda wote hao wanawake hapo juu, wote ni mfano wa kuigwa japo wanamapungufu yao lakini wote ni wachakarikaji hawajajibweteka hata kidogo,
JE? WEWE WAMPENDA NANI KATI YA HAWA?